Mtumishi Mkuu
JF-Expert Member
- Mar 31, 2011
- 259
- 93
Ndugu Nyanshani Ngabire wa Nshamba muleba, anasikitika kutangaza kifo cha mjomba wake Samaki Kiruru kilichotokea ziwani kwa ajali ya mtumbwi. Habari ziwafikie;
-Ndg Mapuli Kandambili wa Marekani
-Ndg Lusato Malyatabu wa Afrika ya Kusini
-Bi Hawa Mwampambuli wa Naijeria
Hilo tangazo hao watu kweli watalisikia au wanaolengwa kusikia ni watu gani? Zamani wakati mawasiliano ya simu yalikuwa mtihani ilikuwa inaingia akilini, lakini ulimwengu wa sasa mimi sioni umuhimu wa Tangazo la kifo redioni, labda kama kuna sababu nyingine.
Naona kama hii kidogo ina mantiki kwamba ni kwa ajili ya wale ambao sio walengwa wa moja kwa moja na msiba.Niliwahi kuwaza hivi lakini baada ya kutafakari sana nimebaini kuwa taarifa hizi zina umuhimu zaidi kwa third party…..unapomtaja Fulani bin Fulani kafa na habari zimfikie Mtoto wa Marehemu Fulani bin Fulani akiwa TRA Mbeya ni obvious kuwa huyu jamaa wa TRA alikuwa na taarifa ya simu nk lkn sisi marafiki zake tuliosoma naye au aliotuacha mathalan TRA mwanza hatukuwa na taarifa kuwa jamaa yetu kafiwa na baba yake….Pia majirani/wanakijiji wenzake ambao kwa sasa tupo Mtwara tunapata taarifa kuwa baba yake Fulani tuliochezea vifuu kula ngamiani kafariki.
Ni suala la mazoea na inategemea hao wenyeji huwa wanapendelea kusikiliza station gani ya radio mara kwa mara. Hebu jaribu kufanya na kauchunguzi uone matangazo mengi ya vifo Radio Free Africa yanawahusu watu wa pande zipi!Salamu zimfikie ndugu Chipumbu Kikubwa akiwa marekani!
Wakati hiyo redio hata huko Obamani haisikiki!
Halafu mbona matangazo mengi ya vifo katika Radio one yanatoka zile pande za juu