Binafsi huwa nawakubali sana watu wenye uwezo mkubwa wa kufikiri ambao haufungamani na upande wowote. Ufikiri wake ni ule unaomuwezesha kufikiria jambo na kulipambanua hadi likafikia mwisho wake na hatimaye kupata suluhisho la tatizo lililokuwa likimkabili katika mazingira yake. Ufikiri huo ni ule unaolenga pande zote yaani mlengo hasi na mlengo chanya ambao hautomfanya muhusika kujutia maamuzi yake. Mfano, wengi huwa tunakuja kutambua baadaye kuwa la hasha, ningefanya hivi yasingetokea haya!