MTAZAMO
Platinum Member
- Feb 8, 2011
- 19,990
- 34,838
Wakuu,
Huko Ngorongoro yanasemwasemwa mengi huko X na bahati mbaya vyombo vya habari havitoi taarifa za kinachoendelea. Mbunge wa huko inasemekana amekamatwa mpaka sasa haijulikani alipo na bahati mbaya kila mtu, kila chombo cha habari na taasisi zingine ikiwemo Bunge na wabunge wenyewe wako kimya.
Haya mambo yatolewe ufafanuzi nini kinaendelea, kwanini mwakilishi wa wananchi hajulikani alipo mpaka sasa. Vyombo vya habari na wana habari wanakiri kila kukicha kuwa wapo huru lakini tunaona jinsi habari zingine wanavyoziepuka!
Tunasubiri tena waraka wa TEC tuone wanachanganya dini na siasa? Nini kinaendelea Ngorongoro?