Rais wa wanyonge maana yake nini?

Fall Army Worm

JF-Expert Member
Jan 8, 2015
9,915
2,000
Wakuu poleni na majukumu ya Ujenzi wa Taifa.Km kichwa kinavyojieleza,nipo nasikiliza wimbo wa Harmonize a.k.a Konde boy, ule ambao anamsifia Mkuu wa nchi.Kuna sehemu nimesikia akisema,Magufuli ndo Rais wa Wanyonge,nikajiuliza Wanyonge ni akina nani?.Nilijiuliza swali hilo kutokana na mambo kadhaa,km ifuatavyo.

1.Harmonize kuna sehemu anamsifu mheshimiwa kwa kutumbua watumishi,lkn anasahau kuwa Watumishi waliobaki na kuendelea kuchapa kazi hawaja kumbukwa na Serikali,matharani kupanda madaraja,mishahara,na stahiki zingine,je hawa wanaotiza wajibu wao vizuri na hawana namna ya kudai madai yao sio Wanyonge?

2.Wakati ule wa tumbua tumbua,hasa kwenye ishu ya Vyeti kwanini Jeshi halikuguswa?,Kwanini waliguswa hao ambao hawana chochote cha kuidhuru nchi kiusalama?,je hao walioguswa kwasababu tu hawana ubavu wa kuifanya chochote Serikali sio Wanyonge?.

3.Jana nimemsikia mheshimiwa akiwa Tunduma,akisema kuwa"Atawapelekea maji tu ikiwa watampelekea mbunge na diwani wa chama chake",kauli hii si ya Mara ya kwanza kutolewa,Je,kuwaumiza watu kwa kutowapelekea huduma za kijamii wakati ni haki yao kwa kuwa nao wanalipa kodi,ndio kujali Wanyonge?, Ni Wanyonge gani wanaozungumziwa?.

4.Siku hizi Wakulima wa baadhi ya mazao ya biashara wanapangiwa pa kuuza mazao yao km vile kahawa,wakati wa kulima wanapambana wenyewe,sasa ni Mnyonge gani mnayemzungumzia kuwa mkuu amemjali?

5.Ishu ya Vitambulisho vya machinga,nashukuru sasa imewekwa vizuri,km itabaki hivyo hata baada ya uchaguzi kuisha itapendeza.

Yapo mengi ya kuhoji lkn wacha kwa leo niishie hapa.Nimewahi kusoma habari za Rais Maskini Duniani aitwaye Jose Mujica,alimaarufu Pepe,Rais mstaafu wa Uruguay huyu ana unyenyekevu wa hali ya juu,na ukiambiwa ni Rais wa Wanyonge unakubali.Inawezekana Harmonize aliimba tu ili kuweka sawa Vina vyake au kumfurahisha mzee bila kujua kuwa kuna kundi kubwa la watu wanaolia machozi ya damu kwasababu ya hali ngumu ya maisha kutokana na mifumo kuwa migumu,si unajua tena "Aliyeshiba hamjui mwenye njaa".

Mimi sipo chama chochote cha siasa ila napenda sana Ukweli,Penye NYEUSI,tuseme hapa ni nyeusi,na penye NYEUPE tuseme hapa ni nyeupe.Kumwambia Ukweli Mtawala si dhambi,mbona Mungu aliye mkuu tunamwambia UKWELI, tukiwa ktk hali ngumu au nzuri tunafunguka mbele yake,sasa sembuse Kiongozi wa nchi mwanadamu tu,aliye hai leo na kesho anakuwa marehemu??!!!!.
Inawezekana mimi si mzuri wa kiswahili ktk kujua maana ya " Rais wa Wanyonge".Wajuzi wa mambo njooni tuwekane sawa.
 

mng'ato

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
28,624
2,000
Ukitaka kujua Rais wa wanyonge anawajali watu wake fuatilia pesa yako nssf,hapo ndipo utaelewa somo vzr.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom