Nini maana ya PMPO na RMS kwenye audio system?

CORAL

JF-Expert Member
Jun 26, 2011
2,789
1,782
Unapoenda kununua mfumo wa muziki au system ya mziki dukani au unapoangalia kwenye Internet kuhusu audio system utakuta kwenye specifications upande wa power output ya spika wamekuwekea 1000w RMS na labda 1600w PMPO kwenye maelezo ya hiyo system. Au utakuta 1500w RMS na 3500w PMPO. Dukani utakuta wameweka label imeandikwa kitu kama hicho kwa maandishi makubwa.

Je, nini maana ya PMPO na RMS?
Je hizo watts wanazoweka mfano 1000w au 2400w ndio matumizi ya umeme ya hiyo mashine?
Kama sivyo watengenezaji wanapoweka hizo watts wana maana gani na lengo gani kwa mteja?

PMPO
Well, kwanza tujue nini maana ya PMPO.
Herufi hizo zina wakilisha peak momentary power output. Kwa hiyo ni kipimo cha power output cha spika za audio system. Pia huitwa "dynamic sound" au "peak music power output". watengenezaji wa audio system wanapotafuta PMPO wanatumia nyimbo zenye mdundo mzito ili kupata reading ya juu kadri inavyowezekana. Kwa kweli spika zinasulubiwa sana kwa sababu wanafungulia sauti ya juu kabisa na hapo hawajali sound qualty wanachotaka ni reading ya juu sana ya PMPO.

PMPO inakusudiwa kuwahadaa wateja na sio halisi. Mazingira yanayotumika na sauti ya juu haviwakilishi hali halisi ya nyumbani kwa mteja.

Isitoshe hiyo reading inapatikana kunapokuwa na "mlipuko wa ghafla" wa sauti ( sound outburst) ambao hutokea ndani ya sehemu moja ya 1000 ya sekunde! (within 1 milisecond=1/1000 sec )Hiyo ndio maana ya matumizi ya neno "momentary". Eti hiyo reading ndio iwakilishe wimbo wa dakika 4, 5 au zaidi! Kiukweli hakuna tone ya muziki inaweza kuwa fupi kiasi hicho.
Lakini wao wanasoma reading watakuwekea 1000w au 3000 w PMPO. Hakuna uhalisia hapo.

RMS. Hii ni root mean square. Kipimo hiki kina logic zaidi kuliko PMPO kwa hiyo mnunuzi wa audio system inafaa aangalie RMS kuliko PMPO.
RMS inapatikanaje?
Ni kwa kusoma readings kadhaa- tuseme 50-kwa kutumia nyimbo tofauti kisha:
*kila reading inakuwa squared,
*squares zinajumlishwa pamoja,
*jumla ya squares wanaigawa kwa idadi ya readings mfano 50,
*baada ya kugawa jibu linatafutiwa square root.

Hiyo ndio RMS
Readings zinasomwa kwa kila spika na kujumlisha pamoja kwa kila reading. (Lakini kwa spika zinazofanana mfano kama stereo system inakuwa ina woofer 2 inapimwa moja na takwimu kuzidishwa kwa 2 kwa sababu zina specifications zinazolingana. Hivyo hiyo kwa spika nyingine zinazofanana kisha jumla ya system nzima Inapatikana).

Kwa kuwa RMS inanapatikana kutokana na readings nyingi za power output, inawakilisha uhalisia zaidi kuliko PMPO na mara zote RMS iko chini kuliko PMPO.

Lakini pia hapa pana shida.Kwa kuwa trend ya watengenezaji ni kupata takwimu za juu zaidi basi wanapotafuta RMS wanachukua readings za juu ndio wanafanya calculation kupata RMS. Hawachukui za chini na za kati kwa hiyo figure wanayotangazia soko sio halisi. Lakini licha ya mapungufu hayo bora RMS kuliko PMPO.

Sasa tuje kwenye swali hili: Je, rating za PMPO au RMS ndio matumizi ya umeme ya mfumo wako wa mziki? Hili swali linaweza kuwasumbua wengi.

Ebu tufikirie hoja hizi zifuatazo:

1. Utakuta dukani Hi Fi system imebandikwa lebo yenye maandishi makubwa: PMPO 2400w RMS 1800w. Je hiyo system inatumia umeme wa 2400w au 1800w? Ingawaje matumizi ya umeme kwenye audio system sio constant lakini hawawezi kukuwekea ratings 2 au zaidi kwa system hiyo hiyo moja. Hakuna kifaa cha umeme kinachoweza kuwa na taarifa 2 za matumizi ya umeme. Pasi imeandikwa 1000w, taa 25w nk Kumbe hizo watts sio matumizi ya umeme.

2. Je, inaingia akilini kuwa mtengenezaji wa surround system au stereo system akujulishe kwa maandishi makubwa kuwa mashine yake inakula sana umeme? Bila shaka hii haina logic kwa sababu atafukuza wateja.

3. Pia ieleweke kwamba hizo ratings za PMPO na RMS anazokuwekea mtengenezaji ni power output ya spika. Audio system sio spika peke yake. Kuna amplifier, dvd player, feni, crossover, waya, nk. Vyote vinatumia umeme na wakati wa kupima power output ni spika tu zinahusika.

3 Hoja ya mwisho ni kuwa audio system ni moja ya vifaa vya elektroniki ambavyo vina operate kwa masaa mengi kwa siku. Mfano audio system ina rating ya 2000w RMS, kama hayo ndio matumizi ya umeme ebu fikiria unasikliza muziki kwa muda wa masaa 8 mfululizo.

