Nini maana ya maisha?

Nini maana ya maisha?

Kusini pride

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2022
Posts
1,762
Reaction score
4,070
Wakuukwanza niseme nakushukuru sana kwa JamiiForums haswa inaleta exposure watu tunapona kimya kimya kwa maana siku niliyojiunga sikulala ni kama nilikesha natafuta hizi parts nasoma mpaka nikajikuta najiahidi kujileta kwako

Kitu niligundua tangu nikufatilie ni uko very so down to earth not judgemental at all unajitahidi sana kuufanya ukurasa wako kuwa sehemu salama ya mtu kuzungumza bila kuwa attacked kwa matusi, na wewe unajua uongee nini bila kuacha kovu, sijui kama unafaidika na haya unayofanya ila unafanya,

Kuna sehemu unaongelea vitu muhimu sana kwa njia nyepesi ili tu mtu aelewe hadi nahisi nje ya humu ni wale watu wenye upendo sanaaa watu wako wa karibu ndio wanaweza kututhibitishia hili

Sijawahi kukaa chini nikamsimulia mtu maisha yangu na hata kiasili mi si muongeaji sana lakini kwako niulize chochote nitakwambia that is how umefanya nikuamini, na kama nilivyokwambia na mimi niko hapa kuelezea safari yangu

Nilizaliwa mwaka ** kiasili ni ila nimekulia mkoani **. Tangu napata ufahamu mpaka nabelehe nimelelewa umamani sikuwahi kumjua baba yangu mpaka nilipofikisha miaka 18.

Mama yetu alizaa watoto watatu na mimi ndiye mkubwa. Nilianza kulelewa kwa bibi mzaa mama. Wakati watu wengine wana drug addicts (Wanaotumia dawa za kulevya) ambao ni labda kaka, dada sijui binamu mimi drug addict alikuwa mama yangu mzazi kabisa. Yaani huyo dada yako anayetumia madawa azae mtoto, ndio mimi sasa

Hakuna kitu kinauma kama kupata ufahamu na kumuona mama yako stendi au kwenye vibaraza vya maduka akiwa kama kichaa.

Nimekuwa bullied sana shuleni sana sana sana, sikuwahi kufurahia shule sababu ya matani na matusi niliyokuwa napewa na wanafunzi wenzangu na baadhi ya walimu kwa sababu mama yangu alikuwa kama drug addict na kuna wakati alipita karibu na shule.

Laura mama yangu alikuwa ananijua kwa sababu kuna kipindi alifungiwa ndani hatukuruhusiwa kumsogolea lakini nilijitahidi kumsogelea kwa kujificha, she was my mom, sikuwa na mama mwingine ni huyo huyo kichaa nilihitaji anikumbatie nilitaka kuita mama nae aitike nilimpenda sana, alikuwa anakuja shule ananiulizia watu wanacheka anafukuzwa na kutishiwa kupigwa nami naambiwa nisilete vichaa shuleni kuna siku alipigwa na mlinzi wa shule maskini akaacha kuja

Alipofungiwa ndani hali yake ilikuwa mbaya kiasi aliachiwa akazurure tu mwisho wakaanza kusema amelogezewa kulala mtaani lakini nahisi mtaani alipata hizo dawa akifungiwa ndani alikuwa anapata arosto mpaka wanamhurumia, kama kuna mtu amewahi kuishi na drug addict anajua naongelea nini

Basi hayo ndo maisha nilioishi mwanzoni kabisa, pale kwa bibi palikuwa na wajukuu wengine nilipofika darasa la tano aliletwa mtoto ambaye mama alimzaa mtaani akapokonywa akaja kulelewa na bibi kwa mtindo huo nilipata ndugu zangu wawili nao kama mimi hawakuwajua baba zao

Nikamaliza Darasa la saba nilifaulu kwenda sekondari ambayo ilikuwa mbali kidogo na nyumbani, Bibi alikuwa anauza pombe ndio napata mahitaji na mimi namsaidia kuuza mahindi ya kuchemsha kwa kutembeza tukipata hela tunagawa za shule na mahitaji ndani,

Kiukweli watoto aliozaa bibi hawakuwa na msaada kwake alizaa watoto saba, kila mmoja alikwenda kutafuta maisha baadhi walileta wajukuu kuishi pale na wajukuu wawili wakaleta vitukuu kulikuwa na mjomba mlevi sana yeye alikuwa mtu wa kunywa na kupigana sana, mwaka **** mjomba aliishia jela kwa mauaji ya mtoto wa dada yake

