Ciprofloxacin.
JF-Expert Member
- Apr 15, 2015
- 1,583
- 2,702
Dr masako na THI sijui hebu uliza na peruzi vizuri naona umerudia masako na jina lako ni dawa utakuwa unasomea udaktari au daktari naomba udadisi jina kwanza usije pata maelezo tofauti
Dr. Ferdinand Masau ninampa heshima ya pekee. Alihusika kumtibu ndugu yangu wa karibu ugonjwa wa moyo kwa gharama nafuu kabisa na amepona hata kidonge hatumii. Hakuwa na tamaaa kabisa. Ilifika mahali akaruhusu tena kwa kutukimbiza kuwa tusiende tena check up akawa alitoa consultation za after every year. Ingekuwa walafi ungeambiwa kila mwezi rudi ili tu akukamue hela. Rest in Peace mtaalam uliyepigwa vita hata na serikali yako. Inakatisha tamaa sana. Ninaamini ingekuwa ni serikali ya Magufuli wala asingepigwa vita kwa kuwa mchango wake ulikuwa wazi.
Unamaanisha marehemu Dr Ferdinand Masau.
UFAFANUZI.
1/Nadhani unamaanisha Dr.Ferdinand Masao ambaye kwa sasa ni marehemu.
2/Fitna, Chuki, Mizengwe dhidi yake kutoka kwa Baadhi ya Watanzania wakiwemo Madaktari, Maafisa wa wizara ya Afya, viongozi kadhaa kutoka serikali ndiyo vilichangia sana Dr.Masao kufariki. Stress za maisha akipambana kutaka kufanikisha ndoto zake zilipelekea kuugua na kufariki. Alikuwa na ndoto njema sana na pana sana kwa Tanzania, hakuwahi kukata tamaa kabisa.
3/Hakuwahi kuwatendea ubaya wowote watanzania, alitumia Muda wake, Utaalamu wake, Kipaji chake na Juhudi zake binafsi katika kuanzisha Hospitali ya kutibu na upasuaji wa moyo ili huduma hiyo iwepo nchini na watu wasiendelee kupelekwa nje, Lakini alichokumbana nacho, kinatia huzuni sana. Alifanyiwa kila aina ya Fitna, alikosa watu wakumtetea, alisakamwa mpaka basi.
4/Kiukweli kabisa, Tanzania tumeitupa Lulu ya thamani sana, Dr.Masao alikuwa ni lulu tena lulu ya thamani sana. Katika hili laana iko juu ya nchi yetu. Mbegu ya Fitna tuliyoipandikiza itatutafuna mpaka basi. Kila mtaalamu atakayeibuka hapa Tanzania atapigwa vita vibaya sana. Usishangae ya Dr.Mwaka kupigwa vita badala ya kusaidiwa kusonga mbele. Ni mwendelezo ule ule.
Aisee jana kwenye uzi wangu wa 'mimi na ka passo hadi Kigali '.kuna sehemu nilisema Tanzania ni taifa lisilo na mbele wala nyuma. duuh watu ikawauma sana, acha waniandame jana, ukweli utabaki Kuwa ukweli tu kuwa Tanzania ni taifa la ajabu sana, ukiinuka na kuonyesha uzalendo unapigwa vita ikibidi hata kuuawa, sasa hapo kuna mbele na nyuma?