Nini mtazamo wako baada ya kurudi nyumbani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini mtazamo wako baada ya kurudi nyumbani?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kwame Nkrumah, Dec 30, 2008.

 1. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #1
  Dec 30, 2008
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Mara nyingi sana tunasikia viongozi wetu wakiwa wanazungumza na Watanzania nje ya nchi, Botswana, Afrika Kusini, Canada, UK na kwingineko wanashauri sana vijana warudi nyumbani kusaidia juhudi za kujenga Taifa.
  Lakini mimi binafsi nimesikia tofauti kidogo kutoka kwa ndugu na jamaa waliofuata ushauri huu. Kwamba fursa hiyo ya kujenga taifa baada ya kurudi hawaipati !!!! Ndugu mmoja alisoma mambo ya computer nje na kufanya kazi hiyo kwa miaka 7 nje. [ ni mtaalamu wa kutisha wa IT } Akaamua kurudi nyumbani kusukuma gurudumu la maendeleo kama wakubwa walivyosihi, lakini baada ya muda alirudi tena na kusema ameshindwa kufanya kazi nyumbani na kwamba atarudi baada ya kustaafu !!
  Mwingine alisoma mambo ya masoko, akapata kazi shirika la umma, lakini bosi wake alimnyanyapaa sana. Jamaa akitoa mawazo mapya bosi anasema anataka kumnyang'anya kazi au anafanya kazi kwa sifa. Sasa yeye hana uwezo wa kurudi nje alikokuwa. Inabidi awe hapohapo huku manung'uniko hayaishi. Na kutusihi sisi " jamani msirudi".
  Jamaa mwingine akaniambia kama siku hizi nina lafudhi ya Ki-Kenya basi nirudi nyumbani !!!Maana hao ndio wana kazi zote nzuri.
  Tupatie experience yako baada ya kurudi.
   
 2. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #2
  Dec 31, 2008
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Ati nini? Kurudi? Muzee naona unaleta utani sasa.

  Kama una-plan kurudi ili uajiriwe ktk public au private co. ujue unataka kufa masikini.
   
 3. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #3
  Dec 31, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Anataka kujua mtazamo wako kama umerudi na kuwekeza maisha yako bongo..! Kama bado upo ughaibuni bandiko hili ni kulitizama na kulipita tu...
   
 4. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #4
  Dec 31, 2008
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Ebo we vp?

  ..Nachangia popote nionapo panafaa..Si lazima ujumbe wangu umsaidie aliyeleta bandiko tu..hata yeyote asomayo hii thread. Thread haianzishwi kwa ajili ya manufaa ya mtu mmoja au kama vp atumie PM basi. This a public domain.

  Nadhani umenielewa...
   
 5. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #5
  Dec 31, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Kuna ndugu yangu alisomea Computer Science na kupata masters; yeye hakutaka kulowea ughaibuni, hivyo alipomaliza masomo yake akarudi Tanzania moja kwa moja. Kufika huko akawekwa accounting department ya Wizara ya Ulinzia kuwa anashughulika na vitabu vya mahesabu. Kwa vile alikuwa hajui kazi hiyo akaonekana kichekesho idarani na kuwa frustrated sana. Akakimbilia Australia ambako sasa hivi ni Manager wa IT Services kwenye kampuni fulani
   
 6. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #6
  Dec 31, 2008
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Mimi nimerudi kama mara tatu. Hivyo ninatoa mtazamo wangu. Kwanza kusoma nje kuna matatizo yake hata kama utakuwa katika shule nzuri au bingwa wa IT kama mshikaji wako. Unakosa mtandao au Network. Kama unachukua undergraduate nje ya nchi utakuwa na marafiki katika shule uliyosomea. Na wale wanaosoma UDSM watakuwa na mtandao wao.

  Vilevile kuna watu wanaosoma nje ya Tanzania wanaofikiri kuwa wanapoondoka Tanzania basi maisha ya watanzania yamesimama. Ukirudi Tanzania unaweza kumkuta yule mtu uliyekuwa unampa tution kwa sababu shule haipandi amekuwa bosi.