Alimpiga sana kisa alimtuma dukani akapoteza hela alimpiga tukishuhudia na hakuna mtu alisogea coz mjomba alikuwa anaogopwa hata na bibi alishawahi kumshikia kisu huku tunaona, ila kipigo kile kilizidi coz mtoto wa mamdogo alimshitaki kwa bibi kuwa usiku anamfanyia mambo mabaya, kukawa na kuzozana baina yao yakaishia chumbani uko ndio baadae kumtuma akapoteza hela

Usiku tumelala mwenzangu akaanza kukoroma sana ikabidi tuamshane akaanza kukohoa damu kufika hospital amefariki ndio mara ya kwanza kujua kifo ni nini kwa mtu unayeishi naye kufariki
Ma mdogo kuja kukawa na kesi ndio ilipelekea mjomba kufungwa.

Hayo mambo yote yanatokea bibi naye akaanza kuumwa sana kipindi hicho sikujua mama alipo maana hata mtaani alitoweka sikumuona tena kwa kipindi kirefu, Wakati bibi anaumwa mdogo wangu wa mwisho naye alikuwa mgonjwa sana, huyu siku zote alikuwa mgonjwa sababu alikuwa na Sickle Cell kwa hio nyumba ikawa na watu wawili wagonjwa,

Baada ya msiba watu waliondoka pale, hakukubakia hata na ndoo ya mchele wala zile hela zilitolewa sikuziona, upande wa baba wa marehemu walikuja na vitu vingi sana, mamdogo alitoka mjini na watu wamemsindikiza walikuja na vitu vya kula. Msiba ulija watu wengi sana, na watu hao tena ndugu walichota vyakula wakaenda navyo makwao hela sijui ziliishia mikononi mwa nani lakini mwisho wa siku mimi na bibi tulibaki chumbani tumekaa kitandani hatuna chakula hatuna pesa, nakumbuka kuna ndugu nilimuomba pesa kidogo alinijibu baba zenu wako wapi watafuteni baba zenu

Hii iliuma sana sidhani kama kuna mtoto huwa hatamani kumjua baba yake au kusaidiwa na baba yake hata aweje au maskini kiasi gani mimi huyo baba hata sikuwa namjua wakati huo

Nimetembeza sana mahindi, nimebeba mizigo midogo midogo, nimeuza sana maji ili nipate hela ya chakula na matibabu ya bibi na mdogo wangu

Maisha yangu kimasomo yalikuwa ya hovyo sana siku zote wa mwishoni uko laura ningesoma saa ngapi, nikiwa form two sijui ilianzaje lakini ulianza utani wa kuitwa jina baya sana ****.

Naomba hili usiliweke kisa tu habari za mamangu zilianza tena kuwa mdomoni mwa watu, kipindi hicho mamangu alikuwa kama changudoa mitaa fulani mbali kidogo alikuwa amedhoofika sana, nilkwambia ilipita kipindi kirefu sijamuona kisha akarudi mitaa hiyo

Nakumbuka siku moja usiku wakati natoka stendi nilitembea mpaka mitaa hiyo ili japo nimuone, I missed her i loved her na nilikuwa najiuliza sana kama aliwahi ata kunikumbuka au kunifikiria, mimi sikuwahi kumsahau, baadae ikaanza kuwa mazoea natembea mpaka huko nakaa sehemu namuangalia wakati mwingine nalia peke yangu kisha narudi nyumbani ambako watu wote wananitazama, Laura sikuwa hata na miaka 18

Siku moja nilienda baada ya kama wiki tatu kupita sikumuona sehemu ambayo alipenda kukaa, nilipata wasiwasi sana nikaenda mpaka eneo lile nikamuulizia, maneno magumu sana kusikia ni huyu *** ameanza kulalwa na vitoto sasa apate stimu,

Nilijiskia vibaya kujitambulisha kuwa mimi ni mtoto wake, Wakanionyesha sehemu ya nyuma ya nyumba kuna kijibanda amelala umo amejisaidia hajiwezi wametelekeza hapo, sikuweza kufanya chochote nilikufuru kwa mara ya kwanza nilikufuru kwanini nimepewa mama wa hivi katikati ya mamilioni ya wanawake wanaojitambua kwanini mimi nipewe kama huyu, lakini ndiyo picha ya mwisho ya mama kunitazama usoni na kutabasamu, coz alifariki wiki moja baadae

NitaENDELEA...
 
Interesting......

ila nina imani katika hizo changamoto bado nakuona you made it .

Hongera Sana stay positive
 
Kufa ukiwa madarakini kama huyu
IMG_0612.jpeg
 
maisha yana ups and downs nyingi katika safari ya maisha kuna milima na mabonde

. Wakati mwingine tunapanda juu, tukiwa na furaha, mafanikio na matumaini. Lakini kuna nyakati tunashuka bondeni, tukikumbana na changamoto, huzuni na majaribu.

ila hatupaswi kukata tamaa.

Milima hutufundisha kushukuru, na mabonde hutufundisha uvumilivu na bidii.

Kila changamoto ni fursa ya kujifunza na kukua.

Tuendelee kusonga mbele kwa imani, tukijua kuwa baada ya bonde, kuna mlima mwingine wa mafanikio.
 
Hii stori aliyeifungulia uzi humu sio yake na ndio maana hakuimaliza,stori yote iko kwa laura Petty kule fb kuna mdau ndio aliitoa na ameimaliza yote mnaweza kuifatilia kule au ntaiweka humu na kumpa credit zake mhusika wa hadithi ambaye ni Laura
 
HUSTLER

Laura kwanza niseme nakushukuru sana kwa ukurasa wako haswa hii part ya hustler inaleta exposure watu tunapona kimya kimya kwa maana siku niliyokufollow sikulala ni kama nilikesha natafuta hizi parts nasoma mpaka nikajikuta najiahidi kujileta kwako

Kitu niligundua tangu nikufatilie ni uko very so down to earth not judgemental at all unajitahidi sana kuufanya ukurasa wako kuwa sehemu salama ya mtu kuzungumza bila kuwa attacked kwa matusi, na wewe unajua uongee nini bila kuacha kovu, sijui kama unafaidika na haya unayofanya ila unafanya,

Kuna sehemu unaongelea vitu muhimu sana kwa njia nyepesi ili tu mtu aelewe hadi nahisi nje ya humu ni wale watu wenye upendo sanaaa watu wako wa karibu ndio wanaweza kututhibitishia hili

Sijawahi kukaa chini nikamsimulia mtu maisha yangu na hata kiasili mi si muongeaji sana lakini kwako niulize chochote nitakwambia that is how umefanya nikuamini, na kama nilivyokwambia na mimi niko hapa kuelezea safari yangu

Nilizaliwa mwaka ** kiasili ni ** ila nimekulia mkoani ****. Tangu napata ufahamu mpaka nabelehe nimelelewa umamani sikuwahi kumjua baba yangu mpaka nilipofikisha miaka 18.

Mama yetu alizaa watoto watatu na mimi ndiye mkubwa. Nilianza kulelewa kwa bibi mzaa mama. Wakati watu wengine wana drug addicts (Wanaotumia dawa za kulevya) ambao ni labda kaka, dada sijui binamu mimi drug addict alikuwa mama yangu mzazi kabisa. Yaani huyo dada yako anayetumia madawa azae mtoto, ndio mimi sasa

Hakuna kitu kinauma kama kupata ufahamu na kumuona mama yako stendi au kwenye vibaraza vya maduka akiwa kama kichaa.

Nimekuwa bullied sana shuleni sana sana sana, sikuwahi kufurahia shule sababu ya matani na matusi niliyokuwa napewa na wanafunzi wenzangu na baadhi ya walimu kwa sababu mama yangu alikuwa kama drug addict na kuna wakati alipita karibu na shule.

Laura mama yangu alikuwa ananijua kwa sababu kuna kipindi alifungiwa ndani hatukuruhusiwa kumsogolea lakini nilijitahidi kumsogelea kwa kujificha, she was my mom, sikuwa na mama mwingine ni huyo huyo kichaa nilihitaji anikumbatie nilitaka kuita mama nae aitike nilimpenda sana, alikuwa anakuja shule ananiulizia watu wanacheka anafukuzwa na kutishiwa kupigwa nami naambiwa nisilete vichaa shuleni kuna siku alipigwa na mlinzi wa shule maskini akaacha kuja

Alipofungiwa ndani hali yake ilikuwa mbaya kiasi aliachiwa akazurure tu mwisho wakaanza kusema amelogezewa kulala mtaani lakini nahisi mtaani alipata hizo dawa akifungiwa ndani alikuwa anapata arosto mpaka wanamhurumia, kama kuna mtu amewahi kuishi na drug addict anajua naongelea nini

Basi hayo ndo maisha nilioishi mwanzoni kabisa, pale kwa bibi palikuwa na wajukuu wengine nilipofika darasa la tano aliletwa mtoto ambaye mama alimzaa mtaani akapokonywa akaja kulelewa na bibi kwa mtindo huo nilipata ndugu zangu wawili nao kama mimi hawakuwajua baba zao

Nikamaliza Darasa la saba nilifaulu kwenda sekondari ambayo ilikuwa mbali kidogo na nyumbani, Bibi alikuwa anauza pombe ndio napata mahitaji na mimi namsaidia kuuza mahindi ya kuchemsha kwa kutembeza tukipata hela tunagawa za shule na mahitaji ndani,

Kiukweli watoto aliozaa bibi hawakuwa na msaada kwake alizaa watoto saba, kila mmoja alikwenda kutafuta maisha baadhi walileta wajukuu kuishi pale na wajukuu wawili wakaleta vitukuu kulikuwa na mjomba mlevi sana yeye alikuwa mtu wa kunywa na kupigana sana, mwaka **** mjomba aliishia jela kwa mauaji ya mtoto wa dada yake

Alimpiga sana kisa alimtuma dukani akapoteza hela alimpiga tukishuhudia na hakuna mtu alisogea coz mjomba alikuwa anaogopwa hata na bibi alishawahi kumshikia kisu huku tunaona, ila kipigo kile kilizidi coz mtoto wa mamdogo alimshitaki kwa bibi kuwa usiku anamfanyia mambo mabaya, kukawa na kuzozana baina yao yakaishia chumbani uko ndio baadae kumtuma akapoteza hela

Usiku tumelala mwenzangu akaanza kukoroma sana ikabidi tuamshane akaanza kukohoa damu kufika hospital amefariki ndio mara ya kwanza kujua kifo ni nini kwa mtu unayeishi naye kufariki
Ma mdogo kuja kukawa na kesi ndio ilipelekea mjomba kufungwa.

Hayo mambo yote yanatokea bibi naye akaanza kuumwa sana kipindi hicho sikujua mama alipo maana hata mtaani alitoweka sikumuona tena kwa kipindi kirefu, Wakati bibi anaumwa mdogo wangu wa mwisho naye alikuwa mgonjwa sana, huyu siku zote alikuwa mgonjwa sababu alikuwa na Sickle Cell kwa hio nyumba ikawa na watu wawili wagonjwa,

Baada ya msiba watu waliondoka pale, hakukubakia hata na ndoo ya mchele wala zile hela zilitolewa sikuziona, upande wa baba wa marehemu walikuja na vitu vingi sana, mamdogo alitoka mjini na watu wamemsindikiza walikuja na vitu vya kula. Msiba ulija watu wengi sana, na watu hao tena ndugu walichota vyakula wakaenda navyo makwao hela sijui ziliishia mikononi mwa nani lakini mwisho wa siku mimi na bibi tulibaki chumbani tumekaa kitandani hatuna chakula hatuna pesa, nakumbuka kuna ndugu nilimuomba pesa kidogo alinijibu baba zenu wako wapi watafuteni baba zenu

Hii iliuma sana sidhani kama kuna mtoto huwa hatamani kumjua baba yake au kusaidiwa na baba yake hata aweje au maskini kiasi gani mimi huyo baba hata sikuwa namjua wakati huo

Nimetembeza sana mahindi, nimebeba mizigo midogo midogo, nimeuza sana maji ili nipate hela ya chakula na matibabu ya bibi na mdogo wangu

Maisha yangu kimasomo yalikuwa ya hovyo sana siku zote wa mwishoni uko laura ningesoma saa ngapi, nikiwa form two sijui ilianzaje lakini ulianza utani wa kuitwa jina baya sana ****.

Naomba hili usiliweke kisa tu habari za mamangu zilianza tena kuwa mdomoni mwa watu, kipindi hicho mamangu alikuwa kama changudoa mitaa fulani mbali kidogo alikuwa amedhoofika sana, nilkwambia ilipita kipindi kirefu sijamuona kisha akarudi mitaa hiyo

Nakumbuka siku moja usiku wakati natoka stendi nilitembea mpaka mitaa hiyo ili japo nimuone, I missed her i loved her na nilikuwa najiuliza sana kama aliwahi ata kunikumbuka au kunifikiria, mimi sikuwahi kumsahau, baadae ikaanza kuwa mazoea natembea mpaka huko nakaa sehemu namuangalia wakati mwingine nalia peke yangu kisha narudi nyumbani ambako watu wote wananitazama, Laura sikuwa hata na miaka 18

Siku moja nilienda baada ya kama wiki tatu kupita sikumuona sehemu ambayo alipenda kukaa, nilipata wasiwasi sana nikaenda mpaka eneo lile nikamuulizia, maneno magumu sana kusikia ni huyu *** ameanza kulalwa na vitoto sasa apate stimu,

Nilijiskia vibaya kujitambulisha kuwa mimi ni mtoto wake, Wakanionyesha sehemu ya nyuma ya nyumba kuna kijibanda amelala umo amejisaidia hajiwezi wametelekeza hapo, sikuweza kufanya chochote nilikufuru kwa mara ya kwanza nilikufuru kwanini nimepewa mama wa hivi katikati ya mamilioni ya wanawake wanaojitambua kwanini mimi nipewe kama huyu, lakini ndiyo picha ya mwisho ya mama kunitazama usoni na kutabasamu, coz alifariki wiki moja baadae

Mama alipofariki ni kama uzito wa dunia ulikuwa mkubwa zaidi ingawa hata hakuwa na msaada wowote sijui nikwambieje lakini nahisi ile kumuona yupo kulikuwa na maana kubwa kwangu kuliko kujua sasa hayupo kabisa,

Kidato cha nne shule ilienda kwa kusuasua sana kwasababu ya majukumu kunielemea na hali ya bibi ilikuwa tete zaidi na kipindi hicho alikuja mamdogo mmoja kuishi pale nyumbani, naye aliachaga watoto wake pale, ujio wake haukuwa wa heri, alikuwa mkali sana, niseme ni wale watu wa kuamrisha, akiitisha kitu ukachelewa unatukanwa, hata mlango ukibaki wazi kidogo unatukanwa so nyumba ikawa haina tena utulivu nikajikuta napachukia sana nyumbani pale

Kiukweli mamdogo alikuwa haoni jitihada zozote nnazofanya ili watu wale wakiwemo watoto wake aliowaacha hapo nyumbani na ikitokea mdogo wangu akazidiwa anakimbizwa hospitali alikuwa mtu wa kulalamika sana kama vile ugonjwa wa ndugu yangu ni mzigo kwake

Tusi kubwa kila siku lilikuwa kuitwa mbwa na kuambiwa nna akili kama za mamangu kwani chizi huzaa chizi. Hata kitu cha kunielekeza alinikaripia na kunitukana nitaishia kama mamangu. Haya maneno sikuyapenda kila alipoyasema na tabia ya kunisukuma kichwa kila akinigombeza, siku moja nilishindwa kabisa kuvumilia nilimvunjia heshima na mimi nikampandishia sauti nadhani na hasira za balehe zilichangia tukapigana.

Kesi ilikuwa kubwa sana huezi amini hata wale watu ambao hawajui tunaishije mle ndani walinilazimishwa kuomba msamaha ambao nilikataa kabisa kuuomba nikaambiwa kama naona nimekua nitoke pale kwa bibi nikajitegemee sasa, roho ilikuwa inaniuma coz alinitegemea na wadogo zangu nisingewaacha vile lakin maisha na mamdogo pia nisingeweza kwakweli niliingia ndani nikachukua nguo nikaondoka pale nikaenda kwa jamaa flani nilimjulia kwenye biashara zetu,

Nakumbuka nilikaa kama wiki au zaidi sijaenda hata shule wala nyumbani mpaka siku moja asb wakaja wanafunzi wenzangu wakasema natafutwa shule mitihani imekaribia mimi kuna vitu sijakamilisha siku nilioenda nikapita pia nyumbani, dah nakuta yule mdogo wangu mgonjwa kaungua mdomoni na miguuni nikaambiwa alisukumiwa uji wa moto kabisa anywe hapo ugomvi mwingine ukazuka, safari nilimpiga mamdogo nikamkaba kwahio wakanikuta nimemkaba kesi ikawa yangu tena nilifukuzwa kama mbwa nikaondoka na wadogo zangu

Nimefanya mtihani natokea kwa yule jamaa na wadogo zangu naishi nao, mtihani kuisha jamaa akawa kama ameanza kutuchoka ikabidi nijiongeze kutafuta pa kuishi, kuna mama alikuwa anapika pombe kama bibi ilibidi nikamuombe atuifadhi hata jikoni akakubali nikawa nawaacha pale naenda kupambana nikipata chochote naleta yule bibi alinisaidia sana kumuuguza mdogo wangu japo mazingira yalikuwa duni,

Kipindi hiko bibi akafariki lakin msibani nilionywa nisikanyage nikawa naitwa mvuta bangi na mm sikwenda

Nikakutana na mmama mmoja alikuwa anafuata mahindi mashambani nilikuwa namsaidia kutafuta usafiri na kusimamia shughuli zake ananilipa kidogo alikuwa mtu mzima sana kwangu lakin dhiki hizi dadangu tukaanza mahusiano kidogo nikapata chumba chenye nafuu tukatoka jikoni kwa yule bibi angalau tukaweza kula hata milo miwili

Katika mahusiano aliniahidi atanifundisha udereva kisha kuna kazi atantafutia nikaona mwanga kidogo unakuja nilikuwa na miaka 17 wakati huo kwa nje usingejua tuna mahusiano, hata mimi sikuwa na namna

Tumeenda hivyo kwa siri siku moja alikuwa ananiita kwenye nyumba flani iko mbali na mji ndo tunakutania huko siku hio tumefika kule tukavamiwa na mme wake kukuta ni mm aliamini kabisa kadanganywa coz umri wangu na yule mama ni mtu mwanae kabisa alikuwa na miaka 52 basi pale akanitambulisha kwa yule baba kuwa mm huwa namsaidia mizigo na uzuri ile nyumba ilikuwa inatumika kama stoo na ulikuwa mchana kama saa sita hivi nilinusurika hapo

Yule mzee akaanza kuniita na kunituma pia ndio akaniuliza asili yangu na ndio kujua anamjua bibi yangu na yeye huyu baba ndo aliniambia mama yangu alizaaga na mtu, na inasemekana ndie aliyemfundisha kutumia drugs, alikuwa mtu anayejulikana tu mitaa fulani pale mjini *** na mama kabla ya kuanza kutumia alikuwa anafanya kazi hapo mjini yaani alikuwa mtu aliyeanza kusimama kimaisha na si haba alisomasoma ila madawa Laura asee mamangu natamani asingeingia uko labda leo ningekuwa na historia tofauti

Basi nilimtafuta babangu mpaka nikampata lakini wala hakuwa na msaada coz nae alikuwa na hali mbaya mno kimaisha na kiafya halafu watoto wake hawakutaka kabisa kunisikia kwahio nikamjua lakini hakuwa na msaada

Mahusiano yangu na yule mama yaliendelea alikuwa ananisaidia hata mahitaji muhimu ya shule na matibabu ya wadogo zangu nlikuwa nasubiri anipe kazi rasmi ya mshahara na kusomeshwa udereva ili nijitegemee mazima ila chenga zilikuwa nyingi kuna muda mpaka alinitishia atowahudumia wadogo zangu au hatanipa hela dogo akiumwa,

Laura kuna wakati hata elfu 10 tu unaitafuta kwa nguvu nyingi sijui kuna mtu anaelewa hili mtu akikupa hata elfu 2 inakuwa kubwa kwenye bajeti, tulienda hivyo mpaka ikafika siku moja mbaya sana maishani mwangu,

Yule baba aligundua kinachoendelea kwa ushahidi, tukiwa mashambani tunakusanya mizigo alituma watu kunichukua kinguvu nilipigwa sana mpaka nikawa sioni mbele mmoja akanifanyia ubaya ambao kidogo uondoke na maisha yangu siwezi kusahau ilikuwa nifie kule ila Mungu alitaka niendelee kuteseka nikaokotwa kama siku mbili mbele sina nguo mwilini na nimejaa majeraha,

Siku hiyo hospitali alikuja mshikaji flani kuniona akaniambia maneno mengi mtaani wanajua nilichofanyiwa na pole nyingi ananipa lakin alipoondoka akaja yule jamaa aliyetupokea mara ya kwanza akanambia unajua akamtaja aliyeondoka ndo kakuchomea kwa mzee,

Nikaamini coz alishawahi kuniuliza mbona niko cloz na huyu mmama nikamwambia ananitaka ila mi napotezea hata hela nilikuwa nikipewa nyingi nae nampa hela ya maji maana alikuwa na dhiki tu kama mimi, basi jamaa akaniambia nikimbie ukute katumwa kuona nikoje watanirudia,

Tulitumia baiskeli kuondoka pale, safari ile ilibidi anifunge na khanga kunishikamnisha nae kama maiti ili nisianguke, ilibidi nikimbie kabisa nje ya ule mji nikaacha wadogo zangu nyuma kuokoa uhai wangu, tulikwenda hadi stendi ya mbali tukapanda basi.

Nilikimbilia *** sina ndugu sina mtu hata afya sina, kufika akanikodia gesti moja uchwara akaniambia nitulie siku chache yeye anarudi kule waliko wadogo zangu, kuna mdada wa gesti ndio alikuwa ananicheki ananihudumia ila ilibidi nitoke na hayo majeraha nikatafute hela coz aliniambia kuna kazi mahali na hela nilolipiwa ilikuwa inaishia, hata watoa kazi walinishangaa ila nilipiga magoti nikaomba nipewe nafasi nitafanya huku napona, Mungu akanitetea katika watu 10 na mimi nikachukuliwa

Nikawa naenda narudi pale gesti sina hata simu ya kujua ndugu zangu wana hali gani, kurudi pia naogopa plus aibu ya kile kilichotokea nikawa najipa moyo kikubwa wako chini ya jamaa maisha yataenda. Pale *** nilikaa miezi nane hivi hadi nikaanza kuwa mwenyeji wakati najipanga nauli na makazi niwalete ndugu zangu pale, malipo ya kibarua yalikuwa madogo sana ila ndo ni bora kuliko kukosa kabisa

Siku nakwenda kule Laura nilitokwa na machozi kumkuta mdogo wangu wa pili tayari analalwa na wanaume kwa ajili ya hela amlee mdogo wetu wa mwisho, jamaa wala hana habari nisiseme sana hili niliumia sana maana wadogo zangu waliponiona walilia kama vile kuna msiba mkubwa umetokea, kitu cha kwanza mdogo wangu alinishika miguuni akaniomba tuondoke wote,

Usiku ule ule tukaondoka sikusubiri hata jamaa arejee ukute mpaka leo atakuwa anasimulia kuwa sina shukuran ila Mungu anajua hisia zangu na yale aliyoweza kunitendea nashukuru kwa moyo wote. Tukarudi kule mimi na wao tukaishi chumba kimoja

Basi maisha yameenda, katika kazi ilitokea tu meneja akawa ananiamini sana kidogo kidogo akaanza kunishirikisha dili zake nje ya kazi, tulikuwa na biashara fulani ya magendo nikaanzia hapo kupata hela ya maana angalau

Nimepiga magendo mpakani *** baadae nikapata connection nikavuka boda mpaka SA kule maisha yalinikaba kidogo yalikuwa mazingira ya kukaa roho juu sana nikarudi, kipindi hiki nilikuwa na mwanamke ndo alibaki na wadogo zangu.

Kulikuwa na biashara nimefungua anasimamia huyo mwanamke, kurudi nikakuta biashara imelala kushoto yaani biashara ya mtaji mkubwa sana imeporomoka, nilitaka kuingia wehu ikabidi niuze eneo nilinunua ili nianze tena. biashara haikusimama vizuri nikaanguka tena yaani kila nnachofanya sasa kikawa kinateleza.

