Nini kitatokea ikiwa haya yatashindikana?

dguyana

JF-Expert Member
Jan 17, 2011
423
110
Katiba Mpya
1. Wananchi tunaijua Katiba ya zamani?
2. Ni lini kamati ya katiba mpya itapita hapa nilipo? Je maoni yatafika vile yalivyokusanywa? Utadhibitisha vipi kama mawazo ya wengi yamepewa nafasi kwenye katika mpya?
3. Nini mstakabali wa taifa juu ya upotevu wa hela zitakazopotea kutokana kama zoezi litashindikana au kufanyika ndivyo sivyo?
Utambulisho wa Uraia.

1. Wananchi tunajua maana ya zoezi hili?
2. Kuna tofauti gani kutambulika kwa kutumia kadi yangu ya kura na hiki kitambulisho? Uendeshwaji wa zoezi zima la uandikishaji wananchi wanalichukulia vipi na usimamizi wake ukoje ikiwa tunasikia baadhi ya watu wanalipishwa hela?
3. Nini mstakabali wa taifa juu ya upotevu wa hela zitakazopotea kutokana kama zoezi litashindikana?
Sensa.

1. Kuna uwezekano wananchi wengi wanao uelewa juu ya hili si geni ila, sasa tunasikia Viongozi wa dini moja wanapinga na wengine wapo kimya vipi hapa hakuna mtu wa kutatua hili? Itakuwaje wakikata kushiriki kiuweli?
2. Nini mstakabali wa taifa juu ya upotevu wa hela zitakazopotea kutokana na zoezi kushindikana?

My take- Hapo juu ni views zangu tu. Mimi katiba ya zamani siijui ki ukweli ila mwenye kujua maana ya mazoezi hayo hapo juu naomba atusaidie tusiojua ila japo tuchore raman ya nini kitakuja baadae.

Ifikie wakati WaTZ tutumie resourse zetu kama JF tulizonazo kutatua changamoto na kuelimishana.
 
Back
Top Bottom