  Vilevile kama mnataka kuisaidia nchi basi ipeni nchi nafasi. Elimu yako ya nje inaweza ikakupa nafasi ya kazi haraka au vilevile ikakuletea matatizo ya kupata kazi.

  Anyway kama wewe ni bingwa wa IT na huko Marekani, kwanini uende bongo kutafuta kazi ya ajira? Huo ubingwa wako nitakuwa na mashaka nao. Tumia ubingwa wako, tengeneza mtaji wa kutosha na rudi bongo ku-invest.
   
 7. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #7
  Dec 31, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Wewe ndio ujanifahamu,
  Yeye anataka mawazo ya WaTz walioishi ughaibuini na kurudi Tz ili kujenga Taifa. Hawa ni wale Wazaelendo waliokubali kujenga nchi kwa kutumia ujuzi na maarifa yao waliyopata wakiwa nje ya TZ.

  Sasa kama wewe bado hujawa Mzalendo halisi bandiko hili halikufai, na hicho kiswahili cha kukopi kwa wazaramo hakina nafasi katika bandiko hili...
   
 8. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #8
  Dec 31, 2008
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Uelewa kumbe ni zawadi adimu na adhimu kiasi hiki?..

  Narudia tena.. Hii thread si kwa ajili ya manufaa ya mtu aliyeanzisha thread pekee..

  Au na hii m'bado?
   
 9. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #9
  Dec 31, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Unapenda ligi wewe, umehusu ukumbi wa dini nini?
   
 10. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #10
  Dec 31, 2008
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Ligi ya kitu gani?..mtu ameanzisha thread kuhusu kinachomsibu yeye na watu wengine , wewe unaanza kutuwekea stds za kuchangia, eti ooh kama upo ughaibuni bado hujarudi bandiko halikuhusu, mleta thread amekuajiri uusemee moyo wake?.. Kati ya wewe na mimi nani anayetaka ligi sasa? Ya Ukumbi wa deen unaingiaje hapa?
   
 11. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #11
  Dec 31, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Naona amekuajiri weye ...:D


  Usimchokoze simba kwa spidi ya baiskeli!
   
 12. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #12
  Dec 31, 2008
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,122
  Likes Received: 617
  Trophy Points: 280
  Msiharibu thread mazee!!!
   
 13. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #13
  Dec 31, 2008
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160

  Bua ha ha ha...

  Haya bwana..Naona umesahau kuwa tunahitaji michango kuhusu mada husika kama ulivyodai: na wala si mikwara mbuzi na utoto-utoto..


  Wasaalam
   
 14. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #14
  Dec 31, 2008
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,122
  Likes Received: 617
  Trophy Points: 280
  Personally nadhani kurudi na kuingia Serikalini ni mistake, lazima uende private sector. Pia kuna tofauti kama unarudi straight ukimaliza masomo na kurudi una experience sana, ukiwa una experience unaweza ukajikuta kazi za huku hazikuchalenge na hazipo as fulfilling.

  Also a lot of times its who you know, not what you know.
   
 15. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #15
  Dec 31, 2008
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Hii hoja ndio haswa sababu iliyonisukuma kusema kuwa mtu kama upo ughaibuni na upo serious na career yako, unakamata hata kama ni bingo mbuzi..haitakaa vizuri ukirudi bongo. Utaratibu wa ajira bongo ni kujuana na kazi zinazolipa kufuatana na ukali wa maisha ni za kuhesabika..wengi wanaishi kwa madeni tu...

  Ukitaka kujua hali ya wafanyakazi bongo ni mbaya jaribu kudodosa savings mtu anazofanya. Mathalan, mzee wangu alipostaafu alikuwa tayari ameshafunga kitabu chake cha benki maana hamna cha ku-save wala nini. Kupokea mafao ilibidi iwe kimbembe cha kufungua akaunti upya..Habari ndo hiyo..

