Nini kimesikika toka watawala wa Afrika tukio la uchaguzi Kenya

TGInnocent

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
1,088
576
Habari za Jumamosi great thinkers

Tukio la mahakama kuu ya Kenya kutengua matokeo ya uchaguzi wa raisi wa Kenya linazungumzwa kama tukio la kihistoria katika demokrasia za siasa za Afrika.

Mimi binafsi sijasikia hotuba au tamko rasmi toka viongozi/watawala wetu na hususani toka katika bara letu. Kama miongoni mwetu amesikia lolote kutoka kwao tunaomba utufahamishe ili tushiriki kupata mtazamo wa hawa wakuu wetu. Kama kweli hawajatoa tamko lolote, toa maoni yako unafikiri kwa nini wameduwazwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmmaa nasikia mke wake ananyatia nyatia
shida ndio ipo hapo/ Kule Uganda tegemea hayohayo na Kule kwa Rafiki yetu mpendwa Mwenye shingo ndefu wala usizungumzie kabisa! Niliona siku ile anaapishwa ana mitoto ya kiume kama mitatu hivi limoja wapo linaandaliwa kuja kukaa pahala pa baba Yake atakapo kuwa amenyakuliwa kwenda kuungana na wazee wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama mwenyewe Kenyatta amesema hakubaliani na maamuzi ya majaji juu ya hukumu hiyo lakini anaheshimu maamuzi yao wewe ulitakaje sasa soma nyuso kwanza anza na Zimbabwe ndio utajua
Katika hali kama hii naamini wana uwanja mpana wa kusema jambo, au kwa kumpa pole na kumtia moyo Uhuru endapo wanaungana na kauli yake au kupongeza demokrasia iliyoonekana miongoni mwa wakenya. Zaidi sana hali ya utulivu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waache wazee wakae kimya mkuu, sentensi zao zina impacts sana barani Afrika wacha watulie mkuu wangu usipende waongeee sana kuhusu hili
 
Lisu, mwana sheria mkuu wa CDM kafurahishwa ila bado mwenye chama EL na Mh. Mbowe hawaja toa tamko.
 
Katika hali kama hii naamini wana uwanja mpana wa kusema jambo, au kwa kumpa pole na kumtia moyo Uhuru endapo wanaungana na kauli yake au kupongeza demokrasia iliyoonekana miongoni mwa wakenya. Zaidi sana hali ya utulivu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hawawez kupongeza maana watakua wanajitekenya na kucheka wenyewe.

Huwezi kumpongeza mtu kwa demokrasia safi wakati kwako demokrasia unaibaka bila kutumia hata kinga
 
Baada ya lile tukio la kumshuhudia Kikwete akiachia madaraka akiwa bado anaonekana kama kijana wa 30yrs,hili la Uhuru ni tukio la pili kuwashangaza akina Mugabe na Kaguta!
 
Back
Top Bottom