Nini nafasi ya biogas Tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini nafasi ya biogas Tanzania?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by babayah67, Jun 15, 2011.

 1. babayah67

  babayah67 JF-Expert Member

  #1
  Jun 15, 2011
  Joined: Mar 28, 2008
  Messages: 493
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Nimepitia hotuba yote ya bajeti ya kambi ya Upinzani pamoja na ile ya Serikali ya wiki iliyopita. Zote kwa pamoja zinafanana katika mtazamo wa namna ya kuondokana na tatizo la uhaba wa nishati. Bajeti zote mbili zinajikita saana katika kufikiria vyanzo vya nishati kama umeme wa maji, na umeme unaotokana na Gesi. Kuna chanzo kimoja rahisi saana ambacho si upinzani au serikali wamejaribu kukiangalia na kukiwekea msisitizo. Chanzo hiki ni BIOGAS. Biogas ni nishati inayotokana na mabaki ya uchafu wa vitu mbalimbali kama takataka za viwandani, mabaki ya mazao ya mashambani na hata takataka toka mitaani na masokoni mwetu. Ukiwa na biogas unaweza kuitumia kwa kupikia, na pia unaweza kuitumia kwa kuzalisha umeme na hata kwa kuendeshea magari. Kwa waliobahatika kufika nchi kama Sweden au Denmark watakuwa wamejionea haya, kwani kwa nchi kama Sweden Mabasi yote yanayotumika kusafirishia abiria mijini yanatumia biogas 40% ikichanganyika na natural gas 60%. Kama nchi Sweden lengo lao kufikia 2020 ni kuwa na karibu 20% ya umeme utumikao humo unaotokana na biogas. Kutokana na teknolojia iliyopo hili linawezekana hata hapa kwetu kama tu Serikali itaamua kwa dhati kuwekeza katika hili. Kwa waliopo Tanga, Hale watakuwa wananielewa zaidi nachoongea maana katika kiwanda cha Katani cha Hale, wameweza kuzalisha umeme kutokana na mabaki ya mkonge ambayo awali walikuwa wakiyatupa tu,(Ambayo wanazalisha kila ukicha tani nyingi tu) umeme ambao wanatumia kuendeshea mitambo yao na ziada wanatumia majumbani mwao na kuwauzia wanakijiji wanaowazunguuka. It is high time now serikali yetu ikaliona hili kuwa ni moja ya solution. Utaalamu wa kisayansi kuhusu uzalishaji wa biogas upo hapa nchini, Tafiti nyingi zilishafanyika kuhusu vyanzo mbalimbali toka majitaka ya viwandani, majumbani, mabaki ya mazao, mabaki ya taka masokoni hadi kwenye mabaki yatokanayo na uchafu wa viwanda vya samaki.
   
 2. Yohana Kilimba

  Yohana Kilimba JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2016
  Joined: Dec 25, 2012
  Messages: 8,132
  Likes Received: 5,211
  Trophy Points: 280
  Hivi naweza kupata umeme kupitia mavi ya ng'ombe?
   
 3. K

  Kadanga Senior Member

  #3
  Aug 13, 2016
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 138
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Mimi nanaweza tengeneza mtambo wakutumia Bio-gas kwagarama nafuu sana call 0625791258
   
Loading...