Nini madhara ya kutosomwa bajeti mbadala bungeni?

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,172
23,975
Kwa wale mnajua sheria na masuala ya kiuchumi naomba mnielimishe madhara kwa serikali kutokana na kambi ya upinzani kutosoma bajeti zao mbadala.

Jana Mbowe alisema kambi ya wapinzani haiwezi kusoma bajeti zao mbadala mpaka pale ofisi ya Spika itakapowapa wafanyakazi 12.

Nimesoma pia gazeti la Tanzania Daima linadai huo ni "Msimamo Mkali" kwa serikali.

Neno "Tamko Zito" limenifanya nitafute uelewa wa athari kwa serikali.

Je, kutofanya hivyo kutasababisha bajeti kutopita?

Je, bunge haliwezi kuendelea na shughuri zake?

Magwiji wa sheria naomba mnielimishe kwa sababu elimu haina mwisho!
 
Kioo huonyeshe mtu kwa mbele, kamwe hutojua nyuma umekalia vumbi limenata sehemu ya makalio, bajeti ya srikali itaonyesha mwelekeo ka mbele, bajeti ya upinzani itaonyesho mapungufu ya nyuma kwa hiyo kukosa kuwepo na bajeti ya upinzani ni sawa na mtu kavaa kaunda suti kumbe matako yako nje.
 
Hizo hizo bajeti kivuli zikitekelezwa huwa mnazipinga
 
Hata upinzani wasiposoma mabajeti haiana madhara kwa sababu bajeti ya awamu iko kichwani mwa mkulu. Anachotaka yeye ni kumsaidia kukusanya tu, kutumia hanashida ya kumsaidia kupanga. Kwanza watu wa kupanga matumizi wakiwa wengi wanasababisha ufisadi wa hela za umma.
 
Asilolijua Mbowe ni kususa kwao kumewapunguzia jukwaa huru na rasmi la wao kufanya siasa na kupata airtime ya media angalau kwa jambo la maana. Acha waendelee kususa mwisho wa siku ukiitaja CDM kwa wananchi inakuja picha ya vurugu, mahakamani na ubishi badala ya picha ya watu wanaotengeneza hoja bungeni.
 
Hiyo bajeti mbadala sijawahi kuona manufaa yake. Sababu wanachokifanya ni kumodify kidoogo kwenye figure na kujaza matusi ili waonekane wanajua kuongea huku shingo zimekakamaa kama "wanapiga bao".

Enzi za JK unakuta bajeti ya serikali ni trillion 18 wao wanaongeza moja inakuwa 19. Hawakuwahi kuja na bajeti hata ya trillion 25. Ameingia JPM akapaisha bajeti kwenda trillion 30 ghafla nao out of the blue wakaweka 31!!! Nyambafu kabisa!!! Kama siyo kukopi na kupesti ni nini hiki!??

Hakuna mbadala wowote ni ujinga tu!! Kama hawakuwahi kufikiria vyanzo vipya vya kodi kipindi cha JK ili kuonyesha umbadala Wenyewe hadi serikali ya JPM imekuja kuwafungua akili, hao wanasifa ya kuitwa mbadala kweli?!!

Wanatupotezea muda, waende zao huko na bajeti zao uchwara!!!
 
Mbona wachangiaji humu mnajibu swali hilo kama vile sio magreat thinker? Ni haibu sana, hivi kweli watu wamefikia hatua ya kushabikia kimahabamahaba hivi? Hamjui mifumo ya kibunge? Hamjui kanuni za Bunge zinavyosema?shame on you!!!!!!!
 
Tuambie wewe, umeshawahi kusikia nini kwenye bajeti mbadala ya kambi ya upinzani? Angalau Zitto alikuwa anatoa madini wakati bado yupo CDM, Mbowe form 6 failure ndio aongoze bajeti iliyojaa maono ya kiuchumi ya Taifa zima kwa mwaka, kweli form six failure kabisa ?
 
Jambo la kwanza, kipi kilipelekea kuwepo umuhimu wa hii bajeti mbadala.

Kwangu sio tu kwamba sioni umuhimu wa bajeti ya upinzani, sioni maana ya bajeti ya bunge na muhimili wote kwa ujumla.

Pesa tunayoiteketeza bungeni ni ndefu mno, hatupati faida kwenye huo uwekezaji.
 
Tanzania tumelogwa kabisa. Hatutaki challenge tunataka tuwe watu wa ndioooooo. Yaani mnashabikia upuuuzi na wote mnataka tuishi kwa kutumia akili ya moja.
 
Tanzania tumelogwa kabisa. Hatutaki challenge tunataka tuwe watu wa ndioooooooooooooooo pumbafu kweli. Yaani mnashabikia upuuuzi na wote mnataka tuishi kwa kutumia akili ya moja.
Mkuu lile li tochi linalikimbizwa nchi nzima ndilo linalotupumbaza. Ukishaliona tu, kwisha habari yako
 
Mipango ya nchi kwa kipindi hiki hupangwa na kikundi cha watu wachache sio Bunge so hakuna impact yoyote wacha maisha yasonge
 
Kwa wale mnajua sheria na masuala ya kiuchumi naomba mnielimishe madhara kwa serikali kutokana na kambi ya upinzani kutosoma bajeti zao mbadala.

Jana Mbowe alisema kambi ya wapinzani haiwezi kusoma bajeti zao mbadala mpaka pale ofisi ya Spika itakapowapa wafanyakazi 12.

Nimesoma pia gazeti la Tanzania Daima linadai huo ni "Msimamo Mkali" kwa serikali.

Neno "Tamko Zito" limenifanya nitafute uelewa wa athari kwa serikali.

Je, kutofanya hivyo kutasababisha bajeti kutopita?

Je, bunge haliwezi kuendelea na shughuri zake?

Magwiji wa sheria naomba mnielimishe kwa sababu elimu haina mwisho!
Nini madhara ya kutosoma bajeti ya serikali bungeni?
 
Back
Top Bottom