Nini kifanyike kunusuru ndoa hii?

mwamba_ngori

JF-Expert Member
Aug 31, 2019
251
294
Jamani ni jambo ambalo kuamini ni shida sana ukielezwa na mke wako akifanya Hivi...

Kulikuwa na Jamaa amepanga na mke wake sasa siku moja alichukua ndoo waliyokuwa wakitumia na mke wake akaenda nayo katika mishe zake. Mke wake alipotaka Kuoga akaomba Ndoo nyingine kwa mpangaji mwingine alikuwa na yeye ni mwana ume.

Sasa baada ya Kuoga akamrudishia yule jamaa ndoo yake. Bila kujua kumbe alisahau Nguo ya ndani{ chupi} kwenye ile ndoo na Jamaa aliiona ila hakutaka kurudisha sababu alijua atakumbuka na kuifata Basi baada ya mda kidogo yule Mwanamke akafata Ile nguo yule jamaa akamwambia Ingia ndani ukachuke ndoo ipo Sebleni yule mwanamke alikuwa na Kanga moja tu.

Baada ya Kuchukua ile anatoka mlangoni tuu Mme wake anamuona anatoka kwenye nyumba ya mpangaji mwenzake na Kashikilia ile Nguo ya ndani Na Ana kanga moja Tu!! .

Mwanaume amekataaa katakata kuamin ya mke wake jeh

Nini kifanyike kunusuru ndoa hii?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwannza kongole kwa ka story ka kufirika, ambapo niliwahi kukasoma zamani kidgo. Sema kimekaa vibaya, iweje mtu huishi na mke then uwe na ndoo moja tu ya matumizi.

Kama ingekuwa na situation imetokea uhalisia ningesema haya.

Mwanamke huyo ni mpumbavu, ktk hali kama hiyo angejiongeza na kujiweka nje kumuomba na kumsisitizia jamaaa ampe, yeye ile ndooo, kwa lengo jema kabisa. Otherwise hao walikuwa wanakulana so hiyo ilikuwa ni sehem ya arobain yao, au manzi alikuwa anajilengesha atafunwe na mchizi. Hiuyo mchiz naye hajisomi au kashindwa kujiongea kuishi kwa amani.

Hakuna la kunusuru apambane na hali yake , zero brain
 
Hii stroy (yakutunga) nakumbuka niliiona miaka hiyo ya zamani enzi smartphone zinaanza kuingia mimi nilikuwa natumia Nokia Ashura nilinunuliwa na bi mkubwa kwa kufaulu mtihani wa kidato cha pili.
 
Jaman ni jambo ambalo kuamin ni shida sana ukielezwa na mke wako akifanya Hivi...

Kulikuwa na Jamaa amepanga na mke wake sasa siku moja alichukua ndoo waliyokuwa wakitumia na mke wake akaenda nayo katika mishe zake. Mke wake alipotaka Kuoga akaomba Ndoo nyingine kwa mpangaji mwingine alikuwa na yeye ni mwana ume.

Sasa baada ya Kuoga akamrudishia yule jamaa ndoo yake. Bila kujua kumbe alisahau Nguo ya ndani{ chupi} kwenye ile ndoo na Jamaa aliiona ila hakutaka kurudisha sababu alijua atakumbuka na kuifata Basi baada ya mda kidogo yule Mwanamke akafata Ile nguo yule jamaa akamwambia Ingia ndani ukachuke ndoo ipo Sebleni yule mwanamke alikuwa na Kanga moja tu.

Baada ya Kuchukua ile anatoka mlangoni tuu Mme wake anamuona anatoka kwenye nyumba ya mpangaji mwenzake na Kashikilia ile Nguo ya ndani Na Ana kanga moja Tu!! .

Mwanaume amekataaa katakata kuamin ya mke wake jeh!!

Nini kifanyike kunusuru ndoa hii.?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu tuhurumie wenzio saivi joto sana kunywa hiki kinywaji.
Ungesubiri subri hata jioni jua likiwa limepoa.
 
Hutakiwi kuumia, toa ushauri kutoka moyoni, hayo mengine ya ametunga achana nayo.

Kwa sababu huwezi kujua unaweza kuta ni kweli msaada unahitajika ila ni ujuaji wetu kumchallenge mleta mada.
Inaumiza sasa kama hii story ya kitambo leo inaombewa ushauri jamani. Ukijua na umetoa ushauri lazima uumie. Maana huu ushauri wa 2020 unaenda vipi kutatua tatizo la 2015 huko.
 
Back
Top Bottom