Nini Kosa la WaPemba as they road to UN.

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,745
Mwaka 1967, Rais Julius Nyerere aliunga mkono kampeni ya wananchi wa Biafra, nchini Nigeria, kutaka kujitenga. Alipeleka jeshi kule kwenda kusaidia wapiganaji wa kundi la MASSOB (Movement for Actualisation of the Sovereign State for Biafra) likiongozwa na Ogumu.
Ogumu na Yakoub Gowon aliyekuwa Rais wa Nigeria wakati huo, leo ni wajumbe wa Baraza la Ushauri la Serikali ya Rais Al Yaradua wa Nigeria.

Wabunge wa Mtwara waliwahi kuitaka Serikali iwaachie wajiunge na Msumbiji ambako ni karibu nao kwa kuwa serikali yao haitaki kuwajengea miundombinu ya kurahisisha shughuli zao za maendeleo. Hawakukamatwa.

(Marehemu) Sebastian Kinyondo alipokuwa Mbunge miaka ya 1990, aliwahi kuitaka serikali iwaachie wananchi wa Mkoa wa Kagera wajiunge na Uganda kwa kuona serikali yao haitaki kuwapatia huduma za jamii kama vile umeme na usafiri wa uhakika. Hakukamatwa.

Wabunge 55 waliounda kundi maarufu likiitwa G55 waliichagiza serikali mwaka 1994 wakitaka irudishwe Tanganyika ili wawe na haki kama walivyo Zanzibar. Hawakukamatwa.

Mchungaji Christopher Mtikila anaamini mpaka leo yeye ni Mtanganyika na angependa itambuliwe hasa Tanganyika ipo. Pamoja na Jamahuri kumfungulia kesi mbalimbali, hakuna kesi kwa hilo. Hajawahi kukamatwa.

Leo Polisi wa Tanzania wanakamata wazee wa Pemba wanaodai haki ya kushirikishwa katika uongozi wa nchi yao. Wangekuwa wabunge, wangedai haki hiyo bungeni, wangekuwa wanasiasa wangedai haki hiyo kwenye jukwaa la kisiasa. Hawa ni raia tu, wameandika barua na kuipeleka Umoja wa Mataifa, tena mchana kweupe.
(From Jabir Idris)
 
Zanzibar si nchi bali ni sehemu ya Tanzania kama vile ilivyo Tanga, Morogoro, Arusha Iringa nk. Hivyo Karume kule Zanzibar ni mkuu wa mkoa. Hapa nakubaliana kwamba Tanzania ina watu wasanii. LAKINI NDUGU ZANGU WA VISIWANI MPAKA KIELEWEKE. ZANZIBAR NI NCHI TAKA WASITAKE. NI BORA WATUACHIE NCHI YETU MAPEMA.
 
Back
Top Bottom