Nini maana ya Azimio la Zanzibar?

Nini maana ya Azimio la Zanzibar?

Zitto

Former MP Kigoma Urban
Joined
Mar 2, 2007
Posts
1,562
Reaction score
10,890
Nini maana ya Azimio la Zanzibar?

Vyama 6 vya Upinzani nchini vimetoa maazimio kadhaa mazito Kuhusu hali ya Demokrasia ya vyama vingi nchini Tanzania. Kwa ujumla maazimio hayo yanaitwa Azimio la Zanzibar. Maana yake nini?

Maana yake ni Kwamba Vyama vya Upinzani nchini vinachukizwa na vitendo vinavyofanywa na Serikali ya Rais Magufuli dhidi ya Viongozi, wanachama na wafuasi wa Vyama vyao kwa kuwafungulia kesi na kuwasweka magerezani. Kuwatangaza Freeman Mbowe na Esther Matiko kuwa wafungwa wa kisiasa Maana yake ni kuiambia dunia kuwa nchini Tanzania sasa watu wanafungwa kutokana na imani zao za kisiasa. Kesi iliyowaweka mahabusu Mbowe na Matiko inaangukia kwenye tafsiri ya Wafungwa wa Kisiasa Kwa mujibu wa Shirika la Amnesty International. Hivyo wanapaswa kuachiwa mara moja. Hii ni mara ya pili kwa wanaharakati za kisiasa nchini kutambua wenzao kama ‘political prisoners’. Mara ya kwanza ilikuwa Mwaka 1991 ambapo Kamati ya Mageuzi ( NCCR ) Katika Mkutano wake wa kidemokrasia ilimtangaza Maalim Seif Shariff Hamad kuwa ni mfungwa wa kisiasa. Serikali ilimwachia huru mara baada ya Tamko hilo.

Freeman Mbowe na Esther Matiko watakuwa ni alama ya mapambano dhidi ya ukandamizaji wa haki za Watu.

Vyama vimeamua kudharau amri batili ya Rais John Magufuli kuzuia mikutano ya hadhara. Hivyo Mwaka 2019 Vyama vitaanza kufanya mikutano ya hadhara kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi bila kujali agizo la Rais. Huu ni uamuzi wa kimapinduzi uliochelewa, uamuzi wa kukataa kutii amri batili isiyoheshimu Katiba na Sheria za nchi. Kwa uamuzi huu Vyama vimeamua kupigania Demokrasia kwa vitendo na kuendesha kampeni ya kuheshimu Katiba inayoruhusu Vyama kufanya mikutano. Kwa ufupi Vyama vimetangaza vita dhidi ya udikteta. Kamati ya Pamoja ya Vyama itatangaza ratiba ya kuanza kwa mikutano ya hadhara kwa mujibu wa sheria mara baada ya Vyama kuidhinisha ( ratification) Azimio la Zanzibar kwenye vikao vyao na kuwasilisha nyaraka ( instruments of ratification) kwenye Kamati hiyo.

Vyama vimesisitiza kuwa havitambui Serikali ya Zanzibar chini ya Ali Mohammed Shein. Vinataka haki ya Wazanzibari kuchagua Viongozi wanaowataka iheshimiwe. Vyama vitachukua kadhaa kuhakikisha kuwa Zanzibar inapata Serikali iliyochaguliwa na Wananchi wa Zanzibar Oktoba 25, 2015.

#AzimioLaZanzibar limesema SASA BASI. IMETOSHA. AZ limetangaza vita itakayoweka misingi ya kuheshimiana miongoni mwa Viongozi na Kati ya Viongozi na Wananchi. Misingi ya Demokrasia ya kweli na kuondoa udikteta Tanzania.
 
AZIMIO LA ZANZIBAR, ni makubaliano kati ya watu wa Marekani na vibaraka wa karne ya 21 wanaoishi Tanzania kwa manufaa ya watu wa Marekani.
Sawa wacha waje tumechoka na utawala huu wa mkoloni mweusi na vibaraka wake watu wasiojulikana.
 
AZIMIO LA ZANZIBAR, ni makubaliano kati ya watu wa Marekani na vibaraka wa karne ya 21 wanaoishi Tanzania kwa manufaa ya watu wa Marekani.
Unatia aibu kubwa sana , na ni hasara kubwa mno kwa wazazi wako na kila aliyekubeba ulipokuwa mchanga , namshukuru Mungu kuniepusha kupata mtoto kama wewe .
 
Mikutano kwenye majimbo yenu inaruhusiwa lakini hamfanyi.

Si mbowe ,zito, mdee wala mnyika anayefanya mkutano jimboni kwake wakati mnaruhusiwa.kwa nini?

Chadema ni washamba wa kisiasa na mtandanganya wajinga wenzenu tu
Hahahahahaaaaa,kwani ni lazima kufanya mkutano?Mnawategea ili muwasweke ndani?
 
Na sisi wananchi tunakubaliana kuwa sasa basi tumechoka na uonevu
 
Mikutano kwenye majimbo yenu inaruhusiwa lakini hamfanyi.

Si mbowe ,zito, mdee wala mnyika anayefanya mkutano jimboni kwake wakati mnaruhusiwa.kwa nini?

Chadema ni washamba wa kisiasa na mtandanganya wajinga wenzenu tu
Kwahiyo Msigwa anapozuiwa kufanya mikutano Iringa mjini halikuwa jimbo lake! Acha ukibaraka uchwara.
 
Back
Top Bottom