Nadhani ujumbe utaupata kwenye matumizi ya umeme kwa kuwa kwa muda huo mashine itakula units 16 kwa sababu unit moja inaishia katika dakika 30 tu yaani sawa na kuwasha jiko la umeme la 2000w kwa masaa 8! Bila shaka watu wangeishashtuka zamani sana. Lakini audio system ya 2000w RMS ukioperate kwa masaa 8 hata impact ya utumiaji umeme hutaiona.

Kumbe basi hizo ratings za PMPO na RMS sio matumizi halisi ya umeme.

Kwa hiyo basi, watengenezaji wa audio systems wanapotuwekea hayo manamba makubwa ya PMPO na RMS wanatufikishia ujumbe gani?

Kwamba muziki wanaokuuzia una mdundo mkubwa sana na ni tofauti na watengenezaji wengine. Ni moto wa kuotea mbali. Ni kweli jinsi namba zinavyopanda ndivyo na power output ingawa takwimu zao kama tulivyoona huko juu sio halisi.
Bado swali linabaki, kama RMS, labda 1000w sio halisi je RMS halisi inapatikanaje?

Kinachotakiwa ni uaminifu tu. Unachukua power output readings za juu, kati na chini (full range). Ukifanya hivyo utapata majibu yapo chini sana kuliko ile namba ya mtengenezaji. Mfano wadau fulani wa masuala ya audio wamefanya hiyo kazi na kupata RMS 7.5w au 10w wakati mtengenezaji anadai ni 1000w! Kama ni umeme hayo ndio matumizi halisi.

Ushauri kwa mnunuzi.
Usiangalie PMPO -hii ni upotoshaji mkubwa yaani propaganda ya kibiashara. Walau unaweza kuangalia RMS inaaminika zaidi ingawa nayo sio halisi.

Kama unaenda kununua mzigo dukani hakuna haja ya kuhangaika na hayo maandishi, wewe beba cd ya nyimbo uzipendazo wape wakuwekee utathmini mwenyewe.ukiridhika lipia chukua mzigo sepa.

Kwa wanunuzi wa mtandao kazi ipo kwa sababu hawana priviledge ya kutest mzigo kabla ya kununua. Utafanyaje? . Ijue RMS ya audio system ambayo unatumia kwa sasa. Ukiona ile ya mtandao ina figure kubwa zaidi jua kuwa power output ipo juu zaidi.Ingawa kuna mapungufu katika kukusanya data ili kukokotoa RMS lakini hili ni tatizo la watengenezaji karibu wote. So for the matter of comparison hautapotea sana. Kwa hiyo kama ya kwako ni 600w ukikuta mtandaoni ya 800w ujue iko juu zaidi kwa power output.

Sasa utajuaje matumizi halisi ya umeme ya audio system?
Angalia nyuma ya subwoofer au amplifier. Utakuta maandishi mdogo yameeleza Model no , power rating yaani matumizi ya umeme, frequency, nk Yaani hapa ni waaminifu kweli. Utakuta RMS wanamwambia 900w kwa maandishi makubwa lakini nyuma wamekuwekea 60w.

Matumizi haya mara nyingi hatuyafikii kwa sababu unahitaji kusikiliza nyimbo zinazohitaji power kubwa na isitoshe lazima volume iwe juu sana. Lakini kwa matumizi ya kawaida nyumbani hatufikii hayo matumizi ya umeme. Hata wimbo mmoja unatofautiana power output ambayo ndio inadetermine matumizi ya umeme. Kwa hiyo hata kwa rating ya 60w unaweza kukuta hata 35w hufiki.

Tatizo kubwa kwenye audio systems hakuna standardization upande wa performance tests. Kila.manufacturer anatumia mazingira yake nyimbo zake nk ili kupima power output. Hakuna third party authority inayothibitisha ratings za manufacturers. Lakini hadi hapa nadhani tumewekana sawa.
 
mimi nina ka hometheatre nyumbani,kadogo tu kameandikwa pmpo 3500w

nilipogeuza nyuma kwenye speaker zote,kubwa in 90w,ndogo zote zina 45w,ambazo kama utajumlisha utapata 300w tu.lakini speciffication naambiwa ni hometheatre ya watt 600.kipi ni kipi??

sema kanatandika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mimi nina ka hometheatre nyumbani,kadogo tu kameandikwa pmpo 3500w

nilipogeuza nyuma kwenye speaker zote,kubwa in 90w,ndogo zote zina 45w,ambazo kama utajumlisha utapata 300w tu.lakini speciffication naambiwa ni hometheatre ya watt 600.kipi ni kipi??

sema kanatandika.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio uongo tunazungumzia hapa. Ukweli upo nyuma ya spika na mashine yenyewe.
 
Huwa hawatumii mziki kutest kupata hizo pmpo au rms ...ni una generate tu frequency na frequency generator
 
mimi nina ka hometheatre nyumbani,kadogo tu kameandikwa pmpo 3500w

nilipogeuza nyuma kwenye speaker zote,kubwa in 90w,ndogo zote zina 45w,ambazo kama utajumlisha utapata 300w tu.lakini speciffication naambiwa ni hometheatre ya watt 600.kipi ni kipi??

sema kanatandika.

Sent using Jamii Forums mobile app
Peak music power huwaga mara mbili ya rms...
 
Back
Top Bottom