Nini kifanyike kuinua Tanzania yetu kimaendeleo?

kelphin

JF-Expert Member
Dec 24, 2019
9,111
14,481
Amani iwe kwenu wakuu,

Nimekuwa nikipita pita mitandaoni kuangalia nchi nyingine hasa za Afrika zilizoendelea kiuchumi, miundombinu hata kiteknolojia.

Nikafikilia je Tanzania hatuwezi kufikia huko?

Hapo juzi nilikuwa naangalia kituo kimoja cha habari.Vijana watatu wamegungundua mita fulani ya umeme (hili linahusu technology) sijajua wamefikia wapi sababu wazo lao ni zuri sana

Wengine wamebuni parking ya kisasa je wao pia wamefikia wapi!
Viongozi wamewasaidiaje kufikia lengo!

Ukitazama Kama China unakuta mtoto mdogo amegundua au kubuni kitu.Je, kwetu Tanzania tufanyaje?

Je, hatuwezi kuingiza mfumo wowote shuleni huko ukatusaidia kutengenezeka akili za watoto wetu?

Nini kifanyike kuinua Tanzania yetu kimaendeleo?



k,k


kelphin kepph
 
Huku ndo hivyo watu wakigundua wanapuuzwa.... Sijui wizara ya elimu,sayansi na teknolojia inafanya nn..kuna jamaa nasikia alitengeneza Ndege ya bati sijui ila alivyotua tu wakamkamata eti anahatarisha uhai wake.
 
Kifanyike nini kuleta maendeleo Tanzania? Kama tunataka maendeleo ya wengi Tz lazima tunyanyue kilimo chetu manake ndicho kinachoajiri zaidi 70% ya Watz.

Badaya ya kujenga daraja moja kwa TShs 700,000.000 kiasi hiki kingetosha kujenga mfumo mzima wa kilimo Tz angalau kwa kuanzia.
  • scheme za umwagiliaji
  • mashine za kilimo
  • viwanda vidogo vidogo vya uchakataji mazao
  • miundombinu ya barabara kwenye skimu za umwagiliani
  • nk
Tunapoteza fedha nyingi mno kufanya miradi ambayo haina tija kwa taifa au watu maskini. Fedha hizi zingewekezwa moja kwa moja kwenye maeneo ambayo mtanzania maskini atanufaika. Tumetumia matrillion kwenye TASAF kugawia watu 20,000/=, 100,000/= etc; hakuna ugawaji wa fedha kiasi chochote utakaowatoa watu kwenye umaskini.
 
Back
Top Bottom