Nini Kinachoendelea IMF na World Bank?


..una HOJA nzuri sana.

..kwa mtizamo wangu serekali walitakiwa waruhusu imf watoe ripoti yao halafu wai-challenge.

..katika DUNIA YA LEO hiki walichofanya serekali kinaleta picha mbaya kuliko kuruhusu imf kuchapisha findings zao.

..jambo lingine ambalo serekali wangeweza kufanya ni kuruhusu wb na undp watoe taarifa kuhusu uchumi wa Tz. In my opinion hilo lingefanyika tungeweza kuwa na picha pana zaidi na ya kuaminika kuhusu hali ya uchumi wetu.
 
Kwa hiyo mtaifanyaje IMF? kumbe hujui IMF ndo US? sasa tutawaona mwisho wenu unadhani IMF ni kama Mbowe?
Taratibu mnavutwa ili mjae kwenye 18 zao kisha wawanyonge kabisa
 
IMF na World Bank ni mapacha wa baba mmoja na huwezi wapomda IMF kuwa ni mabeberu huku ukilala kitanda kimoja na world Bank. Hizo taarifa za takwimu ni muhimu sana kwa ajili ya wawekezaji wa baadae pia na wakopeshaji.

Wakopeshaji watatumia hizo taarifa kwenye kuset riba ya mikopo ambayo Serikali inakopa ,taarifa za ukuaji wa uchumi zikiwa nzuri basi hata riba ya mikopo mipya inakua ndogo.

Pia kuna credit rating agencies kubwa tatu ambazo ni Standard and Poor (S&P), Moody's pamoja na Fitch group ambao wao wanatoa rating ya nchi kiuchumi. Mara ya mwisho (1/4/2019) Moody's wameipa Tanzania credit score ya -B1 kutokana na muonekano hasi wa ukuaji wa uchumi.

Serikali imelia sana kwamba kabla ya kupewa hiyo score na Moody's ilifaa wakae chini wazungumze nk,lakini jamaa wanatumia data sio vikao kwenye kufanya maamuzi yao. Tatizo lililopo sio mabeberu Ila changamoto za ukuaji wa uchumi ambazo zimesababishwa na uongozi dhaifu. Rating ya -B1 Tanzania haijawahi pata toka kipindi cha Nyerere kwa hiyo lazima tuna shida sehemu na tunatakiwa tujirekebishe.
 
Hv Huo ubavu wa Hv huo ubavu wa kujitoa wanaupata WAP?hyo bajet ya nchi mpaka mbuzi dume achangie ndo mambo yanakwenda

..imf wanakuja kutukagua kwasababu sisi ni wanachama wao.

..sasa inavyoelekea hatupendi kukaguliwa ndiyo maana nikasema suluhisho ni kujitoa.

..kuhusu masuala ya misaada ya kibajeti au mikopo tunatakiwa tutafute mbinu mpya maana wafadhili[ EU] na washirika [ WB, IMF]tulionao sasa hivi hawaendani na kasi ya Raisi Magufuli.
 
Mkitaka wasiwaguse hao jamaa wa WB na IMF mjitegemee kama wachina.
 
Wewe una akili sana kuliko wachumi wote wanaosema hali itazidi kuwa mbaya?Nani aliwatuma kupunguza mzunguko wa pesa na kuua biashara pamoja na kuwaona matajiri kama maadui?Saddists wakubwa nyie!
Sijawapinga hao wanaosema hali itazidi kuwa mbaya na pia sipo na wale waliosababisha hali hiyo.
Kushuka kwa kasi ya ukuaji uchumi kunarekebishika na itakuwa ajabu kama hatua hazichukuliwi kuboresha.
 
Thanks for the compliment

Pili unachosema ndio exactly watu wanavyofanya wacha watoe ripoti pinga kwa hoja, nchi za wenzetu ingawa awapingani na IMF maana awakopi huko sana. Hila si ajabu kupinga credit rating za nchi zao zinaposhushwa na watu kama akina Moody's et al kwenye international bond market.

Anyway mpaka sasa serikari ipo kimya lazima kuna sehemu wameshikwa pabaya.
 

..wanatuhumiwa kuchapisha trillions of shillings na kuzitumbukiza kwenye circulation.

..i agree with you. Waachwe ripoti itolewe. Wao wai-challenge, na wakati huohuo waifanyie kazi na kurekebisha kasoro.

..Dr.Mpango, Dr.Kijaji, Dr.Luoga, na Dr.Abbasi, huu ndiyo wakati wa kuitetea serekali. They need to tell us what happened tumepata ripoti isiyoridhisha.Vinginevyo usomi wao utatiliwa mashaka.
 
IMF hawajasema kuwa shughuli za kiuchumi Tanzania zimesimama. Maisha yanaendelea Ila tu kasi ya kukua kwa uchumi imepungua.
Uchumi kudorora ni jambo linaloweza kutokea na kurekebishwa.
Hii kwangu haihitaji elimu ya juu kwa maana tumeshudia biashara kubwa zikifungwa kama migodi na kudorola kwa zao la korosho halafu takwimu zioneshe uchumi unapaa hii itakuwa ajabu ya dunia
 
Miaka ya nyuma niliwai soma kitabu cha Mwaharakati wa Guyana ambaye hata miaka ya 70 aliwai fundisha chuo Kikuu cha Dsm. Kwenye kitabu hicho cha How Europe under developed Africa kwa tafsiri yangu ni:Jinsi Ulaya inavyoifukarisha Africa..


Ukisoma kitabu hicho utagundua mambo mengi sana kuhusu hawa jamaa Imf na world bank jinsi wanavyokuja na sera mbovu za kuendesha uchumi kwenye za Africa.

Na wakikuta Nchi ina msimamo kama tunavyoona hapa sasa Tanzania lazima wanakuja na mizengwe mingi ilmradi tu wao ndo wawe wanashauri wa sera zote za kuendesha uchumi wako.


Ifike mahala Watanzania tuache kushadadia vitu vya hovyo na kuacha mshikamamo na Utaifa wetu hasa kwenye mambo ya msingi kama haya.


Mh Rais Magufuli tunaomba endelea na msimamo wako katika kuendesha uchumi wa Taifa letu sio kupelekeshwa na hawa mabeberu ambao kimsingi huwa hawatutakii mema.

Alex Fredrick
Dar es salaam
 
Mnaficha taarifa za wizi wa hela zetu kwa faida ya nani ?
 
Miaka ya nyuma niliwai soma kitabu cha Mwaharakati wa Guyana ambaye hata miaka ya 70 aliwai fundisha chuo Kikuu cha Dsm. Kwenye kitabu hicho cha How Europe under developed Africa kwa tafsiri yangu ni:Jinsi Ulaya inavyoifukarisha Africa..

Ukisoma kitabu hicho utagundua mambo mengi sana kuhusu hawa jamaa Imf na world bank jinsi wanavyokuja na sera mbovu za kuendesha uchumi kwenye za Africa.

Na wakikuta Nchi ina msimamo kama tunavyoona hapa sasa Tanzania lazima wanakuja na mizengwe mingi ilmradi tu wao ndo wawe wanashauri wa sera zote za kuendesha uchumi wako.

Ifike mahala Watanzania tuache kushadadia vitu vya hovyo na kuacha mshikamamo na Utaifa wetu hasa kwenye mambo ya msingi kama haya.

Mh Rais Magufuli tunaomba endelea na msimamo wako katika kuendesha uchumi wa Taifa letu sio kupelekeshwa na hawa mabeberu ambao kimsingi huwa hawatutakii mema.

Alex Fredrick
Dar es salaam
 
Kwanini mnaogopa kuambiwa ukweli? Mmeiba?
 
Tumesikia ,zito akitaka kutoa ufafanuzi swala LA uchumi nchini.

Kama upo ukweli kuwa Uchumi umeshuka basi watoe ufafanuzi swa la kusubiri Zito ,asema,najua mtimanyongo wataanza kumusakama

Tutamudikia Spika akisema aitwe kwenye kamati ,Mara akamatetwe uuu!

Kwanini Taifa lina jaa uoga tena usio na sababu?

Tuwataka Waziri MpAngo ,atoe takwimu za ukweli za uchumi
Zito was unit I watoe takwimu,wakishindwa toa kwa faida ya Taifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…