Nini kilikwamisha kuhakiki vyeti vya kuzaliwa sambamba na kuhakiki vyeti vya shule?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,682
149,886
Nimemsikia Raisi akiongelea swala kutaka kuhaiki pia vyeti vya kuzaliwa kwa watumishi wa umma katika hotuba yake ya leo ili kubaini watumishi wanaodanganya umri kwa lengo la kujiongezea umri wa kustaafu.

Mimi sina kipingamizi na swala la kutaka kuhakiki pia umri wa watumishi lakini nachojiuliza ni kwanini uhakiki wa vyeti vya kuzaliwaa haukufanywa sambamba na uhakiki wa vyeti vya shule kwa watumishi wa umma?

Swala la udanganyifu wa umri ndio wamelijua leo?

Kama zoezi la kuhakiki tu vyeti vya shule limechukua zaidi ya mwaka,hili la kuhakiki vyeti vya kuzaliwa ambalo linaweza kuwa na changamoto nyingi zaidi litachukua muda gani?

Je,baada ya kuhakiki vyeti vya kuzaliwa,wataanza tena kuhakiki vyeti vya ndoa?
 
Pesa pesa zinakwenda tu bora wangetumia pesa hizo kulipa malimbikizo ya madeni ya watumishi serikalini
 
Naiona point. Birth certificate ni lazima kuhakikiwa coz kuna watu wapo lkn hawajazaliwa!
 
Hakutakuwa na ajira mpya hadi watu wahakikiwe birth cerificate zao. Na hilo zoezi litafanyika kuanzia mwaka wa fedha 2017/2018 hadi 2018/2019.

Hapo ndio utajua mwanasiasa sio mtu wa kumuamini , hata akiwa baba yako mzazi.
 
Tena zoezi hili litaenda pamoja na uhakiki wa jinsia. Kuna watu wamedanganya jinsia na wanaomba likizo ya uzazi.
Sina imani na alichokisema leo kuhusu maslahi ya wafanyakazi hadi kitakapotokea
 
Naona kwa kipind chake cha miaka mitano ataishia kuhakiki na kufukuza watu tu, kweli TZ imepata raisi mzalendo, yeye ni kutimua timua tu
 
Nimemsikia Raisi akiongelea swala kutaka kuhaiki pia vyeti vya kuzaliwa kwa watumishi wa umma katika hotuba yake ya leo ili kubaini watumishi wanaodanganya umri kwa lengo la kujiongezea umri wa kustaafu.

Mimi sina kipingamizi na swala la kutaka kuhakiki pia umri wa watumishi lakini nachojiuliza ni kwanini uhakiki wa vyeti vya kuzaliwaa haukufanywa sambamba na uhakiki wa vyeti vya shule kwa watumishi wa umma?

Swala la udanganyifu wa umri ndio wamelijua leo?

Kama zoezi la kuhakiki tu vyeti vya shule limechukua zaidi ya mwaka,hili la kuhakiki vyeti vya kuzaliwa ambalo linaweza kuwa na changamoto nyingi zaidi litachukua muda gani?

Je,baada ya kuhakiki vyeti vya kuzaliwa,wataanza tena kuhakiki vyeti vya ndoa?
Kuhakiki vyeti vya kuzaluwa ningumu kwani hata yeye mwenyewe raisi hana cheti cha kuzaluwa. Sana sana atakua anatumia afidavit.

Watu wenye kuzaliwa kabla ya 1970 hawakuwa wana pewa vyeti vya kuzaliwa, wengi wao wanakisia tu miaka.
 
Birth Certificate bado hazitoi uhakika wa tarehe ya kuzaliwa ya mtumishi. Labda kama wangeweza kupata kadi ya clinic
 
Labda wataangalia umri wa kwenye vyeti na ukomavu wa sura. Sasa wenye sura za kale kama katibu mwenezi wa chama chakavu sijui itakuwajeee..
 
Mbona kama Kuna tatizo la ufahamu nini cha kufanya kuondoa umasikini kama haielewiki
 
Mleta mada hajafuatilia hotuba nzima lakini sio kosa ,hili gumu mno kufanyika na halitafanyika.

Watumishi waanze kuchekacheka na kutabasamu wakati wote maana tumeambiwa na wataalamu wa afya kutabasamu kunaondoa makunyanzi usoni ili wasionekane wamezeeka halafu wanaenda kununua cheti safiii ningeshauri wawatumie idara ya mambo ya kale wanajua kukadiria umri sana hawakosei
 
Kuna MTU nafikri akili zake siyo timilifu! Mimi nashauri kabla rais hajaagiza kukaguliwa vyeti vya kuzaliwa tupimwe kwanza utimilifu wa akili! Na hii iwe kwa wote bila kujali wanasiasa au babake na Bashite!
 
Birth certificates tayari wakati wa zoezi lote la uhakiki pamoja na lile la vitambulisho vya taifa.. Tusubiri matokeo..
 
Nimemsikia Raisi akiongelea swala kutaka kuhaiki pia vyeti vya kuzaliwa kwa watumishi wa umma katika hotuba yake ya leo ili kubaini watumishi wanaodanganya umri kwa lengo la kujiongezea umri wa kustaafu.

Mimi sina kipingamizi na swala la kutaka kuhakiki pia umri wa watumishi lakini nachojiuliza ni kwanini uhakiki wa vyeti vya kuzaliwaa haukufanywa sambamba na uhakiki wa vyeti vya shule kwa watumishi wa umma?

Swala la udanganyifu wa umri ndio wamelijua leo?

Kama zoezi la kuhakiki tu vyeti vya shule limechukua zaidi ya mwaka,hili la kuhakiki vyeti vya kuzaliwa ambalo linaweza kuwa na changamoto nyingi zaidi litachukua muda gani?

Je,baada ya kuhakiki vyeti vya kuzaliwa,wataanza tena kuhakiki vyeti vya ndoa?
Inaweza kuwa ni sababu nyingine ya ku delay haki za watumishi.
 
Back
Top Bottom