Nini maana ya major katika masomo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini maana ya major katika masomo?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by mhalisi, Mar 22, 2012.

 1. mhalisi

  mhalisi JF-Expert Member

  #1
  Mar 22, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 1,181
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  ndugu zangu nimekuwa nikiangalia website za vyuo vya nchi za nje hususani vyuo vikuu vya nchini china na nimekuwa nikiona kuna kitu wanakiita major katika program zao za masomo lakini nimekuwa sielewi!
  Mfano unakuta kuna chuo kinatoa bachelor of international economy and trade,na hiyo ndio major yenyewe,lakini mwishoni mwa masomo yako chuo kinasema kitakuaward bachelor's degree in economics. Mfano mwengine unakuta chuo kinasema kinatoa bachelor of computer science,ikiwa ndio major lakini mwishoni mwa masomo yako chuo kinasema kitakuaward bachelor of engineering. Ndugu zangu jambo hili linanitatiza,kwasababu inakuwaje kwa mfano mwanafunzi usome bachelor of international economy and trade lakini mwishoni ugraduate bachelor in economics! Ndugu zangu naombeni kueleweshwa vizuri juu ya jambo hili hususani hiki kitu kinachoitwa major,nini maana yake?
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Mar 22, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Kwa Marekani 'major' ni fani kuu ambayo mtu anasomea akiwa chuo kikuu. Mfano, mtu anaweza ku-'major' kwenye English halafu aka-'minor' kwenye Journalism.

  Au 'major' ya mtu inaweza ikawa ni Chemistry halafu 'minor' ni Biology.
   
 3. JS

  JS JF-Expert Member

  #3
  Mar 22, 2012
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kama Nyani Ngabu alivyojibu ni sawa sawa kabisa na hiyo ni system ya vyuo vikuu kwa undegraduate courses. Kwa mfano huo uliotoa ina maana hayo ni masomo ndani ya economics kwa sababu economics ni kubwa imegawanyika katika macro na micro economics. sasa basi ukianza first year unafundishwa basic principles au niseme introductory part of economics. halafu ukiingia second year na kuendelea hapo ndo unaanza kumajor katika baadhi ya masomo ndani ya economics ndo hiyo international economy and trade....lakini pia utakuwa una-minor masomo mengine ambayo yanaendana kiasi na masomo unayo-major. cha muhimu ni mwanafunzi ujue unataka kuja kuwa na fani gani hapo baadae ukishajua hiyo ndo ita-determine greatly what you will want to major in.
   
 4. mhalisi

  mhalisi JF-Expert Member

  #4
  Mar 22, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 1,181
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Nyani Ngabu na JS nawashukuru sana kwa maelezo yenu. Lakini naona vyuo vikuu vyetu vya hapa nchini havina mfumo huu wa major, pengine ndio sababu kwa mfano mwanafunzi anayesoma bachelor's degree of economics, mwishoni mwa masomo yake anagraduate bachelor's degree of economics.
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  Mar 23, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Sasa Tanzania 'major' wanaiita nini?
   
 6. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #6
  Mar 23, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,688
  Likes Received: 654
  Trophy Points: 280
  Kwa Tanzania nadhani ukiamua kuchukua degree hiyo ndiyo Major yako, huwa hawana minor.
  mimi nadhani ni kwa sababu Chuo kikuu unapangiwa nini cha kusoma, hatuna General studies ambazo unaweza kuchagua wakati upo undecided.
  Marekani unaweza kumwambia counselor wako kwamba somo hili silipendi, akakupangia somo lingine, au uka add/drop somo and still get a degree with honors.
  Kwa mfano kama unaweza ukachagua kwenye Department ya Physics either usome Astronomy na ukapewa credit kama umesoma Physics 101.
  Au ukachagua Statistics instead of Calculus au Algebra.
  Ila kwa Tanzania, ni lazima wote mnoachukua degree moja, msome masomo sawa kwenye minors, au prerequisites.
   
 7. D

  DOOKY JF-Expert Member

  #7
  Mar 23, 2012
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  ndiyo maana elimu yetu na wahitimu ni vitu 2 tofauti, aweza kufaulu lakini utendaji mbumbumbu.
   
 8. U

  Uncle Jei Jei JF-Expert Member

  #8
  Mar 23, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,201
  Likes Received: 943
  Trophy Points: 280
  Kwa tanzania major ndo bachelor yenyewe uliyosajiliwa. Mf. Unaweza kuwa unachukua "bachelor of arts in economics" hiyo ndo major yako kwani department ya economics itakupangia coz muhimu za economics zisizo pungua unit zilizopangwa na dept.kama criteria ya kugraduate! But still unaweza ku-opt minor courses from other dept. Kulingana na matakwa yako!! Dept. Zina minimun criteria to meet 4ur undergraduate but hii haikuzui ku-minor coz nyingine mf. Za socialogy au acounts!
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Mar 23, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Major ndiyo bachelor's degree? That doesn't make any sense.

  Kwa kutumia mfano wako wa economics, ukihitimu masomo ya shahada ya kwanzan utatunikiwa BA in Economics. Kwa hiyo hapo major yako ni economics.

  Major ni fani na siyo shahada. Ila ndani ya fani kuna msisitizo (emphasis?) pia. Kwa hiyo unaweza uka-major kwenye economics with an emphasis in agricultural economics, kwa mfano.
   
Loading...