Nini kinafanya Sekta ya Ngozi nchini ishindwe kukua kulinganisha na nyingine?

its official B

New Member
Sep 16, 2021
2
6
Je, Wewe unafahamu Nini kuhusu sekta ya NGOZI nchini hapa Tanzania? Na nichangamoto gani zinaifanya ishidwe kukua hapa nchini?

Ukilinganisha na nchi zingine kama Ethiopia n.k?
 
Shida kubwa ni jinsi ya kuiandaa ngozi jinsi ya kuikata ngozi na ubora wa ngozi hasa kwenye ile sehemu ya kuweka alama kwenye mnyama huwa inapoteza ubora wa Ngozi, kunakipindi Serekali ilikuwa inapitisha matangazo kwaajili ya kuwaelimisha wafugaji jinsi ya kuweka chapa kwenye mifugo ili isiharibu ubora wa Ngozi.
 
Tatizo letu kubwa ni UBORA wangozi kwa maana ya kuiandaa ngozi toka mnyama anapozaliwa hadi anapochunwa ngozi na namna ya kuhifadhi ngozi hiyo

Wasukuma ambao ni wafugaji wakubwa sana na wamasai wanaharibu sana ngozi za mifugo kwa kuweka alama nyingi zinazo haribu ubora wangozi

Uchunaji nao ni shida ngozi inatobolewa tobolewa sana

Na kikubwa kabisa ni namna ya kuitumza ngozi baada ya kuwa tayari imechunwa hadi kuja kuiuza...... hapa ndio kunachangamoto kubwa

Kenya wanajitahidi sana
 
Kuna mahala kwakweli tulilogwa vibaya sana maana kwenye hii sekta Kenya wametupita kila mahala sio ngozi tu hata uuzaji wa wanyama hai na Nyama iliyo tayarishwa na kuwa na mbegu bora ktk kuzalisha .
 
Back
Top Bottom