Neno "Kudadeki" (au kudadadeki) ni neno la mtaani (mseto wa Sheng na lugha ya kihuni/mitaani ya Kiswahili) linalotumika kama kiingishi cha kusisitiza hisia kali kama vile mshangao, hasira, msisimko, au msisitizo mkubwa.
Asili yake ni neno la matusi yaliyolenga dada wa mtu, lakini limefanyiwa mabadiliko ya kifonolojia ili kupunguza ukali na unyanyasaji wa lugha. Leo hii hutumika kwa namna tofauti kulingana na muktadha
We jamaa nilikuwa nakutafuta muda mrefu sana, kudadeki leo nimekubamba!, kudadeke leo nitapiga mtu kama sitalipwa hela yangu. Ni neno la kuhanikiza mshangao kwa kilichotokea kwa shauku kubwa