Nini maoni yako: Serikali Kuipiga mifuko ya Plastiki Marufuku

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,850
Serikali imesema ina mipango ya kupiga marufuku kabisa matumizi ya mifuko ya plastiki ambayo inachangia uchafuzi wa mazingira

Waziri wa Mazingira, January Makamba alisema serikai imeagiza maafisa katika Baraza la Usimamizi wa Mazingira la Taifa (NEMC) kutengeneza mpango wa jinsi ya kukabiliana na utupaji wa mifuko ya plastiki nchini.

Afrika Mashariki ni Rwanda tu iliyopiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki tangu mwka wa 2008.
 
Kwani si ilishapigwa marufuku......... au lile agizo lilishatenguliwa ???????
 
Serikali imesema ina mipango ya kupiga marufuku kabisa matumizi ya mifuko ya plastiki ambayo inachangia uchafuzi wa mazingira

Waziri wa Mazingira, January Makamba alisema serikai imeagiza maafisa katika Baraza la Usimamizi wa Mazingira la Taifa (NEMC) kutengeneza mpango wa jinsi ya kukabiliana na utupaji wa mifuko ya plastiki nchini.

Afrika Mashariki ni Rwanda tu iliyopiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki tangu mwka wa 2008.
Makamba anatakiwa kutafuta njia ya ku recycle uchafu. Nchi zilixoendelea zinapunguza matumizi ya mifuko ya plastic na wkt huo huo wana njia mbadala ya recycling.
Tatizo viongozi wa Tanzania wanachanganya siasa na responsibilities zao km viongozi wa nchi.
 
Walisema sijui microns ngapi za hayo mamifuko ndo zinaruhusiwa tunaona bado rambo nyepesi zipo wafute tu maana hamna namna sasa
 
Mifuko hiyo ni sehemu ndogo sana ya mambo yanayotakiwa kushughulikiwa kama kweli Waziri ana nia ya dhati kuondoa kabisa tatizo la uharibifu wa mazingira, bado kuna changamoto kubwa sana
  • Viwanda kutiririsha maji yenye sumu kwenye mito inayotumiwa na binadamu pamoja na mifugo (Mf. ni ule mto unaopita mjini Morogoro kutokea Mindu na ule unaotokea Mjini kule inakokutana kuna viwanda vinamwaga maji taka huku mbele yake zaidi binadamu na mifugo wakiyatumia kupikia na kunywa
  • Halimashauri za miji zimeshindwa kuondoa takataka katikati ya miji, kwenye masoko na stand za mabasi, mitaro imeziba na machinjio zilizopo mijini nyingi zinatiririsha maji machafu mitaani na barabarani
  • Magari mengi mijini yamechoka yanatoa moshi mwingi sana kiasi kwamba hata baadhi ya maeneo unakuta majani ya miti na nyasi kandokando ya barabara zina masizi ya moshi wa magari
  • Ukataji wa miti hovyo (kama micharaka) hukohuko jiji kasoro bahari, uchomaji wa mkaa, umekithiri kiasi kwamba maeneo mengi yamekuwa jangwa.
  • Kelele za muziki kwenye makazi ya watu, kelele zinazotokana na bodaboda kutoboa mabomba ya moshi kwenye pikipiki zao, viwanda vya kufyatua matofari ya cement kwenye makazi ya watu, mashine za kukoboa mpunga kwenye makazi ya watu, uchomaji wa taka hovyo na hasa hizo za nailoni na chupa za maji na makopo ya sumu za kuulia wadudu havipigiwi kelele na mamlaka husikajapo ni miongoni mwa matatizo yanayotakiwa kufanyiwa kazi haraka zana kutokana kuathiri moja kwa moja afya za raia.
 
Serikali imesema ina mipango ya kupiga marufuku kabisa matumizi ya mifuko ya plastiki ambayo inachangia uchafuzi wa mazingira

Waziri wa Mazingira, January Makamba alisema serikai imeagiza maafisa katika Baraza la Usimamizi wa Mazingira la Taifa (NEMC) kutengeneza mpango wa jinsi ya kukabiliana na utupaji wa mifuko ya plastiki nchini.

Afrika Mashariki ni Rwanda tu iliyopiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki tangu mwka wa 2008.
Hakuna kitakachifanyika hii kitu inajirudiarudia Lakini utekelezaji zero! Wazenji wameweza sisi tumebaki na matamko
 
Wapige marufuku tu....turudi kwenye zama za mifuko ya karatasi....zanzibar walishaanza...
Nevertheless , resistance should be anticipated....watu wamewekeza kwenye hiyo biashara.
 
Wachina watafanya fitina ya hela na ndugu zao wahindi manake Ndio wenye viwanda vingi vya hii bidhaa
 
Safi sana Waziri Makamba, hali ilishakuwa mbaya sana, Hebu fanya random walk katika miji yetu unaweza kulia machozi jinsi hali ilivyo mbaya, mitaro imeziba, Vyanzo vya maji, Mitaa, Soil quality, hivi vyote vimeathiriwa sana na plastic bags, Fanya hima mheshimiwa waziri, Nakuunga mkono 100/100
 
Bila kubeza juhudi zinazoendelea za ukusanyaji taka katika miji yetu, zoezi hili ili liwe na matokeo makubwa zaidi inabidi:

1. Zoezi hili liende sambamba na mufunzo kuhusu suala zima la Waste management

2. Waste Management is not simply collection of wastes

3. Waste management inahusisha waste segregation i.e decomposabel , non decomposable, hazordous etc

4. Kila category ya waste ina namna yake ya ku- dispose

5. It is not recommendable to have open dumping, of waste and opening burning as it creates air pollution

6. It was clearly observed that wakati wa usafi open burning of waste ilifanyika kila sehemu ya mji na kusababisha moshi mzito

7. Mifuko ya plastic inayotumika sana kwa ajili ya shopping - badala ya kupiga marufuku serikali inaweza kuwalazimisha wazalishaji wakajenga simple recycling factories ambazo zitatoa ajira kwa waste collectors na waajiriwa kwenye viwanda hivi- scenario hii menza kuonekaana kwenye plastic bottles used for drinking water na soda

8. Liquid waste management pia inabidi serikali iangalie kwani kuna viwanda vingi sana vinapeleka effluents kwenye environment, pia domestic liquid waste zinapelekwa sana kwenye mazingira bila utaratibu.

Kwa sababu tumeanza.... basi tuwe na haya kichwani kama tunataka kuwa na proper waste management program kwa ajili ya nchi na mitaa yetu
 
Naona CCM bado haijajifunza kuhusiana na permanent solutions to problems, bado wanakimbilia kutumia quick fix approach to problem solving. Hapa serikali wanatakiwa waandae bajeti ya kununua magari maalum ya kuzolea takata ngumu pamoja halafu zitawanywe ktk halmashauri za manispaa mbalimbali hapa nchini kwaajili ya kupita maeneo mbalimbali ya miji na majiji kukusanya uchafu.Pia zinunuliwe dustbins nyingi za kutosha zitakazoweza wekwa ktk mitaa mbalimbali ya miji na majiji kama vile barabarani,kwenye stendi za daladala,kwenye masoko,shuleni,vyuoni.Pia ktk mitaa ziwekwe dustbins kubwa zile kwaajili ya matumizi ya households ambapo yale magari maalum ya taka yatakuja kuchukua taka kutoka ktk hayo mapipa.Hayo magari ya taka ninayoyazungumzia siyo haya malori ambapo wafanyakazi wake hutumia koleo kupakia taka!?ninazungumzia yale magaria ambayo yana uwezo wa kuyanyanyua mapipa ya taka yenyewe,kwa waliowahi kuishi Namibia na South Africa wanajua hayo ninayoyazungumzia.Wakifanya hivi nitaona kweli serikali imedhamilia kuweka miji yetu ktk hali ya usafi.
 
Mifuko hiyo ni sehemu ndogo sana ya mambo yanayotakiwa kushughulikiwa kama kweli Waziri ana nia ya dhati kuondoa kabisa tatizo la uharibifu wa mazingira, bado kuna changamoto kubwa sana
  • Viwanda kutiririsha maji yenye sumu kwenye mito inayotumiwa na binadamu pamoja na mifugo (Mf. ni ule mto unaopita mjini Morogoro kutokea Mindu na ule unaotokea Mjini kule inakokutana kuna viwanda vinamwaga maji taka huku mbele yake zaidi binadamu na mifugo wakiyatumia kupikia na kunywa
  • Halimashauri za miji zimeshindwa kuondoa takataka katikati ya miji, kwenye masoko na stand za mabasi, mitaro imeziba na machinjio zilizopo mijini nyingi zinatiririsha maji machafu mitaani na barabarani
  • Magari mengi mijini yamechoka yanatoa moshi mwingi sana kiasi kwamba hata baadhi ya maeneo unakuta majani ya miti na nyasi kandokando ya barabara zina masizi ya moshi wa magari
  • Ukataji wa miti hovyo (kama micharaka) hukohuko jiji kasoro bahari, uchomaji wa mkaa, umekithiri kiasi kwamba maeneo mengi yamekuwa jangwa.
  • Kelele za muziki kwenye makazi ya watu, kelele zinazotokana na bodaboda kutoboa mabomba ya moshi kwenye pikipiki zao, viwanda vya kufyatua matofari ya cement kwenye makazi ya watu, mashine za kukoboa mpunga kwenye makazi ya watu, uchomaji wa taka hovyo na hasa hizo za nailoni na chupa za maji na makopo ya sumu za kuulia wadudu havipigiwi kelele na mamlaka husikajapo ni miongoni mwa matatizo yanayotakiwa kufanyiwa kazi haraka zana kutokana kuathiri moja kwa moja afya za raia.
vituo vya kuuza petroli vilivyojengwa karibu na makazi ya watu
 
Serikali imesema ina mipango ya kupiga marufuku kabisa matumizi ya mifuko ya plastiki ambayo inachangia uchafuzi wa mazingira
Waipige marufuku tu! Haina msaada wowote zaidi ya kuharibu ardhi na kuua mifugo!

Turudi kutumia mifuko ya karatasi!

Afrika Mashariki ni Rwanda tu iliyopiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki tangu mwka wa 2008.
Na hawana takataka kama hizo.
 
TEKNOLOJIA umenena ukweli ktk issue ya kufanya nchi iwe safi. Lakini hii mifuko ni haribifu sana aisee. Na waiondoe tu. Kipindi kile walitaka kuitoa sijui hata nini kilitokea serikali ikanywea. Ilinisikitisha sana!
 
Kaka Gamba la Nyoka
Naunga mkono post yako yenye hoja fupi zenye busara, mifuko ya plastiki ni moja ya majipu uchungu, yanapaswa yapasuliwe na wakati muafaka ni sasa.
 
Back
Top Bottom