Nini kifanyike kuleta umoja na mshikamano wa kitaifa?

Nini kifanyike kuleta umoja na mshikamano wa kitaifa?

msovero

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2019
Posts
913
Reaction score
1,730
Ndugu Wana JF karibuni kwenye mjadala wa wazi wa kutoa maoni juu ya mambo gani yafanyiwe kazi ili kurejesha umoja na mshikamano wa kitaifa bila kujali tofauti za itikadi zetu za dini na kisiasa.

Mimi kama Mtanzania mwenzenu nashauri mambo haya;

1. Kutengwa siku maalum ya kitaifa ya kuomboleza watanzania wenzetu waliotangulia mbele ya haki katika kipindi hiki cha uchaguzi. Siku hii maalum iwe inafanyika tarehe 29 OCTOBER kila mwaka.

2. Kuundwe tume huru ya uchaguzi ambayo haiegemei upande wa chama kimoja tofauti na tume huru ya mchongo iliyopo sasa.

3. Wananchi tupewe katiba mpya inayotokana na Sisi wenyewe kwakuwa ndio hitaji letu la msingi Kwa sasa.

4. Kukomesha matukio yote ya utekaji na upoteaji wa raia Kwa sababu za kisiasa au Vinginevyo

5. Viongozi kuzingatia busara katika matamshi Yao ili kujiepusha kuchochea chuki na hasira Kwa raia

6. Vyama vyote vya siasa viwe huru kufanya siasa Kwa kuzingatia Sheria, kanuni na taratibu zilizopo bila upendeleo

7. Mahabusu wa kisiasa na vijana wote waliopo mahabusu kutokana na vurugu za uchaguzi waachiwe huru

Wewe nini maoni yako?

KARIBU TUYAJENGE ILI KULETA UMOJA WA KITAIFA PAMOJA
 
Back
Top Bottom