Nini maana ya neno UCHOCHEZI?

Kwa mujibu siri kali ya mkoloni mweusi na makaburu weusi uchochezi ni pale utakapowakòsoa viongozi wa serekali hii na kujadili udhaifu wao kwa kuongea ukweli bila chenga.
Uchochezi ==kuongea ukweli kwa kuwakosoa viongozi ambao wapo madarakani?
 
Uchochezi ni mtu kusema ukweli ambao wahusika hawataki kuusikia
 
"wachochezi" wana tabia ya kukosa "uzalendo" na ukikosa uzalendo wewe ni "wakushughuliliwa" tu. Haya maneno hutumiwa na wenye madaraka na wao ndio hujipa mamlaka ya kutoa tafsiri yake.

Troika mpya ya nchi kwenye mishahara, marupurupu na vinginevyo-ni bunge (watunga sheria), mahakama (watoa haki), na wajeda (kukufungulia mashtaka au kukutafutia kosa, kukuhifadhi gerezani, .........) no wonder kazi moja wapo wata wa shughulikia wachochezi hasa waliokosa uzalendo.
 
Hakika Maana Vyombo Muhimu Na Vyeti Kama Mahakama Idara Yao Ya Elimu Kwa Umma Itupatie Maana Na Tafsiri Ya Neno Uchochezi Ili Tuwe Makini Kuhusu Hilo Neno.

Kwasasa Ni Kama Uonevu Na Ukandamizaji Kutufunga Mdomo Tusiseme Jambo Lolote
Ni kweli kabisa wanatakiwa kutoa ufafanuzi nini maana ya neno uchochezi
 
Mjadala kwa manufaa ya nani sasa? Hawa wahuni akina Lema na Lisu? Waache waisome namba.

AasiyefundiShwa na ***** hufundishwa na ulimwengu.
Mjadala kwa manufaa ya watu wengi ukiwepo hata na wewe
 
Sijaelewa hapo
 
Mambo madogo kama haya hayahitaji mijadala ya kitaifa, ni suala tu la uelewa, uchochezi kitendo kinachotokana na neno chochea ni kama upuuzi kutoka kwenye neno puuza. Swali, unapochochea unakua unafanya matendo gani na dhamira ya kitendo cha kuchochea inakuaga ni ipi? Pamoja na kiwango chetu kidogo cha IQ (National Average) sidhani kama jambo hili linaweza likatushawishi kuwa na mjadala wa kitaifa.
 
Katiba ya kikoloni huzaa sheria za kikoloni. Uchochezi ulitumiwa na wakolono na sasa wakoloni weusi wanaendeleza
 
Nini maana ya neno uchochezi?
 
Naomba nieleweshwe ni ipi maana ya uchochezi kutokana na katiba yetu ya JMT, maana nakuwa confused sielewi, inamaana ukitaka kufikisha kero za wananchi mahala huska ni uchochezi pia?

Ukutumia uhuru wako wa kutoa maoni, mikusanyiko, au hata migomo pale unapohisi haki yako ya msingi inaminywa ni uchochezi pia?

Maana sielewielewi hili neno UCHOCHEZI naombeni msaada wenu ili nisije vunga najua kumbe sijui lolote kuhusu uchochezi.
 
kama ni kwenye mpira wa miguu unaweza kufanya uchochezi kwa kuwashangilia kwa nguvu wachezaji wa timu yako wakaongeza bidii ya kucheza,maana utakuwa umewachochea kama unavyochochea kuni kwenye moto
 
Kwa sasa nafikiri hakuna neno maarufu hapa nchini kama neno uchochezi maana karibu kila kosa utasikia ni uchochezi!

Sasa katika hizi mahakama zetu neno hili uchochezi linatafsiriwa kwa kufuata Kamusi ya Kiswahili au hili neno lina tafsiri maalumu ya kisheria?

Mwenye majibu atusaidie maana neno hili sasa limekuwa kama wimbo wa taifa na kuna watu kila wakati wanahukumu wengine kwa uchochezi utadhani wao ndio mahakama.

Hivi mwanasiasa wa upinzani angewataka wakulima kwenye jimbo lake wauze kwa mfano gunia la mchele kwa bei kubwa kuliko kawaida(walangue) angeachwa kuitwa mchochezi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…