Nini kimetokea gesi ya Mtwara hadi kuanza upya na Stiegler`s Gorge?

mkuuwakaya

JF-Expert Member
Mar 18, 2013
923
1,272
Tumeaminishwa na kuimbiwa nyimbo na mapambio miaka yote kuwa gesi ya Mtwara ndiyo suluhisho. Nakumbuka kuna watu walipoteza maisha na jeshi letu liliweka kambi kule.

Kwa anayejua ni kitu gani kimetokea hadi tunaenda kugombania maji na wanyama wa Selous game reserve na wakati kwa miaka kadhaa tumeimba wimbo mzuri wa gesi ya Mtwara?. Waandishi wa habari mtusaidie kujua hili.

Fedha nyingi sana za wavuja jasho zimetumika kwenye mradi wa gesi. Bomba zimetandazwa tokea Mtwara hadi Dar halafu leo hii anatokea mtu mmoja tu as if hajui kama kuna mradi wa gesi.Ningependa kumsikia Magu akijenga hoja na kushawishi kwanini Stieler's Gorge na sio gas ya Mtwara ambayo JK alishaanza.

Mimi bado sielewi, kwamba gesi haitatoa umeme wa kutosha au kuna kingine ambacho hatukijui? Anayejua atiririke hapa. Afadhali fedha za huo mradi wa Stiegler`s Gorge ziende Mchuchuma na Liganga ambako umeme utakuwa wa uhakika mara dufu.
 
1: Mtwara ni kama kuna element za upinzani, japo mbunge wa sasa ni kama si mpinzani tena lakini bado kuna wasi wasi kuwa upinzani thabiti unaweza kutwaa hilo jimbo 2020 ikiwa polisi watajisahau. Rejea bunge la mwaka jana kuwa maendeleo hayatapelekwa kwenye majimbo ya upinzani.

2: mradi wa gesi inaonekana kazi kubwa imeishafanyika, kipande kilichobaki kinahitaji pesa kidogo tu. Hivyo kwa akili ya kawaida ni bora kuanzisha mradi mpya utakaogharimu pesa nyingi ili wajanja wapige mpunga wa kutosha. Mfano ww ukiambiwa pesa ipo, chagua mradi unaotaka kusimamia kati ya ule wa 900B au 10B utachagua mradi upi? Definitely you will opt for the most expensive one with the hope of making the best possible manoeuvre.
 
Ningependa kukuelewesha kuwa gesi siyo ya Tanzania ila Tanzania ina hisa kwenye gesi hiyo,mwenye gesi asilimia kubwa ni mwekezaji hivyo gesi itauzwa kwa tanesco kwa bei ya soko,umeme wa maji una gharama nafuu sana na itakuwa mali ya Tanzania kwa asilimia 100,hicho ndicho kinachofanya stiglers gorge ijengwe,
 
Kwani mikataba ya gas imesha pitiwa upya? Maana huenda ni kama ile ya makinikia.

Sina hakika kama bomba la gas lilishazinduliwa. Na kama halijazinduliwa jua tu shughuli ni kubwa maana hatakulisogelea kulizindua watu wanaogopa kunuka harufu ya gas ingwa ya sasa tunambiwa hailipuki kama ile ya zamani.
 
Ningependa kukuelewesha kuwa gesi siyo ya Tanzania ila Tanzania ina hisa kwenye gesi hiyo,mwenye gesi asilimia kubwa ni mwekezaji hivyo gesi itauzwa kwa tanesco kwa bei ya soko,umeme wa maji una gharama nafuu sana na itakuwa mali ya Tanzania kwa asilimia 100,hicho ndicho kinachofanya stiglers gorge ijengwe,
Hizo siasa tu,wakati ule wanaipitisha mikataba bungeni hadi wapinzani wakatoka nje hayo hawakuyaona? Wakati wanatuaminisha kuwa gesi ndio mkombozi wa tatizo la umeme tz, na umeme utashuka sana bei hayo hawakuyajua kwani?kipindi kile wanatuambia kuwa umeme wa maji umeshapitwa na wakati kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi si ndio hao hao wanao upigia kelele kuwa huo mradi mpya ndio suluhisho la umeme tanzania?tumeshawachoka kwa siasa zenu!
 
1: Mtwara ni kama kuna element za upinzani, japo mbunge wa sasa ni kama si mpinzani tena lakini bado kuna wasi wasi kuwa upinzani thabiti unaweza kutwaa hilo jimbo 2020 ikiwa polisi watajisahau. Rejea bunge la mwaka jana kuwa maendeleo hayatapelekwa kwenye majimbo ya upinzani.

2: mradi wa gesi inaonekana kazi kubwa imeishafanyika, kipande kilichobaki kinahitaji pesa kidogo tu. Hivyo kwa akili ya kawaida ni bora kuanzisha mradi mpya utakaogharimu pesa nyingi ili wajanja wapige mpunga wa kutosha. Mfano ww ukiambiwa pesa ipo, chagua mradi unaotaka kusimamia kati ya ule wa 900B au 10B utachagua mradi upi? Definitely you will opt for the most expensive one with the hope of making the best possible manoeuvre.
Tuache hilo la namba moja, kwa sababu ni blah blah.

Elezea hapo kwenye bold. Kwa kutumia maneno na numbers.

Pesa kidogo zilizobaki ni kama kiasi gani? Na muda kiasi gani mpaka completion? Na gesi itaisha lini? Au ni renewable?
 
Ningependa kukuelewesha kuwa gesi siyo ya Tanzania ila Tanzania ina hisa kwenye gesi hiyo,mwenye gesi asilimia kubwa ni mwekezaji hivyo gesi itauzwa kwa tanesco kwa bei ya soko,umeme wa maji una gharama nafuu sana na itakuwa mali ya Tanzania kwa asilimia 100,hicho ndicho kinachofanya stiglers gorge ijengwe,

Ina maana haya yote serikali hawayajua ndio wanafahamu leo?
 
Wakati wa Kikwete tuliaminishwa kwamba ujio wa gesi ya Mtwara utaondoa kabisa tatizo la umeme wa maji (kidatu, mrera, Hale, Nyumba ya Mungu n.k.)

Cha kushangaza awamu hii ya Magufuli tunaambiwa kuna mradi wa matrilioni wa umeme wa Stiegler's Gorge ambao ni wa maji, kama ilivyo kidatu, mrera, Hale, Nyumba ya Mungu n.k.

Sasa hapa tunaenda mbele au kurudi nyuma?

Kwa nini Stiegler's Gorge na Sio Gesi ya Mtwara?
 
Back
Top Bottom