Malisa Godlisten
JF-Expert Member
- Jan 20, 2010
- 201
- 1,536
Kauli ya Rais kuwa watuhumiwa wa ujambazi wanaokamatwa na silaha wasipelekwe mahakamani bali "wapandishwe cheo" ina maana gani? Nini maana ya "kupandishwa cheo" kwa mtuhumiwa wa ujambazi?
1. Kusamehewa
2. Kuuawa
3. Kunyang'anywa silaha
4. Kutubu
5. Mengineyo...
Na kwanini "Rais wetu mwema" asingesema "wapandishwe cheo" baada ya Mahakama kudhibitisha tuhuma zao? Ina maana Rais wetu hana imani na mahakama?? Kuruhusu Polisi "kupandisha cheo" watuhumiwa wa ujambazi sio kukiuka utawala wa sheria?
Je Rais haoni kwa kauli yake hiyo atasababisha watu wengi wasio na hatia "kupandishwa cheo" kwa kusingiziwa tu ujambazi?? Yani Polisi kama ana kisa na wewe anakubambikizia tu silaha kisha "anakupandisha cheo" bila kukufikisha mahakamani. Je huku si kukiuka misingi ya haki za binadamu na utawala bora?
Unakumbuka wale wafanyabiashara wa Ulanga "waliopandishwa cheo" kwa kusingiziwa ni majambazi na Kamanda Zombe lakini baadae ikaja kubainika kuwa hawakuwa majambazi?? Kwanini Rais ameruhusu Polisi "wapandishe watu vyeo" kwa tuhuma tu, wakati mahakama zipo??
Malisa G.J