Siasa Yetu, Maridhiano, na Mwelekeo wa Taifa

Siasa Yetu, Maridhiano, na Mwelekeo wa Taifa

covid 19

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2014
Posts
8,295
Reaction score
20,663
Kwa viongozi wa CCM, kwao ni kheri kuendelea kuishi kwenye mazingira ya migogoro na mtifuano kuliko kukubali maridhiano ya kweli ile inayoweza kufungua milango ya katiba mpya itakayowabana, iwajibishe dola, na hatimaye kuwafanya wasiwe kwenye “comfort zone” yao waliyodumu nayo kwa miaka toka uhuru.

Na ukiangalia hali ilivyo sasa, haichukui hata sekunde kugundua kuwa viongozi wakuu wa CCM tayari wameshapanga namna ya kukabiliana na mazingira mapya ya kisiasa nchini. Hawashangazi, na hawatashangaza. Kupuuzia maridhiano ya dhati ni kama desturi yao. Maridhiano “ya kweli”—si yale ya kinafiki, si ya mezani tu—yale yenye uwezo wa kusababisha katiba safi, huru, na yenye kubadilisha mfumo mzima wa uendeshaji wa nchi. Hapo ndipo hawako tayari kabisa.

Kwao, CCM = dola, na dola = CCM. Hawataki kutenganisha chama cha siasa na taasisi za nchi kama ilivyo kwa vyama vingine kama Chadema, ACT-Wazalendo au CUF. Huu ndio mzizi wa tatizo lote.

Nini kifanyike?

Kwa CCM

Hili ni chama kilicho na nguvu na ushawishi mkubwa. Hilo halipingiki. Lakini upepo wa sasa si mzuri—na kila ishara inaonyesha kwamba kuendelea kutumia mabavu au mbinu za kulazimisha mambo kunawaingiza kwenye wakati mgumu mno.
Kama wanataka kusalia madarakani kwa muda mrefu (na inawezekana), basi njia ni moja tu:
👉 Fanya mabadiliko (reforms) ya kweli ndani ya chama.

👉 Jifunzeni kutoka kwa mfano wa ANC Afrika Kusini—chama chenye historia kama yenu lakini chenye uwezo wa kusoma upepo wa kisiasa.

👉 Tumia ushawishi wa mazungumzo na si rafu dhidi ya vyama vingine.

👉 Acheni mbinu za kudanganya umma ambazo sasa watu wanaziona waziwazi.

Kwa mazingira ya sasa, CCM inaweza kuendelea kuwa chama tawala—lakini si kwa msimamo wa kukataa mabadiliko.

Kwa Vyama vya Upinzani
Kwenye uhalisia, upinzani wenye nguvu nchini umebaki:
Chadema
ACT-Wazalendo
Na kwa mbali: CUF

CHADEMA

Hiki ni chama kikuu cha upinzani lakini ndicho kilichopigwa zaidi. Mashambulizi kwa wanachama, viongozi kutekwa, wengine kuuawa… wapo kwenye kipindi kigumu mno. na toka bwana Lissu kuwa Mwenyekiti ndipo majanga yakazidi kuwatikisa.

Kwa namna ya kipekee kabisa (au nguvu ya Mungu), TEC imekuwa kama malaika mlezi kwa Chadema kwa sasa, kwa sababu ndicho chombo pekee kilichosimama hadharani kutetea misingi ya haki waziwazi. Wakati vyombo vya dola viliposhindwa, na wengine kunyamaza kimya dhidi ya uovu waliokuwa wanatendewa hawa chadema TEC kwa sasa ndio mwanga wa pekee kwenye giza kwa chadema.

ACT-Wazalendo
Hawa ni kama chama timamu lakini chenye “mood swings”.
Kabla ya uchaguzi—waliunga mkono kila kitu cha serikali, wakakubali tume, wakakubali mazingira.
Baada ya uchaguzi—wakageuka. Wakaanza kupinga, wakaanza kuikosoa tume na uchaguzi.
Ni kama walikaa wakasikiliza upepo, wakaona upande unaowapa faida zaidi, ndio wakaamua “huku tupo”.

Mwisho wa Siku…
Tunabaki na picha hii:
CCM haitaki maridhiano ya kweli kwa kuogopa katiba huru kiufupi hawataki na hawatataka ushindani huru.
Upinzani uko kwenye mapambano magumu mno lakini bado unavuta pumzi labda watapata mwanga na matumaini mapya.
Wananchi wanahitaji mfumo wenye haki, maridhiano ya kweli, na mabadiliko ya msingi—siyo maigizo.
 
Unavyosema chama chenye ushawishi unamaanisha nini? Chama chenye ushawishi kinaogopa kufanya reforms kwenye tume na kuweka uwanja sawa? Chama chenye ushawishi kinaiba kura na kujitangazia ushindi? Tuache kuishi kwa mazoea CCM hiki chama kimeonyesha kitaondoka madarakani kwa kumwaga damu za watu au Civil War sio kwenye box la kura hakuna mwana CCM yoyote ukitoa Warioba anaetaka reforms na katiba mpya
 
Kwa CCM
Hili ni chama kilicho na nguvu na ushawishi mkubwa. Hilo halipingiki.
Sijui umetumia kipimo gani kuipata hiyo nguvu na ushawishi mkubwa walionao ccm!

Chama chenye nguvu na ushawishi mkubwa hakiwezi kuogopa uchaguzi ulio huru.
 
Unavyosema chama chenye ushawishi unamaanisha nini? Chama chenye ushawishi kinaogopa kufanya reforms kwenye tume na kuweka uwanja sawa? Chama chenye ushawishi kinaiba kura na kujitangazia ushindi? Tuache kuishi kwa mazoea CCM hiki chama kimeonyesha kitaondoka madarakani kwa kumwaga damu za watu au Civil War sio kwenye box la kura hakuna mwana CCM yoyote ukitoa Warioba anaetaka reforms na katiba mpya
ni kweli wataondoka madarakani kwa kumwaga damu hilo lipo wazi kabisa ila kwa sasa bado wana ushawishi ni wao tu wanashindwa kuchanga karata zao vyema.
 
CCM MBINGU walizo baki nazo kushinda na kuendelea kutawala

1.Kununua na kufadhili kwa pesa nyingi sana vyama vya kawaida vya upinzani kina CHAUMA,CHAUSTA,UPDP,DP etc

2.Kuteka na kuua
 
Chawa wa ccm mtahangaika sana, siku zenu za kutamba zimeisha, mlipigwa upofu wa mabavu ili liwe anguko lenu, mtaishia jela za kimataifa na za ndani, ipo siku
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom