Nini kipimo cha maisha bora? Maisha bora yana maana gani kwako?

james nderimo

Member
Jul 7, 2011
20
0
Habari zenu, kabla sijaanza kuelezea uzi huu. Mimi naamin,( God was very serious, creation ya ulimwengu, na vyote alivyojaza, alifanya kwa umakini mkubwa, hamna anaesema. Huu mlima au bahari, ingekaa upande wa mashariki na sio magaribi. Hivyo mimi kama mwanadamu, inanipasa niwe serious kwa jambo ninalo lifanya, (kupenda, maendeleo, imani)chini ya ulimwengu ulio umbwa kwa umakini wa juu.) I take my life very serious and wishing for more wisdom, nd not less problems. ) Turudi kwenye hoja yangu.

Kila mtu anatamini kitu kinacho itwa "maisha mazuri/bora" ngoja niwaulizwe swali. Maisha mazuri mni yapi haswa? Nini hubadilia kutoka kwenye maisha duni mpaka maisha bora?

Na uhakika ukiuliza watu mia hili swali, majibu mia tofauti yatapatikana . Pamoja na majibu tofauti lakini bado kutakuwa na majibu yanayoendana, majibu muhimu ambayo yatamgusa kila mtu.

JE UNAAMIMI UNAISHI MAISHA BORA/MAZURI.
Kama jibu lako ni hapana, basi nini kitakugarimu kuyapata? Hili ni swali refu na pana sana. Kama hutokaa chini na kujiuliza maisha mazuri na bora ni yapi kwako? Utawezaje kujua kama unaishi maisha mazuri na bora?

Wewe binafsi, ndo unahusika kujibu swali hili, wewe mwenyewe ndio unauwezo wa kutaka maisha mazuru na bora unayoyataka. Haya ni maisha yako tunayo ya ongelea. Vyombo vya habari(TV shows, movies) vinamchango au mtazamo tofauti sana. Na jinsi wanavyokuonyesha maisha bora ni yapi.

USIKUBALI WAO WAKUAMULIE NINI KIZURI NA NINI KIBAYA!
Wafanya biashara wa matangazo, hufanya kazi kubwa kukushawishi, kuwa maisha hayatokuwa mazuri, usipo nunua bidhaa zao. Mfano ( hamia airtel) nunua simu ya kisasa, au gari ya kisasa. Propaganda kama hizi, hutopotosha kabisa, na kusahau nini tunahitaji ili kuwa na maisha bora.
Ni kweli kabisa, mambo kama haya hutuweka mbali na maisha bora.
Watu wengine hudhani kuwa na pesa, ni kielelezo cha maisha bora, wengine hudhani vitu ambavyo pesa haiwezi nunua hayo ndo maisha bora/mazuri.

FEDHA INAMCHANGO GANI KWAKO?
Kusema ukweli ukiwa na pesa, ugumu wa maisha hupungua, na una relax. (Uhakika wa kula). Ni vizuri kusema, pesa inaweza ikawa ni kielelezo tosha cha maisha bora/mazuri. Hata hivyo tunawajua watu wenye pesa nyingi, lakini maisha yao sio mazuri. Kwahiyo pesa inaweza isiwe sababu ya misingi ya maisha bora.
Mtu mwengine anaweza kusema, maisha bora ni kumiliki mali nyingi. Kuna ambao wana mali nyingi, na vinageuka kuwa mzigo kwao. Kujifunza kupata haja za moyo wetu, inaweza kutusaidia kufikia maisha bora na mazuri.

VIASHIRIA 7 VYA MAISHA BORA.
Sasa basi vip ni viashiria vya maisha bora pamoja na maisha ya furaha? Hivi vyeto vinaweza kuwa vigezo muhimu, katika maisha yetu. Ili kuweza kufikia "maisha bora na furaha" kuna intrinsic needs. Hebu tuziangalie.
1. Uzalishaji mwenye maana.
2.Mahusiano mazuri.
3.Kujitambua kiroho(Dini/imani)
4.Afya
5.Akili(kuchambua mambo kwa fikra pevu)
6. Kuweka pesa inapostahili(matumizi)
7. Kupandikiza roho ya kujali.

Nimechoka. Ntaendelea. Kwa kuelezea hayo mambo 7.
 

bategereza

JF-Expert Member
Dec 26, 2013
3,316
0
Maisha bora. Uwe na mke na watoto 3
uwe na nyumba na kigari kimoja
uwe na uwezo wa kula mara 3 kwa siku na family.
uweze kunywa bia tano na nyama choma nusu kilo (baba)
Uwe na nyumba ndogo japo moja unayoipangishia nyumba Sinza (nyumba ndogo inaumuhimu wake nitaelezea bdy). usiwe na mtoto na hii nyumba ndogo.
Uwe na uwezo wa kuivisha familia na kuwasomesha vijana. Uwe na cheo msikitini kwako. mtu ukiwa na kipato cha kumudu hayo kwa mwanaume. utataka uongezewe nini kama sio mshipa ?
 

SaaMbovu

JF-Expert Member
Oct 8, 2013
5,987
2,000
1.Afya nzuri
2. Imani na Amani
3. Kupendwa na watu
wengi kwenye jamii yako
4. Kuwa muaminifu kwa kila jambo
5. Kuridhika kwa chochote unachopata.

Kwangu mie hayo ndio maisha mazuri, siwezi kusema kuwa na nyumba ndio maisha mazuri kwasababu baadhi ya watu wanatelekeza nyumba kisa hakuna amani ndani ya nyumba na wengine wakiwa na magari ndio yanawafilisi.
 

james nderimo

Member
Jul 7, 2011
20
0
Maisha bora. Uwe na mke na watoto 3
uwe na nyumba na kigari kimoja
uwe na uwezo wa kula mara 3 kwa siku na family.
uweze kunywa bia tano na nyama choma nusu kilo (baba)
Uwe na nyumba ndogo japo moja unayoipangishia nyumba Sinza (nyumba ndogo inaumuhimu wake nitaelezea bdy). usiwe na mtoto na hii nyumba ndogo.
Uwe na uwezo wa kuivisha familia na kuwasomesha vijana. Uwe na cheo msikitini kwako. mtu ukiwa na kipato cha kumudu hayo kwa mwanaume. utataka uongezewe nini kama sio mshipa ?

Hahaha, nyumba ndogo (epuka michepuko)
 

KAMP2015

JF-Expert Member
May 27, 2013
281
170
Maisha bora ni:
1 upatikanaji wa huduma bora za afya
2 utolewaji wa elimu bora
3 upatikana wa huduma za maji, umeme, barabara lishe kwa wananchi n.k
4 kupungua(hadi zero) kwa idadi ya vifo vya watoto na kina mama wajawazito
5 utawala bora unaozingatia mawazo tofauti na demokrasia
My take:kulingana na ccm ndo ilitakiwa kuwa hivyo lakini hakuna chochote
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom