Nini kimeikumba chama changu CHADEMA?

Nini kimeikumba chama changu CHADEMA?

Mimi sijaona viti vikibadilishwa zaidi ya 'ziara za kushtukiza' zinazofanywa na Magufuli na mawaziri wake huko Dar utadhani serikali hii ni ya Dar peke yake.Huku mikoani hakuna kilichobadilika ufisadi uko palepale na maisha yanazidi kuwa magumu kuliko hata kabla ya uchaguzi.

Kuongeza makusanyo ya kodi sio mabadiliko?

Kurudisha nidhamu kwenye kazi sio mabadiliko?

Kuwajibishwa wazembe sio mabadiliko?

Wanafunzi kupata elimu bure sio mabadiliko?
 
Wafuasi wa cdm ni dizaini ya Mmawia....what do u expect
 
Last edited by a moderator:
1. Katiba ya wananchi CCM imefanya nini?
2. Wizi wa ESCROW nini kimefanyika?
3. Vurugu zote za uchaguzi wa mameya maeneo ambayo CCM wameshindwa, nani anakemea uhuni unaofanyika? rejea Kinondoni, Ilala, Morogoro na kwingineko
4. Uchaguzi wa Zanzibar umefikia wapi? wananchi ambao ndo wenye nchi wamepewa mrejesho wowote?

Acha kuishi kitumwa na kujitoa ufahamu. Elimu huletwa na tafakuri na kudadisi, la sivyo huwezi jua nini kiko vipi na kwa nini?

Katiba mpya ni muhimu ila rais anafanyia kazi kwanza kero za wananchi wa kawaida, watu wa huko site katiba kwao sio kero kubwa kama social needs like elimu maji umeme barabara etc.. Sisi kama chama inabidi tujitahid kuaddress aya mambo bila hivyo tutakosa hoja.
 
Umekosa cha kuandika siyo???Hiv ww unaona nn kimebadirika ktk hii serikar ya makufuli.....hizo ziara anazoziita za kushitukiza wakati waandishi wa habari wanakuwa na taarifa nazo....?hakuna pilote like bado maisha ni magumu kupit? maelezo......afu we siyo mwana Chadema tuachie chama chetu site usituingilie!!!!!

Hahahahahah inamaana uoni kama magufuli amebadili utendaji maofisini ebu tuulize sisi tunapata huduma za serikali kila siku tukuambie utofauti na huko nyuma.
 
Ovu lipi ambalo kama CHADEMA, limetetea?

Watu wakisimamishwa kazi kwa ufisadi kina Saanane na Kubenea wanawatetea.

Watu wakiwajibishwa wafanye kazi watetezi wao wamekuwa chadema.

Wavamizi wa maeneo yasiyoruhusiwa wanatetewa na chadema.

Kila ovu ambalo rais anachukua hatua na mawaziri wake chadema tumekuwa ni watu wa kutetea vitu tulivyo vipigania vibadilike.

Inawezekana hii inatokea pasipo sie kujua tumejiweka wrong position ila naona kuna siku itatugharimu.
 
Kwa ufupi CDM kwa sasa hawana kazi ya kufanya,natural death,maana ili wawe active lazima CCM wafanye makosa,vinginevyo ukisema wasimamie kwenye sera yao ipi,kwa hiyo kwa sasa wamefutika na hasa baada ya tinga tinga kuanza kulima
 
Kwa mtu ambaye yupo tz na hajaona yaliyofanywa na JPM lazima awe mchawi kidogo,yaani mataifa ya nje waone wewe wa ndani usione,hata kama ni ushabiki wa vyama unakuwa umekifikisha hatua mbaya,Tanzania imebadilika mnoo
 
Mawaziri wakishtukiza kosa.

Wakitoa muda wa siku kadhaa kosa.

Rais akichukua hatua on the spot anakurupuka.

Akiunda mchakato serikali ni ile ile.

Wakiondoa wahamiaji haramu chadema tunasema tutumie busara yani tuendelee kuwaacha.

Hivi tunachotaka ni nini wananchi hawatuelewi.
 
Hata mimi siku hizi siwaelewi wenzangu.Ati wanasema yeyote anayechekelea mafisadi wakitumbuliwa kanunuliwa na ccm.!!!!
 
Tulizoea zamani Chadema ndio chama kinachofichua maovu na kupambana nayo na CCM ndio kulikuwa chama cha kutetea maovu na kufanya madudu yote yasiyofaa.

Ila leo sielewi kimetokea nini Chadema imekuwa ndio chama cha kutetea maovu na kupinga lolote zuri litalofanywa ili kuleta nidhamu kwenye nchi. Alafu ccm ndio kimekuwa chama cha kushughulikia maovu na kuyakemea kwa nguvu zote.

Sikuwai ata siku moja kuwaza itafika siku Chadema watapambana kuwatetea waovu na watu waliofanikisha ufisadi, rushwa, wizi, uvunjaji taratibu nk.

Mimi wakati tunapigania mabadiliko niliamini tunataka mabadiliko kweli. Sasa vitu vinabadilishwa tutapinga ni kama hatutaki vitu vibadilike na sielewi tunaitaji nini!

Jamani ebu mnisaidie kuelewa tatizo nini wana Chadema wenzangu?

Kuwa ccm hivi ni lazma uache likizo akili zako?
 
Usiwe na wasiwasi kuhusu CDM. Chama chochote kinachopoteza uchaguzi huwa kinachukua muda fulani kabla hakijarudi kwenye agenda yake kamili. This is true everywhere in the world, hata kwa wenzetu ambao demokrasia yao imekomaa kuliko yetu. CCM lazima ianze kwa nguvu ili kuonyesha wananchi kuwa ilikuwa chaguo zuri. Tatizo ni kuwa kuna watu kwenye chama ambao hawaelewi siasa wanaona umuhimu wa kupinga kila kitu hata vile vizuri lakini hao nao watatulia baada ya muda na CDM ita settle na kuendelea na agenda yake ya kuwatetea wananchi.
 
Mkuu hiyo agenda ya kutetea wananchi wakati wa uchaguzi ilikuwa nini unaweza kuorodhesha. Kwa kuwa ninachokumbuka ni dk 2-5 hotuba ya Lowassa akisema nichagueni na kuzungusha mikono na kusema mabadiliko.
 
Kwani hujui chama kimeuzwa kwa mafisadi wawili mapacha wa huko kaskazini
 
Mimi sijaona viti vikibadilishwa zaidi ya 'ziara za kushtukiza' zinazofanywa na Magufuli na mawaziri wake huko Dar utadhani serikali hii ni ya Dar peke yake.Huku mikoani hakuna kilichobadilika ufisadi uko palepale na maisha yanazidi kuwa magumu kuliko hata kabla ya uchaguzi.

we malata ww kama Nabii waje na huku mikoani maisha magumu saana huku kila kukicha vitu vinapanda bei kama unavyoota Uyoga kifuku hiii ni tabu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom