Nini kimewapata Watanzania?

mogulnoise

JF-Expert Member
Oct 28, 2014
2,434
5,535
Nimefanya utafiti mdogo kwenye mitandao miwili ya Kijamii wa kwanza ni JF na wa pili ni Instagram.

Nilichokiona ni post nyingi karibu ya asilimia 85% ya post zote zinalaumu aidha direct au in derect Rais Magufuli.

Kweli hali hii imenishangaza huyu Rais ambaye alipoanza post nyingi zilikuwa za kamsifia na kuwa na matumaini makubwa juu yake leo hii wanamshambulia kama mbwa mwizi au mgoni kwenye nyumba ya mjane.

Napata shida kuelewa haya mashambulizi ni kutokana na utendaji wake au hali ya kiuchumi kwa wa TZ.

Hata ndugu yangu Salary slip naye amechoka ni hatari jamani.

Embu wadau wekeni maoni hapa kipi kilichowakuta wa Tanzania hadi wamefika hapa.

Cc Mshana Jr, swiseme etc
 
Katika hizo post wanazomlaumu hawakuandika kilichowapata?
 
Wana ya moyoni yanayowaumiza. Haiwezekani kundi lote hilo la watu kila mtu analaumu tu. Lazima kuna kitu hakipo vizuri.
 
Wacha tusome namba sote mpaka hapo rutakapofika mahali pa kupata akili ya kuchagua mtu kwa manufaa ya taifa na sii manufaa ya chama.
Chama chenyewe nao wameelemewa na zigo lao wenyewe wanakufa na tai shingoni
 
Kuwa makini na any new project unayotaka kufanya..its either uta end up in ruins au kupoteza kila kitu kama una project zako za zamani dnt make any current big moves unless una 2 or 3 back up plans ur very sure of.


Mtazamo Tu na Mtanishukuru Baadae.
 
Nimefanya utafiti mdogo kwenye mitandao miwili ya Kijamii wa kwanza ni JF na wa pili ni Instagram

Nilichokiona ni Post nyingi Karibu ya asilimia 85% ya post zote zinalaumu aidha direct au in derect Rais JPM

Kweli hali hii imenishangaza huyu Rais ambaye alipoanza Post nyingi zilikuwa za kamsifia na kuwa na matumaini makubwa juu yake leo hii wanamshambulia kama mbwa mwizi au mgoni kwenye nyumba ya mjane

Napata shida kuelewa haya mashambulizi ni kutokana na utendaji wake au hali ya kiuchumi kwa wa TZ

Hata ndugu yangu Salary slip naye amechoka ni hatari jamani

Embu wadau wekeni maoni hapa kipi kilichowakuta wa Tanzania hadi wamefika hapa

Cc Mshana Jr, swiseme etc
Rabish.... kajifunze kuandika kwanza.
 
Wanaofanya kazi hawalaumu..
Wanaoishi kwa mapato halali hawalaumu...
Waliozoea kuishi kwa kupiga dili haramu ndio wanaolalamika fanyeni kazi Watanzania wenzangu upepo umebadilika huu
 
Nimefanya utafiti mdogo kwenye mitandao miwili ya Kijamii wa kwanza ni JF na wa pili ni Instagram

Nilichokiona ni Post nyingi Karibu ya asilimia 85% ya post zote zinalaumu aidha direct au in derect Rais JPM

Kweli hali hii imenishangaza huyu Rais ambaye alipoanza Post nyingi zilikuwa za kamsifia na kuwa na matumaini makubwa juu yake leo hii wanamshambulia kama mbwa mwizi au mgoni kwenye nyumba ya mjane

Napata shida kuelewa haya mashambulizi ni kutokana na utendaji wake au hali ya kiuchumi kwa wa TZ

Hata ndugu yangu Salary slip naye amechoka ni hatari jamani

Embu wadau wekeni maoni hapa kipi kilichowakuta wa Tanzania hadi wamefika hapa

Cc Mshana Jr, swiseme etc
HIVI SALARY SLIP ALIKUWA MLANGO HUO?
 
Nilichogundua kwenye nchi yangu ni kuwa watz kwa namna yoyote ile hawakosi lawama..Kipindi cha kikwete watu walilalamika sana kuwa rais dhaifu, kipindi hiki tena wanalalamika rais mkali au amekaza sana mpaka hali imekuwa ngumu..Swali la kujiuliza je, kama mtu binafsi umechukua hatua gani kujiongezea kipato kama hali ya mfukoni ni mbaya?Au unasubiri raisi au serikali ikuletee hela?

Je kulalamika kunakusaidiaje kuongeza kipato chako mfukoni?
Je, kodi tunazohimizwa kulipa ni makosa kwa serikali kukusanya mapato kwa wanachi wake?
Je kufungwa kwa mahoteli ina maana hakuna mbadala wa masoko ya wateja zaidi ya watumishi au warsha za serikali pekee?

Ukiangalia maswali hayo yote juu ni kuwa watu wengi wamebwetekea, yaani unafikiria muda wote serikali ndio sehemu ya kuwaingizia kipato na hapo unapata conclusion kuwa kumbe kuna vimchezo vichafu vilikuwa vinafanyika serikalini..Kwa mfanya biashara mwenye tactics na mbinu za kibiashara si rahiisi kulalamika kwa sasa..Wengi wa wafanyabishara wamefeli kwa kuangalia soko la huduma au biashara zao ni serikali pekee..Yaani pesa ilikuwa nje nje kwa vitu visivyo na tija kwa taifa!

Mwisho kama mambo yamekuwa tight kwa nini tusitafute shughuli mbadala za kutuingizia vipato kuliko kulalamika?.Watz tuna kazi kubwa sana ya kubadili fikra, bure ilitugharimu na kuona serikali itufanyie kila kitu mpaka pesa zote za biashara zitoke serikalini ili mzunguko uwe mkubwa..Fikra hizo ndizo zinatufanya kila siku kulaumu serkali ya Magu, ambapo kimtazamo naona ni udhaifu wa watz tulio wengi..Kama mambo yamekuwa magumu, kamata jembe ukalime!
 
Back
Top Bottom