Nini maana halisi ya Interchange?

Nini maana halisi ya Interchange?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
137,573
Reaction score
272,319
Je, ni kama picha hii?

Au hata barabara iliyokaa kama msalaba kwa maana ya kutoka kulia kwenda kushoto na kutoka nyuma kwenda mbele nayo yaitwa Interchange?

Lengo la uzi huu ni kujifunza tu ili kuongeza ujuzi.

Naomba kuwasilisha.

FB_IMG_1614177975354.jpg
 
Katika fani ya usafiri wa barabara, interchange ni makutano ya barabara ambayo yanatenganisha barabara kwa wimo tofauti ili kuruhusu magari ya upande mmoja kupita katika makutano ya barabara bila kukutana/kupishana njia na magari yanayotokea upande mwingine.

Kwa kifupi interchange inahusisha barabara moja au nyingine kupita juu ya nyingine katika mielekeo tofauti.

Kuna aina saba za interchange kutokana na mkao na mpishano wa barabara. Aina hizo ni kama ifuatavyo:

.1 Cloverleaf interchange.

2 Stack interchange.

3 Cloverstack interchange.

4 Turbine interchange.

5 Windmill interchange.

6 Other "windmill" interchange.

7 Roundabout interchange.

8 Hybrid four-way interchanges.

Hii ya kwetu pale Ubungo ni muunganiko wa Stack Interchange na Roundabout Interchange.
Hii ya kwetu inayojulikana kama Kijazi interchange kwa juu inaonekana kama hybrid lakini kwenye design ni muunganiko wa stack na roundabout.
Ni miongoni mwa design bora kabisa katika interchange.

Interchange yenye kimo kirefu zaidi duniani ipo Dallas Marekani ambayo barabara tano zinapishana kwa juu. Hii inajukana kama Dallas Fort Worth Metroplex..

Interchange maarufu barani Africa ni ile ya Mount Edge Combe mountain - South Africa ambayo ndio kubwa zaidi kwa Kusini mwa jangwa la Sahara, Kwame Nkurumah Circle Interchange pale Accra Ghana.
Kwa wasiojua tu, moja kati ya interchange ambayo timu ya Tanzania ilikwenda kuitembelea ni hii ya Kwame Nkurumah Circle pale Accra, Ghana.
........
In the field of road transport, an interchange is a road junction that uses grade separation, and typically one or more ramps, to permit traffic on at least one highway to pass through the junction without interruption from other crossing traffic streams. Interchange is a grade-separated intersection(one road passes over another) with ramps to connect them.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Namimi ngoja nijifunze kupitia huu uzi, ila twende mbele turudi nyuma ile kitu (Daraja, Interchange, Flyover) vyotote vile itakavyoitwa imesaidia sana lile eneo, KUDOS kwa WALIPA KODI.
Sure mkuu ifike mahali tujipongeze tunapoona kodi zetu zinatumika ipasavyo. Wakikosea pia tunawapasua kama kawaida kuwa mpinzani haimaanishi tupinge kila kitu.
 
Katika fani ya usafiri wa barabara, interchange ni makutano ya barabara ambayo yanatenganisha barabara kwa wimo tofauti ili kuruhusu magari ya upande mmoja kupita katika makutano ya barabara bila kukutana/kupishana njia na magari yanayotokea upande mwingine...
So tunakubaliana pale ni sahihi kuitwa kijazi interchange?
 
Katika fani ya usafiri wa barabara, interchange ni makutano ya barabara ambayo yanatenganisha barabara kwa wimo tofauti ili kuruhusu magari ya upande mmoja kupita katika makutano ya barabara bila kukutana/kupishana njia na magari yanayotokea upande mwingine....
Asante sana mkuu
 
Nia ya ndani kabisa ya mwandishi ni Ujinga wa kiupinzani usiosaidia kitu na ndio huo ujinga uliwakera wananchi wakaamua kutoa Adhabu ya karne
 
Katika fani ya usafiri wa barabara, interchange ni makutano ya barabara ambayo yanatenganisha barabara kwa wimo tofauti ili kuruhusu magari ya upande mmoja kupita katika makutano ya barabara bila kukutana/kupishana njia na magari yanayotokea upande mwingine...
Mkuu, nilijua wewe ni kwenye kula kimasihara tu kumbe hata kwenye mambo ya kitaalam pia unashusha nondo.
 
Back
Top Bottom