Nini kinaendelea Saint Augistine University?

MKEHA

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
715
1,141
Kumekuwa na sintofahamu kwa chuo cha SAUT kiasi cha kuwafanya wafanyakazi kukimbia kwa sababu ya hali ngumu.

Wahadhiri waandamizi na wahadhiri wasaidizi hali zao ngumu kweli kweli mpaka wengine wanajuta kuwa sehemu ya jamii ya SAUT.

Chuo kile kweli kimefikia hatua ya kuchelewesha mishahara kwa wiki mbili mbele ya muda wa kawaida kuwalipa wafanyakazi.

Idadi ya wanafunzio nayo imeporomoka kiasi cha kushangaza. Zile vurugu za Main Compus na Malimbe hazionekani tena.

SAUT ilikuwa taasisi imara kweli na ilijizolea sifa kemi kemi kwenye suala zima la kuandaa wataalam hususani wa fani ya media.

Ilikuwa ni vigumu sana kwenye fani kama za MASS COMMUNICATION kumkosa mhitimu wa SAUT.Radio gani,Tv gani ma Gazeti gani lilikosa mwandishi na watangazaji waliosoma Saut.

Nasikia eti kodi zimewafanya wawe na hali mbaya hiyo sijui wakati wa akina Dr Kitime kodi zilikiwa hazilipwi.

Napenda sana SAUT iendelea kupasua mawimbi angani kama zamani. Kilikuwa chuo ambacho kila mmoja angependa kusoma pale.Sijui na TCU nao wanahusika maana siku hizi ngazi zote za juu za management lazima mtu awe ni Profesa ndo aweze kuwa VC na DVC. Sijui kama hilo lina athali kwa kuporomoka kwa SAUT.

Anyway ni muda wa kusubiri tuone nini kitatokea in future.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo mtoa post unanyumba za kupangisha wanachuo. Ndio maana unalalamika. Chuo kipo vizuri, tatizo nyinyi wenye nyumba za kupangisha wanafunzi zimedolola. Chuo now kina nyumba zake, zenu fugieni kuku
 
Vyuo vikuu binafsi karibia vyote hali yao ya kifedha ni mbaya sana. Ni kama vile zama hizi kuendesha taasisi binafsi ni ushetani!!

Vingi ya hivyo vyuo vilikopa hela ili kujenga miundombinu na mifumo ya uendeshaji vyuo, lakini sasa wanakiona kilichomtoa Kanga manyoya!!
 
Back
Top Bottom