  Kibs upozz?
   
 16. Maarifa

  Maarifa JF-Expert Member

  #16
  Dec 31, 2008
  Joined: Nov 23, 2006
  Messages: 2,880
  Likes Received: 1,051
  Trophy Points: 280
  Baada ya kusoma maoni ya watu hapa, it seems kuna contradictions ya mawazo. However majority supports kutorudi. However there are lods of factors ambazo zitampa mtu uwezo wa kupata kazi nzuri ama la even if umesoma nje ya Tanzania.
  1. Kuna mtu amesema mtandao (who are U? Unamjua nani) is afactor kwa Tanzania,
  2. How competent are U. Maana kusoma nje si kigezo cha wewe kuwa competent na hivyo kupapatikiwa
  3. Je elimu hapa tunayoongelea ni kiwango gani? Certificates, Diplomas, undergraduates, Masters or PhDs. Maana kila kiwango cha elimu kina nfasi tofauti, Also umesoma nini. Kuna mchangiaji emeandika hapo juu mtu kasoma IT anakuwa mhasibu! simply kwa sababu kasoma nje. That is wrong.

  Either kuna waliosoma Tanzania ama hawajasoma kabisa. Lakini maisha yamewanyokea sana sometimes lucky or 'BONGO' Sasa mtoka ulaya au marekani Bongo ya ubabaishaji huna sometimes you may not fulfill yr dreams. Maana hujazoea ubabaishaji. Kwa you just conclude kuwa Tanzania ni ngumu. But I know few people who are now saying they have wasted their time for staying abroad too long . walipofika Tanzania wamechupa! By the way hawafanyi kazi serikalini!!!!! maana watafunga account kabla ya kustaafu.
   
 17. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #17
  Dec 31, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Wandugu najua mnatetea nafsi za familia zenu na za kwenu binafsi lakini kwa mtazamo wangu ukweli unabaki pale pale kuwa kumbukeni mlipoenda kusoma huko ughaibuni baadhi yenu mlisoma kwa pesa za walipa kodi wa bongo kiasi kwamba tunategemea angalau mkimaliza hizo shule zenu mrudi bongo kuendeleza uchumi na mambo mengine.

  Lakini nasikitika kuona wengi mmekuwa waoga wa kurudi kwenu kwa kisingizio cha kuogopa hali mbaya (eti hakuna ajira n.k.). Hivi tuchulie katika miaka 10 ijayo wote watakaoenda kusoma nje wasirudi bongo mnadhani mwisho wake ni nini?? Mjenga nchi ni mwenye nchi, huo ufisadi na hali ngumu nyingine mnazoziogopa nyie ndio mnaotegemewa kuja msimame kidete kuweka mambo sawa. Kumbukeni kama nyie mlibahatika kwenda huko, mna ndugu zenu waliobaki huku ina maana mko tayari wao waendelee kupondeka eti kisa mnaogopa kurudi kwa kukosa ajira?

  Mbona rebels wanaingia misituni kupigana ili kukomboa nchi zao ambazo wanaamini zinaendeshwa ndivyo sivyo? sasa kama wangeamu kukimbia na kukaa kimya ughaibuni kwa kuwa tu wao wako salama maisha yangekuwaje? Mjue itafika mahali fulani lazima kikundi fulani cha watu ki-sacrifice nguvu na uhai wao ili kujikomboa na pia kuwakomboa watakaokuja sio kukimbia...

  Pia muwe na broad mind jamani haya mambo kuwa lazima ukitoka kusoma nje ukirudi lazima uajiriwe na kupewa li-post kubwa sijui Director, Manager etc, hivi huo ujuzi na uzoefu wako una uhakika utakuwezesha kufanya kazi za watu au ndio mnadaka tungo tu na nyie mnaimba bila kujua mantiki ya wimbo? Hata hapa Tz kuna vyuo vinatoa watu wenye uwezo wakati mwingine kushinda hata nyie mliotoka ughaibuni mnaowanaje hawafai? Hivi ukienda China, Japan au India hao wanaondeleza nchi zao ni wageni au wenyeji? Nyie mnakimbia kupigania na kujenga nchi yenu mnataka nani awafanyie hayo mambo? Mnapenda mtafuniwe mkija mnakula tu na kupenda good time bila kutoka jasho? Tukikimbia wote itakuwa vipi?

