Nini kifanyike ili watawala wetu wasikie kilio chetu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini kifanyike ili watawala wetu wasikie kilio chetu?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Domy, Sep 8, 2012.

 1. Domy

  Domy JF-Expert Member

  #1
  Sep 8, 2012
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 4,702
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Salaam wana JF

  Nasikitishwa sana, na watanzania wanasikitika sana na jinsi mambo yanavyokwenda ndani ya nchi yetu,

  Sasa hivi Tz imekuwa siyo nchi salama tena kwa kuishi binadamu na kufanya mambo yako kwa uhuru ingawa nchi inadai kwamba ina katiba.

  Hii siyo nchi iliyoachwa na Baba wa Taifa Mwl Nyerere, ambayo ilikuwa tanzania ni kwa ajili ya watanzania, leo imekuwa ni nchi tofauti kabisa na matarajio,imekuwa ni nchi ya mafisadi na wauaji.

  Takwimu zinaonyesha Tanzania ni miongoni mwa nchi kumi zinazoongoza kwa ukatili wa polisi duniani,watawala hakuna wanalofanya kutunusuru na hilo bali wamegeuka miungu watu wanaotamani kuabudiwa kuliko hata MUNGU mwenyewe,

  Watu wanauwawa ovyo hatusikii hata kauli ya mkuu nchi, hii maana yake nini? Tulimchagua atumike kwetu lakini amekuwa ni mtu wa masafa kila kukicha huku tukikosa majibu ya maswali yetu.

  Rais anatakiwa na wananchi wake kuunda tume huru kuchunguza mauaji ya watu,utekaji wa watu wanaodai haki matokeo yake anaweka pamba masikioni na kuvaa miwani ya mbao huku wasaidizi wake wakituambia LIWALO NA LIWE tunapelekwa wapi watanzania,

  Maisha ni magumu sana mtaani,hali ni mbaya,kuishi Tanzania sasa ni adhabu wakati tuliahidiwa maisha bora kwa kila mtanzania inawekana,matokeo ni maisha bora kwa kila kiongozi na watoto wao imewezekana,

  Tuna viongozi kama Paul chagonja huyu nae anaitwa kiongozi sijui kwa vigezo vipi,akina Kamuhanda wanaua mkoa mmoja wanahamishiwa mkoa mwingine nako wanaua wanaachia wanastarehe uraiani,tunapelekwa wapi,

  Watu wanapigwa risasi na mabomu na kufa tunaambiwa wanarushiwa vitu vizito kweli!! Damu ya kijana yule muuza magazeti ALY ZONA nani ataitetea? Damu ya MWANGOSI inatulilia ardhini tufanye nini? Watawala wanatudanganya

  mwana JF toa maoni yako nini kifanyike uwatetee watanzania wenzako wanaouwawa ovyo,Leo kwao kesho kwetu.

  Naomba kuwasilisha.
   
 2. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #2
  Sep 8, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  kama waislam walivyofanya jana nahisi hiyo ndio njia sahihi tuungane wote kwa pamoja!!!!!!!
   
 3. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #3
  Sep 8, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  Inasikitisha sana. Kwa kweli ccm MAFISADI/MAJAMBAZI/WAUAJI wametufikisha kubaya. Yote ni kwa sababu ya kuijona wao ndo binadamu kuliko wengine, na wao ndo warithi wa hii nchi hata kama wameshindwa kumhakikishia mtanzania uhakika wa huduma za kijamii. Mtanzania anazidi kutaabika kila kukicha, viongozi wa serikali ndo kwanza wanakula bata kana kwamba wao ndo miungu watu. Hawataki kukosolewa, ukiwakosoa wanatishia kukuua na hata kukuua kabisa. Nchi si shwari tena.


  Tuendeleeni kuwaelimisha watanzania, waelimike ili waling'oe madarakani li serikali la ccm MAONGO/MAJAMBAZI/MAFISADI/WAUAJI.
   
 4. Domy

  Domy JF-Expert Member

  #4
  Sep 8, 2012
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 4,702
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  mkuu watz bado ni waoga sana...,
   
 5. Root

  Root JF-Expert Member

  #5
  Sep 8, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,217
  Likes Received: 12,928
  Trophy Points: 280
  Itafika wakati wataondoka sioni umuhimu wa kuandamana wakati hujui kitacho kukuta huko mbele bora utulie tu yataisha they cant last forever itafika muda wataondoka
   
 6. Domy

  Domy JF-Expert Member

  #6
  Sep 8, 2012
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 4,702
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  hata wakati utakapofika watagoma kuondoka watatumi mtutu
   
 7. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #7
  Sep 8, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  mkuu Andybird, i understand Pride comes before a fall but what if you wont live that long to see wao hadi wakimaliza?

  -kama wanatenda ubaya na wanaujua na despite kuelezwa hawasikii kwanini tusiwa-terminate tu?

  -how many are they nasi tuko wangapi?..naona kama in total kwa TZ nzima hawafiki hata 150.

  this is what give them pride, kusema kwamba,"ngoja hadi amalize muda wake".. tukiwatoa, hata kama ni mmoja hawatakuwa na hicho kiburi mkuu.
   
Loading...