Nini maana ya ndoto hii?

Nini maana ya ndoto hii?

Program Manager

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2018
Posts
3,082
Reaction score
4,472
Mwenye kuelewa maana ya ndoto hii na anipe tafsiri.

Tulikuwa tuna kampeni za uchaguzi mkuu,
Mimi nilikuwa Mfuasi wa Chama Fulani Cha upinzani lakini nilikodiwa kufanya kampeni kwenye chama kinachotetea kiti.

Mgombea wa Chama kilichonikodi ni mama,naye alikuja kwenye kampeni hizo Kwa malengo mawili.
1.kujinadi
2.kutu assess ikiwa tunafaa kupewa nafasi za uongozi endapo atashinda.

Kampeni zilikuwa zinafanyika Kijijini kwetu siku hiyo, shuleni niliposoma kwenye chumba Cha darasa la 7.

Mimi nilikuwa wa mwisho kuingia na pia niliandikwa ubaoni kwenye orodha ya wazungumzaji,Tena niliandikwa Kwa jina langu moja tu lakini wengine waliandikwa Full names.

Wahudhuriaji (wasikilizaji)walikuwa ni wachache ni kama robo darasa tu na kadri muda ulivyosonga walizidi kupungua,walikuwa ni watu ninaowafahamu Kwa sura Tena ni wanafunzi wenzangu niliosoma nao hapo miaka ya nyuma.

Kulikuwa na watu wengine nje ya darasa lakini hawakuingia kusikiliza Tena walikuwa wanaendelea na michezo na shughuli zao kama kawaida na hawakusogea kusikiliza kampeni.

Zamu yangu ilipofika nikapewa mic Ili nimpambe mgombea ambaye naye alikuwepo na alikaa kwenye dawati mbele kabisa,

Sikufanya ajizi,niliongea maneno yenye kumfurahisha mpaka akajawa na Furaha na tabasamu,wenzangu walionitangulia hawakufanya hivyo Hali iliyopelekea mgombea kuinanimia dawati muda mwingine,lakini ilipofika zamu yangu Mimi hakusinzia.

Cha ajabu nilipomaliza kuongea hata yule MC aliyenipa mic hakuwepo Tena darasani na baadhi ya watu pia walishaondoka,nikarudi mezani Kwa heshima nikamuaga mama mgombea naye akanijibu Kwa Furaha lakini hapakuwa na wa kuendesha tena mkutano kwani ameshaondoka.
Ni kama wote walisusia hivi.

Mwisho wa ndoto.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom