Nini maana ya honours degree?

Nini maana ya honours degree?

Nahisi pamoja na maelezo yenu chuo na senet yake pia wanaweza kuamua kutoa honours degree kulingana na matukio flan flan mf : graduate Wa udsm wengi wamepewa hiyo mwaka Jana koz chuo kilitimza miaka 50 kipindi chao bila kuzingatia vigezo vya kitaaluma
 
mi GPA yangu sio kali ila sijawahi
kusupp,je ninastahili kuwa na
honour?
hujapata supp ila unafloat kwenye kiGPA cha 2.X mzee Hon. sio ya kwako, lazima uwe na atleast 3.5 in each end-of-the year reasult, na iwe inapanda mwaka hadi mwaka, na uwe hujawahi kupata supp hata moja, I got this info from Director wa school fulani hapa UDSM
 
Vigezo vinatofautiana kulingana na vyuo na pia prospectus ya mwaka huo. Nilipohitimu mm kwa mwaka huo ilikua ni kwa GPA ya kuanzia second class isiyokua na supp. Bila kujali inapanda au inashuka.
 
Kuna jamaa yangu alikua ame carry lkn pia ana 2.8 alipata honour
vyuo gani hivyo mtu anakula supp, anafeli tena anakula carry, ana GPA ya 2.X na anakula Hon. Degree?? au ndo vyuo vyenu vya Bahari University?? ...sasa ingekuwa hivyo si graduates wote wangekuwa wanakula Honorary
 
Kwa ufahamu wangu, kwa vyuo vingi hapa nchini, mtu anaweza kupata shahada ya heshima (Honours degree) endapo atakuwa amefaulu masomo yake yote (At fisrt sitting bila kuwa na Supplimentary au carry-over.....) kwa kiwango cha first class au upper second......vilevile, consistency katika kiwango cha ufaulu kwa kila semister ni moja ya vigezo muhimu ili uweze kupata Honours degree kwa hapa nchini...... UDSM ni moja ya vyuo hapa nchini vinavyofuata kanuni hii katika kutoa Honours degree (e.g. katika prospectus ya UDSM 2012/13 kipengele cha 12.8 kinaelezea award ya aina hii)

Kwa nchi kama South Africa, Honours Degree ni programme inayojitegemea kabisa (ni postgraduate programme inayofundishwa kwa mwaka mmoja kama moja ya requirements za kujiunga na Masters kwa wale wenye qualifications zinazotambulika na South African Qualification Authority), vilevile, baada ya kumaliza undergraduate mtu anayehitaji kuongeza ubobezi katika fani aliyoisomea atalazimika kuongeza mwaka mmoja wa ziada ili kusomea Honours degree kwa ku-specialize katika somo moja.

NOTE: Kuna utofauti kati ya Honours degree niliyoizungumzia hapo juu na Honorary degree ambayo pia hutambulika kama Degree of Honoris Causa inayotolewa kwa lengo la kutambua na kuheshimu mchango wa kipekee wa mtu (ambaye siyo lazima awe na mahusiano yoyote ya kitaaluma na chuo husika) katika jamii kwa ujumla.........bila kujali sababu za kutolewa kwa Honorary degree, aina hii ya heshima haina uwiano sawa na Honours degree ama kutambulika kama moja ya qualifications za kitaaluma katika maeneo ya ajira au kwa malengo ya kitaaluma na mara nyingi kwenye CV Honorary degrees hukaa upande wa awards tofauti na Honours degree ambayo ni academic qualification. Hadi kufikia mwaka jana (2015) Mchungaji Theodore Martin Hesburgh ambaye alikuwa kiongozi wa chuo cha Notre Dame nchini Marekani ndiye aliyekuwa anashikilia rekodi ya dunia kwa kuwa na awards nyingi za aina hii (Ana Honorary degrees zaidi ya 150).
 
Binafsi nimewapata ,binafsi nasubiri graduation soon ,swali langu je hyo degree y heshima kutawekwa nn kwenye cheti or elsewhere kuonyesha uwepo wake?
 
Binafsi nimewapata ,binafsi nasubiri graduation soon ,swali langu je hyo degree y heshima kutawekwa nn kwenye cheti or elsewhere kuonyesha uwepo wake?

Mara nyingi Honours degree huoneshwa kwa kuweka ufupisho wake mbele ya ufupisho wa jina la degree husika....e.g. BA. Economics (Hons) au kwa kirefu Bachelor of Arts in Economics (Hons).
 
Back
Top Bottom