Kwa kweli mimi nafikiri kwamba kuwa "mhafidhina" kunabeba wazo la kuhifadhi mambo yanoyodhaniwa ni yenye ubora maishani. Zaidi ya hayo, mtu mhafidhini hukaribisha maendeleo mapya kama hayapingi wazo lake kuhusu anachofikiri kitafaa kulingana na falsafa yake. Siku hizi neno "mhafidhina" huchukuliwa mara nyingi kama neno lenye kudharau au kubeza maoni fulani ya mtu. Ni lazima dhana hili litofautishwe na dhana la "fundamentalist". Mawili hayo si visawe hata kidogo.