Ninavyojua mimi, double-standard ni UBAGUZI au UTABAKA (Strata) yaani kama ilivyoelezwa hapo juu kwamba unamhudumia huyu kwa kiwango hiki na mwingine kwa kiwango kingine wakati ilipaswa wote wawe viwango sawa. Mfano kuna idara fulani ya maji huko Arusha ina wateja wenye mita na wanalipishwa zaidi ya elf 40 kwa mwezi wakati wateja wengine hawana mita wanalipa flat-rate elf 7 tu kwa mwezi hata maji yangemwagika mwezi mzima. Neno zuri la undumilakuwili ni double-agent. Nisaidieni kama nimeelewa vibaya...