๐—ก๐—ถ๐—ป๐—ถ ๐—ธ๐—ถ๐—ป๐—ฎ๐˜๐—ผ๐—ธ๐—ฒ๐—ฎ ๐—ถ๐—ธ๐—ถ๐˜„๐—ฎ ๐—บ๐˜๐˜‚ ๐—ฎ๐˜๐—ฎ๐—ธ๐˜‚๐—ณ๐—ฎ ๐—ฎ๐—ธ๐—ถ๐˜„๐—ฎ ๐—ฎ๐—ป๐—ด๐—ฎ๐—ป๐—ถ?

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Apr 28, 2020
445
754
Umeshawahi kujiuliza nini kitatokea ikiwa mtu atakufa au kikundi cha watu watakufa wakiwa angani labda wako mwezini, mars nk?

Ikiwa imebaki mwaka mmoja shirika la Anga za juu nchini marekani NASA kutaka kutuma wanaanga kwenda mwezini mwaka 2025 pamoja na safari ya mars miaka kumi ijayo.

Ndani ya kipindi Cha miaka 60 takribani watu ishirini wamefariki dunia katika matukio ya kutaka kusafiri Kwenda angani.

Kutuma watu kwenda angani ni kazi ngumu na hatari sana kwani mwaka 1989 mpaka 2003 jumla ya watu 14 walifariki katika safari za Anga za juu kupitia NASA.

Mwaka 1967 watu 3 walifariki katika tukio la kupaa kwa chombo Cha Apollo 1 na mwaka 1971 Wana Anga wengine 3 walifariki katika safari ya Suez 11.

Usafiri wa Anga unataka kuonekana usafiri wa kawaida kama ulivyo usafiri wa pikipiki au gari japo usafiri wa Anga ni mgumu hatari na wa gharama kubwa.

Je nini kitatokea ikiwa Wana Anga watafariki wakiwa angani labda Wana kwenda au kurudi ??
Profesa Emmanuel urguieta anasema ikiwa mwana Anga atafariki angani au chini katika mzunguko wa dunia basi mwili wake utaweza kurudishwa duniani kupitia kifaa kimoja chenye muundo wa kidonge ndani ya saa chache toka kufa kwake.

Ikiwa mtu atakufa akiwq mwezini itachukua muda wa siku chache mwili mwili wake kurudishwa duniani na ikitokea mtu amekufa wakati Wana Anga wanafika Kwenye Mars.

Itachukua zaidi ya miaka mwili kurudishwa Kwenye huu ulimwengu wa Dunia .

mwezini%20%E2%80%93%202-1.jpg


Wana anga wataendelea kufanya kazi iliyowaleta na kuweka mwili Kwenye begi maalum wakimaliza watarudi nao duniani kuuzika.

Kwani haitawezekana kuzika mwili Kwenye sayari ya Mars bakteria na viumbe vingine kutoka ndani ya mwili vinaweza kuuchafua uso wa Mars.
 
Back
Top Bottom