Nini kilianza kuvunjwa, je ni amani au haki ?

Nini kilianza kuvunjwa, je ni amani au haki ?

matonyamswanu

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2025
Posts
361
Reaction score
429
Serikali, wengi wa wana CCM na baadhi ya watu,, wamesimamia upande mmoja tu.

Kutuambia tudumishe amani., amani, amani na hawana neno jingine angalau la tofauti.

Wapinzani, wanaharakati, na wadau baadhi, wamesema wanahitaji amani inayoambatana na haki.
Angalau wao, wanaona mambo yote mawili yana umuhimu.

Kumbukumbu zangu, ni kuwa Serikali ndiyo ilianza kunyima na kuvunja haki za raia.

Madaktari waliwahi kudai haki ya maslahi Bora kazini wakati wa Kikwete. Yaliyomkuta Kiongozi wao, Dr Ulimboka ni majanga mazito. Na utekaji ukaanzia hapo rasmi.

Wakati wa Loliondo gate, yaani kashta ya kuuzwa kwa mbuga ya Loliondo kwa waarabu, wakati wa Rais Ally Hassan Mwinyi, alijitokeza mwandishi mmoja anaitwa Katabalo wa gazeti la mfanyakazi. Hakuishi.

Dunia,, watawala usiwaguse wanapoharibu. Ukiwakosoa wanatumia madaraka yao kuuwa na kutesa, na kuwalazimisha raia kutunza amani iliyokwishahama kabisa mioyoni mwao.

Unamuulia mtu ndugu yake halafu unamwambia awe na amani, Kweli ????

Hiyo ni amani au kunyamaza na kukaa kimya kwa amri kama mahabusu.
 
Huwezi kujifanya ni muhubiri wa amani kipindi ambacho tu unaona hiyo amani inataka kutoweka wakati hukujari kipindi ambacho yanafanyika mambo yenye kuhatarisha amani.
 
Back
Top Bottom