Doubtful debts ni madeni katika kundi la madeni yaliyo mashakani kulipwa.
Provision for doubtful debts ni kuyaonesha madeni hayo mstari pekee katika orodha ya madeni kwenye taarifa za fedha hususan mizania.
Shirika linakuwa na sera kuhusu madeni mabaya. Sera itaonesha ili deni liwe baya limecheleweshwa kulipa kuanzia siku ngapi.
Itaonesha pia asilimia ya tozo dhidi ya kiasi kilicho cheleweshwa. Kiuhasibu kiasi cha tozo kinaongeza matumizi katika hesabu ya mapato na kuongeza kiasi cha akiba ya madeni mabaya katika mizania sehemu ya mtaji au mstari chini ya madeni kwa kupunguza.
Kuelewa kwa kina suala hili, unahitaji kukaa na mtaalamu mhasibu na kutumia maandishi yaani kuoneshana jinsi kanuni ya MPE na MTOE inavyofanyiwa kazi.
Sent using
Jamii Forums mobile app