a fikra_og
Member
- Jan 1, 2019
- 8
- 1
Umepewa link hapo juu, fungua
Na tatizo kubwa hapa ni ukosefu wa elimu....serikali iko kimya na inakuwa makini Kwenye kuwahukumu wale waliowauwa watafiti kule Dodoma lakini, Watanzania wengi bado hawafahamu Freemason ni nani hasa, wanashughulika na nn, nk.nk...Ilikuwa kundi la wajenzi waliokuwa na maisha duni sana na walikuwa wanateswa sana na watawala na waajiri wao.......waliamua kujiunga pamoja wakaunda chama na hatimae kufanikiwa kuwa na uchumi mkubwa sana na wakawa na wanachama dunia nzima na wakawa na uwezo na ushawishi mkubwa kutoka kudharaulika na waliweza kutumia ushawishi wao wa kifedha na kijamii kweza hata kupandikiza baadhi ya viongozi kwenye baadhi ya nchi na mashirika.
Hawana uhusiano wowote na ushirikina ama mauzauza kama wajinga wanavyodanganywa hapa Bongo. Wamejikita katika kufanya tafiti za biashara mbalimbali zinazolipa haraka kinyume na hapa bongo wanapowahusisha na umwanamalundi.
Natahadharisha baadhi ya waandishi uchwara , na wahubirei mbalimbali wanaopotosha hilu suala kupitia kwenye vimagazeti na mimbari mbalimbali za mahubiri kwamba eti wana nguvu za kiza za kuua watu, kutoa makafara na kupata pesa kwa njia ya majini.
Huu ni uongo mkubwa na umesababisha tafurani kwa jamii mbalimbali za kibongo, mfano ukitajirika gafla na watu hawakujua chanzo cha fedha zako wanaita freemarson, hasa vijijini unaweza kwenda kijijini kwako wakakukimbia ama ukiwapa msaada hawataki biashara za kidijitali zipo nyingi za online siyo lazima mtu afungue duka ama kulima shamba ndio apate fedha.
Jambo hili limeleta madhara makubwa na kusababisha baadhi ya watafiti kutoka arusha kuuawa huko dodoma wakihisiwa ni freemason kadhalika kuna baadhi ya watu vijijini walikimbia fedha za maendeleo kwa kaya maskini TASAF wakihisi ni za majini . Zaidi ya hapo matapeli mbalimbali mijini ndio wanatumia fursa hiyo kuwaibia wajinga eti wanakuunganisha na freemarson, Matangazo yao yapo kwenye miji mikubwa na namba za simu wameweka matapeli hao nashauri mamlaka ziwasake na kuwatia mbaroni.Tujitahidi kuelimisha jamiii iondokane na ujinga huu, na wale wapotoshaji wachukuliwe hatua.
A Fikra_ogIlikuwa kundi la wajenzi waliokuwa na maisha duni sana na walikuwa wanateswa sana na watawala na waajiri wao.......waliamua kujiunga pamoja wakaunda chama na hatimae kufanikiwa kuwa na uchumi mkubwa sana na wakawa na wanachama dunia nzima na wakawa na uwezo na ushawishi mkubwa kutoka kudharaulika na waliweza kutumia ushawishi wao wa kifedha na kijamii kweza hata kupandikiza baadhi ya viongozi kwenye baadhi ya nchi na mashirika.