Mtu aliyeponea Rehab baada ya kuwa na uraibu wa dawa za kulevya ni wa kumwamini?Hivi karibuni, Fatma Karume ameonekana kubadili mwelekeo wa mijadala yake ya kisiasa kwa namna ambayo imeibua maswali miongoni mwa watanzania, hasa wale wanaoamini katika harakati za mageuzi ya kweli. Mwanzo, alivamia vikali kauli za Askofu Gwajima aliyekuwa anapinga matukio ya utekaji na ukiukwaji wa haki unaodaiwa kufanywa na vyombo vya dola, akimtuhumu kuwa anatafuta "attention" ya kisiasa, licha ya kwamba hoja za Gwajima zilikuwa na uzito wa kulinda utu na uhuru wa raia.
Sasa, ameibukia tena kwenye mtandao wa X (zamani Twitter), akizibeza juhudi za CHADEMA na sera yao ya "No Reforms, No Elections", akikariri kuwa kusitisha uchaguzi ni kosa la jinai. Kauli hii imechukuliwa na wengi kama kejeli isiyoakisi hali halisi ya mazingira ya kisiasa nchini, ambapo haki za msingi, uhuru wa kisiasa na uhuru wa kutoa maoni vinaendelea kukandamizwa.
Cha kushangaza zaidi, kauli hizi za Fatma Karume zinatolewa wakati ambapo Tundu Lissu, mmoja wa viongozi wa upinzani na mwanasheria mwenzake, yuko rumande akikabiliwa na mashtaka ya uhaini, ambayo kisheria adhabu yake ni kunyongwa hadi kufa. Hali hii imezidi kuzua maswali: je, Fatma Karume bado yupo upande wa watetezi wa haki, au amebadili msimamo kwa sababu ambazo bado hazijafahamika wazi?
Ikumbukwe kuwa katika utawala wa Hayati John Magufuli, Fatma Karume alijitokeza kuwa mmoja wa sauti thabiti zilizokuwa zikikemea dhuluma, ukandamizaji, na matumizi mabaya ya madaraka. Lakini katika utawala wa sasa, ambao nao umeonesha mwelekeo wa kukiuka misingi ya demokrasia, sauti yake imekuwa ya mashaka, wakati mwingine ikisikika kama ya kukubaliabiana na mfumo badala ya kuukosoa.
Je, ni mabadiliko ya kiitikadi? Ni mkakati wa kisiasa? Au kuna mambo ya ndani zaidi ambayo bado hayajawekwa wazi kwa umma? Kwa vyovyote vile, hatua na kauli za Fatma Karume zinahitaji tafakari, hasa kwa wale wanaoamini katika dhana ya "principled activism" yaani, kupigania haki bila kujali nani yuko madarakani.
Alikua mgonjwa kumbeMtu aliyeponea Rehab baada ya kuwa na uraibu wa dawa za kulevya ni wa kumwamini?
Yule ni mpuuzi kama wapuuzi wengine tu. Wanaomsikiliza nao wana shida ya akili.
Nakuamini Lord, sikupingi jamboMtu aliyeponea Rehab baada ya kuwa na uraibu wa dawa za kulevya ni wa kumwamini?
Yule ni mpuuzi kama wapuuzi wengine tu. Wanaomsikiliza nao wana shida ya akili.
Mtatukana kila mtu,the end is hereMtu aliyeponea Rehab baada ya kuwa na uraibu wa dawa za kulevya ni wa kumwamini?
Yule ni mpuuzi kama wapuuzi wengine tu. Wanaomsikiliza nao wana shida ya akili.
Alikuwa teja yule wakati anaishi UK. Baba yake alifunga safari kuhakikisha anapata matibabu ya Rehab ndo akapona.Alikua mgonjwa kumbe
Duh! Atashika jani au shela!? Lakini huyu si anatokea katika ukoo wa kifalme?Dini,asili kwa kuzaliwa na jinsi yake lazima wawe bega kwa bega kudemka na "mbarikiwa kutoka kwa Mwamposa"!
NB:Uzee upo puani na haoni mbele atashika jani au shela.
Lakini mbona inaonekana kama yeye mwenyewe ndiye anayetoa taswira ya udini kwa namna alivyojenga hoja zake dhidi ya shutuma alizozitoa Gwajima? Badala ya kujibu kwa msingi wa hoja au ushahidi wa kimantiki, hoja zake zinaonekana kujengwa juu ya misimamo inayogusa hisia za kidini.Kuna post aliwashutumu chadema kwa udini,kashtuka,kaujua muundo wa wadini,kajiweka kando, kupitia mitandao fitna inageuka,wadini na walioweka misingi hiyo hawatofika kokote
Kumbe ni teja.!?Mtu aliyeponea Rehab baada ya kuwa na uraibu wa dawa za kulevya ni wa kumwamini?
Yule ni mpuuzi kama wapuuzi wengine tu. Wanaomsikiliza nao wana shida ya akili.
Ni kama watoto wa princess Diana tu. Ufalme wameudhibiti mikononi mwao? Wana uhakika wa kesho yao? Yule kamuoa Katherine, akatengwa kiaina. Huyu akakosoa serikali na kuegemea upande wa ukimzani, akachukiwa. Wote wameanza kurudi na kukumbuka kudeka kwenye miguu ya "baba" zao. Nadhani tupo wote!Duh! Atashika jani au shela!? Lakini huyu si anatokea katika ukoo wa kifalme?
Kazi kweli kweli… mtaani kwa motoNi kama watoto wa princess Diana tu.Ufalme wameudhibiti mikononi mwao?Wana uhakika wa kesho yao?Yule kamuoa Katherine,akatengwa kiaina.Huyu akakosoa serikali na kuegemea upande wa ukimzani,akachukiwa.Wote wameanza kurudi na kukumbuka kudeka kwenye miguu ya "baba" zao.Nadhani tupo wote!
And,there could have come a fool and say...,the islanders are not much of segregatives and fundamentalists"...?Charity begins at home
Wakati huo Watanganyika wamelala usingizi wa pono, hawashtuki, hawahoji, hawashtuki kwa uhalisia wa yanayotendeka mbele ya macho yaoCharity begins at home