Nini majukumu ya wizara ya uwekezaji na uzezeshaji?

Noti mpya tz

JF-Expert Member
Mar 23, 2011
974
244
Wakati tunalia na matumiz makubwa huku jk akihofia kuigawa wizara ya maliasili na utalii kutokana na kutokuwa na bajeti kwa hili, kuna wiza ya Mary Nagu, uwezeshaji na uwekezaji.
Nini majukumu yake?
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Ivi wizara hii nayo ina katbu mkuu? na wanamwezesha nani? Hii ni dalili kuwa hatuna vipaumbele kawa taifa.

@Noti
 
1. Bado sijaelewa tofauti ya majukumu kati ya wizara hii ya Uwekezaji na uwezeshaji na Wizara ya viwanda na biashara?

2. Pia sijui majukumu ya wizara ya mahusioano iliyo chini ya Wassira.

3. Kuna Wizara ya wanawake na watoto - Hii inafanya nini? Inasaidiaje wanawake na watoto?

4. Wizara ya kazi - utani mtupu.

5. Kuna wizara ya katiba na sheria, sasa kwa nini tuwe na wizara ya utawala bora?
 
FJM hapo umezidi kunifungua macho, kumbe tuna wizara nyingi ambazo majukumu yake yanaingiliana na watu wanapiga dili tu...

@Noti.
 
mswali mazito haya
JK hana majibu.
mwaswahiba wengi, atawaweka wapi?
 
Back
Top Bottom