Nini maana ya neno Mama katika maisha yangu?

Nini maana ya neno Mama katika maisha yangu?

Innocent Kirumbuyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2014
Posts
4,647
Reaction score
4,495
Neno mama lina maana nyingi sana katika maisha yangu,nikianza kipindi nipo mtoto,mama yangu hukuishi na furaha kwani furaha yako ilitoka kwangu.nilipocheka nawe ulicheka pia,ila nilipolia uliumiza kichwa ili kujua ni kipi hasa kinilizacho.wakati mwingine hukuwa na pesa ya kunipeleka kwenye vipimo hosptali,basi uliweka mkono wako katika shavu langu ili kupima joto.Neno "Labda" halikukatika mdomoni mwako,maana hukupenda kabisa kuniona nikiwa sina raha.

Kwa neema ya Mwenyezi Mungu aliyonijaalia nikakua na kuanza shule,mama yangu ulinisihi sana kusoma kwa bidii,huku ukinikumbusha jinsi ulivyonilea kwa tabu.
Lakini ujana ulinipitia na kushindwa shule na kuwa mtu wa nyumbani,maisha yalipozidi ugumu,mama yangu hukunipa mgongo kwani hata nilipokuwa natafuta vibarua nakumbuka ulinisihi sana kutokukata tamaa na kumtanguliza sana Mungu.
Kwa mara ya kwanza nilipokuwa nataka kutoka nyumbani sikuwa na pesa ya nauli,ila mama ulifanya kila njia ili mwanao nipate pesa,na hata ulipokosa hukuona shida kuuza nguo zako ili mimi nipate nauli ya kwenda kutafuta maisha
Nakumbuka uliwahi kusema kuwa,huogopi kufa hapana,maana kufa ni lazima utakufa.ila ulidai unaogopa sana kufa na kuniacha mimi nikiwa sina mbele wala nyuma.

Mama maisha upande wangu bado magumu sana,ila kuna kitu najivunia kuwa nacho "subira na uvumilivu" nimetafuta sana maisha ila nashukuru kuwa Mungu ananisikia,maana mama ulidai kuwa ulinizaa nikiwa uchi hivyo kuwa na suruali 2 na t-shrt 3 ni moja ya mafanikio katika utafutaji wangu.

Mama yangu unatumia simu ya shilingi elfu 25,lakini mimi niliwahi kuhonga simu ya laki 4 kwa msichana ambaye badae alinitemea mate na kuniacha.ila yote hayo mama yangu hukuyajali,bali uliniombea mema ili uone maisha yangu yakiwa katika mstari uliyonyooka.Ninapokula raha na rafiki zangu huwa sikukumbuki,ila nilipopata shida na kuja kwako ulinipokea kwa tabasamu tamu na kunikalisha chini kama mtoto mdogo.kisha kutaka kujua kipi hasa kinisumbuacho . pumzika kwa amani mama yangu mpendwa
#Hakuna kama mama yangu#
FB_IMG_1531413655644.jpg
 
Pole mkuu.. Strong mothers never die but rest in peace.
 
Wamama huwa wanahangaika sana na watoto jamani.
 
Ninaumiaga sana mama yangu pamoja na kuhangaika kote, bado alienda zake bila kuyaona mafanikio yangu.
 
Back
Top Bottom