Nini maana ya wanyonge? (Weak, hopeless, & downtrodden)

Nini maana ya wanyonge? (Weak, hopeless, & downtrodden)

stinger_bug

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2019
Posts
856
Reaction score
1,716
Huwa natafakari sana Rais anapojitambulisha kuwa anaongoza watu wanyonge (weak, hopeless and downtrodden people).

Sielewi huyu rais ana mpango gani na hawa anaodai ni wanyonge. Labda ni mbinu ya kuwapumbaza wasiwe na ujasiri wa kuhoji lolote linalofanyika na serikali yake.

Binafsi ninaamini kumwita mtu mnyonge ni tusi kubwa sana. Ni sawa na kumwita mtu mlemavu. Asiyeweza lolote, asiyejitambua, na kadhalika.

Sijui watanzania wenzangu mnawaza nini mnapoitwa nyie ni watu hopeless, msiojitambua, msio na uwezo hata wa kujipigania, mnaoonewa, mdebwedo, nk?

Kwa kayli hizi, tutarajie watu hawa hawa eti wajenge viwanda? Tunatarajia mtoto anayeambiwa kuanzia anapozaliwa kuwa ni mnyonge eti aweze kuwa binadamu anayeweza kufanya mambo makubwa kwa dunia na nchi yake? Mnyonge ataweza kuipigania nchi yake anapoona inahujumiwa au imevamiwa kijeshi?

Binafsi nadhani wanyonge tulipaswa kuwaita wale wakimbizi ambao hawana makwao. Nachukizwa sana ninapoona mtanzania anaitwa mnyonge kisha anashangilia.
 
Mnyonge ni mtu yoyote asiyehoji lolote kuhusu serekali na anaamini atapata ahueni ya maisha. Na anachotakiwa ni kusifia chochote cha serikali na kiongozi wake huku akisubiri kuwa iko siku atakuwa na maisha bora.
 
Namshukuru Mungu mimi si mmoja wao. Wanyonge wote wako ccm. Hasa wale wanachama wa chini na wasiojitambua. Mwakilishi wao humu jukwaani ni ndugu yao Mikocheni Junction.
 
Binafsi nachukia hii kauli ya kuitwa mnyonge kwani inawapumbaza watu na kuwafanya too submissive kwa viongozi wanaowaita hivyo,cha ajabu watu wameshalizoea na ni sehemu ya maisha yao na wanafurahia kweli. Wasichokijua ni kuwa wanafanywa daraja tuu na wanufaika ni viongozi. Mimi binafsi sio mnyonge.
 
I rebuke the word mnyonge in Jesus name Christ ...Mimi sio mnyonge na sintokua mnyonge na zaidi sio miongoni wa wanaoitwa wanyonge na siongozwi na yoyote. Mungu ndio kiongozi wangu. Ana kura yangu kila siku kila wakati kila saa na kila mwaka.
 
Linachefua sana hilo neno...linatia kinyaaa....

Nafikiri twende na hashtag
#MimiSioMnyonge
 
Namshukuru Mungu mimi si mmoja wao. Wanyonge wote wako ccm. Hasa wale wanachama wa chini na wasiojitambua. Mwakilishi wao humu jukwaani ni ndugu yao Mikocheni Junction.
Na ni kweli huyo ndio mnyonge mwenyewe, tena ni senior mnyonge na kilaza wa ukweli
 
Mnyonge ni mwenye nguvu hafifu ya kiuchumi...asie na ushawishi wa kisiasa
 
I rebuke the word mnyonge in Jesus name Christ ...Mimi sio mnyonge na sintokua mnyonge na zaidi sio miongoni wa wanaoitwa wanyonge na siongozwi na yoyote. Mungu ndio kiongozi wangu. Ana kura yangu kila siku kila wakati kila saa na kila mwaka.
Mungu ana kura yako...kwamba ndo imemuweka hapo alipo?
 
Mheshimiwa Rais Magufuli yupo sahihi kwa 100%. Watz wengi wenu ni wanyonge ndio maana tunahitaji Rais aliyelelewa katika tabaka la watawaliwa aje afanye mabadiliko yatakayopelekea wananchi wengi walio wanyonge waweze kupata nafuu.

Kwenye hilo tuko tayari abadilishe mihula ya uongozi na kutawala kwa miaka mingi zaidi hadi pale watz watakapoacha unyonge.
 
Kwanza Rais kuita raia wake wanyonge ni kuwakosea heshima wananchi wake,

Sijawai kusikia Rais yeyote duniani akiwaita wananchi wake wanyonge"
Tangu lini mtu kuambiwa ukweli ikawa kukosewa heshima.
Anachofanya magufuli ni kuwapa black and white yaani yeye harembi kitu kama mlivyozoea . Sisi ni wanyonge period. Kama kusingekuwa na wanyonge Leo hii Lisu angeweza kuhakikishiwa ulinzi na angeweza kurudi bongo au zile chaguzi za maradio wale wahuni wa ccm wasingepata ubunge.
 
Mheshimiwa Rais Magufuli yupo sahihi kwa 100%. Watz wengi wenu ni wanyonge ndio maana tunahitaji Rais aliyelelewa katika tabaka la watawaliwa aje afanye mabadiliko yatakayopelekea wananchi wengi walio wanyonge waweze kupata nafuu.

Kwenye hilo tuko tayari abadilishe mihula ya uongozi na kutawala kwa miaka mingi zaidi hadi pale watz watakapoacha unyonge.
[emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom