Nini kilimkuta mwandishi wa habari wa DW, Kabendela Shinani na kupelekea kifo chake?

Babe la mji

JF-Expert Member
Dec 14, 2019
983
2,053
Nakumbuka huyu alikuwa mwandishi wa redio ya kimataifa ya Ujerumani DW idhaa ya Kiswahili na alikufaga kifo cha kutatanisha Sana. Mtu katoka kwake na gari hadi bandari ya Bukoba na akafika na kupaki gari yake akatoka kwenye gari na ikaelezwa baadae alijirusha majini na kufariki dunia.

Lakini wengine wanadai ni kutokana na ishu za matokeo ya uchaguzi kwa kuutangazia Ulimwengu kuwa mgombea wa CUF bwana Rwakatale kuwa ndio mshindi wa uchaguzi huo huku mamlaka za kutangaza matokeo zikiwa bado hazijatoa matokeo rasmi.

Wahenga wenzangu nafahamu bado mnakumbuka hili sakata naomba tujuzane nini kilimkuta huyu mwandishi.
R.I.P Kabendela.
 
Nakumbuka huyu alikuwa mwandishi wa redio ya kimataifa ya Ujerumani DW idhaa ya Kiswahili na alikufaga kifo cha kutatanisha Sana. Mtu katoka kwake na gari hadi bandari ya Bukoba na akafika na kupaki gari yake akatoka kwenye gari na ikaelezwa baadae alijirusha majini na kufariki dunia...
Uchaguzi wa awamu gani?

Kwamaana kuna watu waliibuka "hawajulikani" awamu ya 5 walikuwa wakitekeleza matukio kama hayo
 
Mimi namkumbuka Kabendera Jr aliyenyooshwa na Magu majuz juz, huyo Kabendera mwingine ndio namsikia leo
 
Nakumbuka huyu alikuwa mwandishi wa redio ya kimataifa ya Ujerumani DW idhaa ya Kiswahili na alikufaga kifo cha kutatanisha Sana. Mtu katoka kwake na gari hadi bandari ya Bukoba na akafika na kupaki gari yake akatoka kwenye gari na ikaelezwa baadae alijirusha majini na kufariki dunia...
Huyu nasikia ilikuwa ni issue ya uraia .sasa aliposhtukiwa kuwa anatoka Rwanda na anatakiwa kurudishwa kwao akaamua kujimaliza na kujitupa ziwani.
 
fundisho siku nyingine mkisikia mkurugenzi ndio mwenye mamlaka ya kutangaza matokeo muwe mnaelewa
 
Manic Depression...

Hata kabla ya kifo chake hakuwa sawa....

Took his own life...

Unataka kusema aliuwawa?
 
Huyu jamaa alikuwa mtanzania mzaliwa Kamachumu, alisoma bukoba seco na akawa mwandishi WA HABARI. Alipenda tend akiwa mtangazaji WA kiswahili radio rwanda. Nakumbuka enzi hizi alikuwa na serushago bin nestory na Ally Yusuf Mugenzi mkurugenzi WA BBC gahuza miryango. Vita ya 1994 aliikimbia Rwanda via congo na BAADAE KIGOMA. Alimobe Hadi kagera Kwani alikuwa amejenga eneo la mafumbo- kashai. Yes alikuwa mwanzilishi WA idhaa ya kirundi/kinyarwanda BBC. Lqkini kumbuka alikuwa anatangaza matukio mbalimbali ya mkoa wa kagera. Uchaguzi wa 1995 rwakatale alikuwa strong SANA Kwani HAPA alikuwa ameacha KAZI afsa utumishi mansoaa ya bukoba. Pia Sir kahama aliitaji ubunge Jimbo la karagwe KWA nguvu zote. Yes kama msema kweli alitangaza kilichojili Jimbo la bukoba mjini na karagwe. Yasemekana hata serikali ya wanyaru walianza kumtafuta kuwa alishirikiana na byalimana government. Frustration, harassment, intimidation zilimuua huyu mwamba wa HABARI
 
Nakumbuka huyu alikuwa mwandishi wa redio ya kimataifa ya Ujerumani DW idhaa ya Kiswahili na alikufaga kifo cha kutatanisha Sana. Mtu katoka kwake na gari hadi bandari ya Bukoba na akafika na kupaki gari yake akatoka kwenye gari na ikaelezwa baadae alijirusha majini na kufariki dunia.

Lakini wengine wanadai ni kutokana na ishu za matokeo ya uchaguzi kwa kuutangazia Ulimwengu kuwa mgombea wa CUF bwana Rwakatale kuwa ndio mshindi wa uchaguzi huo huku mamlaka za kutangaza matokeo zikiwa bado hazijatoa matokeo rasmi.

Wahenga wenzangu nafahamu bado mnakumbuka hili sakata naomba tujuzane nini kilimkuta huyu mwandishi.
R.I.P Kabendela.
Kabendera Shinani akiandika na kuripot BBC,wakati RPF inachukua nchi Rwanda,kabendera alielekea huko na akaukana uraia wa Tanzania.Baadaye akawa anamkosoa Mr Mwembamba kikaumana ikabidi arudi Tanzania.Mwaka 2000 akakamatwa anajiandikisha kuwa mpiga kura,kwakuwa alikuwa na mrengo wa shoto akadakwa ,akafunguliwa kesi.Yaliyotokea ziwani inaelezwa kwamba aliacha ujumbe kwenye gari ukisema"Tanzania Hawanitaki na Rwanda Hawanitaki."
 
Huyu mwamba walimuandalia kesi ya Uhaini kisa ni baada ya kutangaza ukweli, na ukizingatia alikuwa ashaukana uraia wa Tanzania na kuamia kwa mr slim
 
Back
Top Bottom