Nini manufaa ya bomba la mafuta kupitia Tanzania au Kenya?

respect wa boda

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
4,556
3,838
Guys habarini za jioni...

Kwasiku kadhaa sasa kumekuwa na sintofahamu juu ya sehemu haswa litakakopita Bomba la Mafuta ghafi toka Uganda. Nchi za Tanzania na Kenya kwa nyakati tofauti zimeonekana kila moja ikitaka Bomba hilo lipite kwake. Hali hiyo imezusha hofu baina ya Washirika hawa wa Jumuiya ya Africa Mashariki juu ya Mahusiano yao.

Sasa naomba kujua yafuatayo...

Mosi,
Nimanufaa yapi Nchi husika itayapata kwa Bomba hilo kupita kwenye Nchi husika? Ukiondoa manufaa hayo, Ni madhara gani yanategemewa kwa kupita kwa Bomba hilo kwenye Nchi husika?

Mbili,
Bomba hilo litagharamiwa na Nchi gani endapolitaruhusiwa kupita kwenye Nchi husika? Je litagharamiwa na Nchi mpitiwa na Bomba au Uganda mtoa Bomba?

Tatu na mwisho,
Ni kwanini vikao vifanyike kushirikisha Nchi zote tatu ikiwemo mbili zinazoshindania mradi huo? Kwanini isitathiminiwe na Uganda ambao hapa ndio wenye mradi kisha wao ndio waseme BOMBA LITAPITA Nchi fulani.

Wakuu viswali hivyo vichache vimekuwa vikiniumiza sana. Nikipata ufafanuzi itakua poa sana na nitakua nimeongeza uelewa kwa namna fulani. KARIBUNI

BACK TANGANYIKA
 
Duuuuuuuuuuuuuuhhh

Kwamba swali gumu, Majibu hakuna au uzi hauonekani?

BACK TANGANYIKA
 
Back
Top Bottom