Nini kinaendelea Ngorongoro?

Nini kinaendelea Ngorongoro?

Ngorongoro hali sio shwari kabisa kuna mambo mbalimbali yanayoendelea huko ya uvunjifu wa haki za binadamu

Moto unaowaka Ngorongoro hakuna tofauti na DP world sema issue ya Ngorongoro hatujaipa airtime

Ni wakati sasa watanzania tupaze sauti kwa kuendelea kuandika mitandaoni hali halisi ya Ngorongoro na tusiwategemee waandishi wa habari waliokambishwa asali

Ngorongoro hali sio shwari kabisa.
Nenda kule uwatetee
 
Sawa Mimi nitakukumbusha tu wakati ukifika.
Jamaa nikikusoma between the lines nakuona unataka sana hili la DPW liishie hewani, ndio maana upo kimya sana kuhusu hilo jambo, mimi naamini haki ya watanganyika ipo tu.
 
Huko Ngorongoro ni mwendo kamata, weka ndani, peleka kusikojulikana, piga, vunja maboma ya wamasai na piga marufuku kutoa habari!
Kuna genocide ya kimya kimya inaendelea ngorongoro
 
Wakuu,

Huko Ngorongoro yanasemwasemwa mengi huko X na bahati mbaya vyombo vya habari havitoi taarifa za kinachoendelea. Mbunge wa huko inasemekana amekamatwa mpaka sasa haijulikani alipo na bahati mbaya kila mtu, kila chombo cha habari na taasisi zingine ikiwemo Bunge na wabunge wenyewe wako kimya.

Haya mambo yatolewe ufafanuzi nini kinaendelea, kwanini mwakilishi wa wananchi hajulikani alipo mpaka sasa. Vyombo vya habari na wana habari wanakiri kila kukicha kuwa wapo huru lakini tunaona jinsi habari zingine wanavyoziepuka!

Tunasubiri tena waraka wa TEC tuone wanachanganya dini na siasa? Nini kinaendelea Ngorongoro?

Acha kupotosha umma, unao ushahidi wa hili? Nani akuamini na maelezo yako!
 
Back
Top Bottom