binafsi tangu Jmosi jioni kuna hela natakiwa nizitoe ili zifanye kazi iliyokusudiwa lakini nimeshindwa na sijui lini m-pesa itarudi kama kawaida, nawaza yasije yakawa kama ya DECI,
naani hii huduma itakuwa imeathiri wengi, tiririka ilivyokuathiri,
Vodacom watuambie nini shida jaman..............
yaani hapa hata sielewi
Poleni saana mliohifadhi hela zenu mpesa. Vodacom sasa ni kama shoprite. wameuza sasa wanarudi kwao south. nyie mlie tu. imekula kwenu.
Nyie ni kina nani bana! Wenye pesa wanaweka hela benki, hiyo pesa ya mawazo tu ndiyo transaction zake zinapita MPESA, ha ha ha!
Hayo ndiyo mawazo ya mabosi wa Voda! Halafu ukichukulia kwamba wameiweka mjini serikali.
Wadau ni siku ya tatu sasa transaction ya M-Pesa ni shida! Customer care number inaita mpaka inakata haipokelewi!! Mwenye habari yeyote atujuze!
Ndugu mteja, tunashughulikia tatizo la kiufundi kwenye huduma ya M-Pesa na tunakuhakikishia pesa zako ziko salama. Tutakujulisha mara tu huduma itakaporejea.
hujapata hiyo msg?