Nini kinazuia mji wa Moshi kuwa Jiji?

The Humble Dreamer

JF-Expert Member
Oct 12, 2015
7,440
10,233
Wakuu Salaam;

Mji wa Moshi ndiyo kitovu cha mkoa wa Kilimanjaro na kwa sasa hivi mji huu umepanuka kimaendeleo kulinganisha na miaka 15 iliyopita.

Sasa mji huu tangu mda tu haupandishwi hadhi ya kua jiji ilihali mchana kweupe tunaona kwingine kunapanda tu. Na sifa za huu mji zinajulikana zinazodhihirisha kua unastahili kua jiji.

Kipindi cha Mh. Amos Makala zilionekana dalili za kua jiji, na wakati JK alipokuja kwenye uzinduzi wa jengo la Uchumi alihaidi kuifanya kua jiji lakini haikufanikiwa. Ikakumbushiwa lakini hakuna.

Wazee wa mji na viongozi husika wameshajaribu vya kutosha lakini imeshindikana.

Miaka na miaka inazidi kwenda tukisubiri na wakati huu wa Jpm ndiyo kabisa hakuna chochote.

Sifa za mji wa Moshi zinajulikana kote na hivyo inastahili kua jiji.

Nini sasa kinazuia mji wa Moshi uliopo mkoani Kilimanjaro kua Jiji?
 
shida ni hao wazee wa kichaga wanakataa kwasababu mashamba yao wanataka yasipimwe viwanja implication ya kuwa jiji eneo litaongezeka na mashamba yote ya kuanzia kibororoni uchira na kwingine kote kutapimwa na wao bado wana mentality ya kulima mahindi soweto mule
 
Chadema wanasema mabarabara ya lami hayana faida, kupeleka umeme kila kijiji sio maendeleo
Katika Ilani ya ccm ya 2015/2020, kuna sehemu yoyote ambayo waliandika miradi kama airport chato, sgr, stigler, mbuga mpya n.k? Kama hawajafatisha ilani yao, nini maana ya kuwa na ilani?
 
Soma tena swali nililokuuliza, kisha angalia na jibu lako kama vinaendana.
Msingi wa swali lako linatokana na comment yangu uliyoni quotet niliyosema"Chedema jambo dogo wanasusa na kutoka bungeni"inamaana nafatilia bunge.
 
Chadema wanasema mabarabara ya lami hayana faida, kupeleka umeme kila kijiji sio maendeleo
Mtu akikuita mwanamke ilhali wewe ni mwanaume unabadilika kuwa mwanamke?

Kama kweli mmeleta maendeleo na wananchi wanayaona mna haja gani ya kujisumbua na CHADEMA.
 
Msingi wa swali lako linatokana na comment yangu uliyoni quotet niliyosema"Chedema jambo dogo wanasusa na kutoka bungeni"inamaana nafatilia bunge.
Msingi wa swali langu ni kuhusu kauli kwamba "Maendeleo hayana chama" ila Mwenyekiti huko anapopita anahubiri kitu tofauti
 
Mpendwa mtoa mada yaweza kuwa uko sahihi.

Ila naomba nikukosoe.
IDADI YA WATU ndiyo hufanya mahali fulani paitwe kijiji ,mji, au jiji.
Kwa sababu watu wakiwa wengi katika eneo fulani wanakuwa wamesukumwa na vitu potential zaidi ni kiuchumi.

ili sehemu iwe jiji nadhani ni lazima iwe na wakazi kuanzia million moja. Yaani hapo moshi mjini pawe na watu million moja.

Kwa mfano dar nzima ina wakazi million 4 jumla. Ila kwa makadirio yangu ni kuwa pale dar penyewe achana na huko Goba yaweza kuwa na watu kama 1.5 M.
So nipe statistics za hapo moshi pana watu wangapi
 
shida ni hao wazee wa kichaga wanakataa kwasababu mashamba yao wanataka yasipimwe viwanja implication ya kuwa jiji eneo litaongezeka na mashamba yote ya kuanzia kibororoni uchira na kwingine kote kutapimwa na wao bado wana mentality ya kulima mahindi soweto mule
Katika wote waliomjibu mleta uzi wewe ndio umeeleza sababu halisi na ya kweli. Manispaa ya Moshi ilishapata kibali cha kuanza mchakato wa kua Jiji miaka kadhaa iliyopita tokea enzi ya uongozi wa Bernadette Kinamo akiwa kama Municipal Director

Tatizo ni hilo kwamba watu wa maeneo ya Mbwa Haruki, Uchira, Sango n.k wamegoma mashamba yao kupimwa viwanja. Kwa sheria za mipango miji Jiji haliwezi tena kua na mashamba

Katika hili sio Serikali kuu inayoongozwa na CCM wala Manispaa ya Moshi inayoongozwa na CHADEMA ambayo inastahili kulaumiwa bali ni wananchi wenyewe wa Moshi ndio wanajichelewesha
 
Nyie Ndio mlianza siasa Baada ya lissu kutandikwa risasi
Hifadhi ya chato ilikuwepo hata kabla ya Rais Magufuli hajawa Rais wa Tanzania

Tatizo lenu ni washamba mnarukia rukia tu mambo
Asante kwa elimu ya bure ndugu mjanja.

Naomba pia unielimishe kama wanyama walikuwa wanahamishwa na magari kwenda chatto kabla ya Maguful.
 
Chato sio ya kwanza ndio maana nakuambia Wewe ni mjinga

Unajua saadani ilivyoanza?
Jibu swali

Inawezekana mimi ni mjinga sawa, na sio kosa kisheria.
Wewe ni mjanja vyema,

Swali langu nimekuuliza kabla ya magufuli twiga walibebwa na magari kupelekwa chatto?
 
Back
Top Bottom