Kuna jamaa alikuwa ana hela ni mfanyabiashara nikafanya kila njia nikaonana nae nikamueleza biashara yangu na matatizo yeye alikuwa tayari kunipa mtaji ila sharti alinipa ni kupeleka damu. Utajua utakakoitoa ila yeye mpekee lita ya damu anakupa hela

Ugumu wa maisha kwa mwanaume ni ukatili unaotisha maana watu hawatarajii ushindwe au ukwame pili nilikuwa naogopa sana kurudi maisha ya chumba kimoja na wadogo zangu, kule nilikopita sikutaka kabisa kurudi, lakini inshu ya damu pia ikanishinda ikawa basi,

Laura nikatoka kwenye kumiliki biashara pikipiki na kiwanja mpaka kuuza maji kwenye toroli kwa kifupi nilifirisika, nilijaribu kuigiza nipo sawa ila pesa sina nikaona nikikomaa kuigiza nitashika bunduki nifanye uhalifu,

Nikakubali matokeo ambayo unajua dada mitaa yetu ukiporomoka unakuwa mfano mbovu kwa kila mtu na kituko kila unakopita na mwanamke akanikimbia pia nilirudi yale maisha niliyoyaogopa ya chumba kimoja na hivi wadogo zangu wakubwa acha dada yale sio maisha

Nimeuza maji sana, life imeenda mdogo wangu akapata mimba yupo shule, akanificha akaenda kutoa kienyeji nakuja kuitwa yuko nusu mfu ilikuwa na maana gani mimi kumpambania? Alipoteza mtoto yeye akanusurika, Ule wakati nilitamani mama au bibi wangekuwepo, hilo tukio ndio lilifanya niuze kila kitu nikaondoka na ndugu zangu mpaka ***

Nikaenda kuanza upya na vibarua kiwandani, nimefanya sana nikapata mtu pale pale akanishika mkono akaniambia kuna watalii wanakuja dili ni hili. Mi lugha ilikuwa haipandi sana ila kujiamini ndio kila kitu, nikakutanishwa na hao watalii.

Kuna vitu siwezi kuandika sana Laura ila mtalii mmoja alinipa mchongo wa kwenda uko kwao kupitia shirika linalofanya kazi hapa nchini, wadogo zangu ikabidi niwaweke chini niwaambie hakuna wa kuwalea tena isipokuwa wao kwa wao, wakati mimi naondoka

Basi process zilifanyika miezi kama nane hivi nikawa tayari kuondoka, nikamwacha mdogo wangu wa pili kwenye chumba cha kupanga, mtu pekee nilimwomba awaangalie ni mmama alikuwa anaishi hapo tulipopanga

Maisha ya kule nje hayakuwa rahisi ni kazi kazi kazi muda wote lakini ndiko nilikopatia nafasi ya kujenga upya maisha yangu, kidogo nikipata namtumia mdogo wangu ambaye alianza kujifunza kushona hapo mtaani, tumeishi hivyo kwa miaka, niliporudi nikanunua kiwanja nikaanza ujenzi nikaondoka tena, niliporudi nikakuta mdogo wangu ana mtoto, sikuwa na jinsi

2021 mdogo wangu wa mwisho akafariki, ikabidi nirudi kumzika. Tukabaki wawili na mpwa wangu. Nikaanza process za kumchukua mwenzangu aje huku kupumzika, tukiwa tumeshaandaa kila kitu

2022 mdogo wangu na mpwa wangu walikwenda kijijini kule alikozikwa mama, alitaka kuwaaga mama na bibi wakati wanarudi wakapata ile ajali ya *** nao walikuwa mingoni mwa waliofariki, usiniulize nilikuwa na hali gani 2023/24 siwezi kuelezea

2025 ninavyokuandikia nimebaki mimi tu na picha za watu wangu niliowapenda. Ukiniuliza maana ya maisha sina jibu Laura, hayo ndio maisha yangu mimi, watu wakiniona kwenye haya mabarafu wanasema *** kayapatia maisha hawajui ni kwenye hizi barafu huwa ninalia peke yangu na kutamani niamke niwe japo na ndugu zangu. Sasa hivi ndio wajomba na mama wadogo wananitafuta sana nasalimiwa sana lakini vyote havina maana kwangu

Hawajui nishatamani kujirusha kwenye hizi treni nawafuate wenzangu kumbukumbu nyingi zinaniumiza sana, katika madarasa uliyokuwa unaandika nilipata faraja kubwa kuyasoma niliona kama unaongea na mimi japo sikujui ile channel ya darasa kule youtube irudishe siipati tena ile ilikuwa Therapy kwetu tunaoijua depression. Ninamiliki vitu nilivyoota kumiliki ila sina wale watu niliopambana waje kuvifurahia.

MWISHO!

CREDIT-
LAURA PETTIE
 
Back
Top Bottom