  Mambo ya kufunga akaunti ya benki kabla ya kustaafu ni mipangilio ya mtu mwenyewe ( Refer thread ya George Liundi) kama unafanya kazi na kipato unapata ni juu yako kuji-savia kwa manufaa yako ya baadae kumbuka kuna watu walikuwa wakurugenzi, Makatibu wakuu wa wizara, Mawaziri lakini leo wengi wao ni choka mbaya kisa walipokuwa madarakani ufuska na ulevi viliwajaa wakadhani pepo iko siku zote..Na wewe Je???
   
 18. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #18
  Dec 31, 2008
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mnaposema watanzania wanapomaliza shule nje wanapaswa kurudi nyumbani kujenga nchi hivi wakuu mnaamanisha mnachosema au mmekariri tu huo msemo?Hivi ukipata kazi nje hata isiwe nzuri sana lakini walau ukawa una save na kuwatumia kina mjomba na shangazi dola kadhaa kila mwezi ili wasomeshee watoto wao unakuwa hujengi nchi?Unakuwa siyo mzalendo mpaka nawe urudi ukanyanyaswe na mafisadi pamoja na taaluma yako safi?
  Huko bongo tunasikia kila siku kuwa kazi ni za shida.Watu wanamaliza mlimani wanaendelea kula msoto,nyinyi mnasisitiza turudi.Sasa tukirudi wote patatosha hapo kweli?
  Mimi nawashauri wabongo wote walioko nje kama una kazi ambayo inakuwezesha kusave na kufanya ka investment fulani bongo kama nyumba(for future)na kusaidia ndugu zako wala usikimbilie kurudi otherwise kama una godfather au baba ako fisadi fulani basi nenda manake uhakika wa kukamata kazi BOT unao!!
   
 19. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #19
  Dec 31, 2008
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Mukulu Laligeni,

  Hili suala la kufunga akaunti naona hukulielewa kwa mapana yake. Hapa nazungumzia ukweli kwamba wafanyakazi wengi bongo wana hali mbaya na wanaishi kwa madeni kutokana na kipato kisichoendana na gharama halisi za maisha achilia mbali kuwa na surplus. Nasema haya nikiwa kama mfanyakazi na ka - experience ninako, wengine tunafikia hatua hadi mama lishe tunawapiga mizinga huo ndo ukweli.

  Nilijaribu kutoa mfano wa mzee wangu kama mfano halisi kwa sababu nazijua nyendo zake na najua hana makeke yeyote ya 'kuwekeza kwenye vibanda' wala 'kufungua baa'.. ni hivyo maisha bongo bakora muzee. Angependa sana afanye savings lakini ndo hivyo tena .. nakumbuka enzi zile anatupeleka skuli hususan boarding, gharama za vitabu na ada (ya shule ya serikali) ilikuwa haitimii mpaka abembelezwe bosi atoe mkopo kazini. Hiyo ni kudhihirisha kuwa kipato cha mfanyakazi wa kawaida ni kituko.
   
 20. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #20
  Dec 31, 2008
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mtarajiwa, Mimi mpiganaji halisi. Na mpiganaji halisi apigwi risasi ya kichogoni. Najiandaa kwenda kujenga taifa, Mimi mzalendo halisi naenda kuicheza hiyo ngoma ya mabadiliko nikiwa ndani ya nchi yangu kwani utamu wa ngoma sharti uingie na si kuishi katika ulimwengu wa kufikirika. Naenda kuwa mpambanaji! Haya shime vijana twende tukaibadilishe nchi yetu na si kupiga kelele ngoma yenywe twaogopa kuicheza.
   
Loading...